Habari wakuu,
Leo moja kwa moja kutoka bungeni, aliekalia kiti leo ni mheshimiwa mama Anna Makinda. Swali la kwanza linaulizwa na Freeman Mbowe na linahusu wizara ya afya.
Swali: Serikali ina mkakati gani kuongeza watumishi (tasnia ya afya) (Lorensia Jeremia-Bukwimba)
Jibu: Walau jitihada inaonekana kwa allocation iliofanyika
Swali: Serikali ina mkakati gani kuongeza vitetendea kazi na vifaa tiba
Jibu:Intergreted logic system itasaidia pia itakuja sheria ya kulazimisha watu kujiunga kwenye mifuko badala ya hiyari na mifuko italeta uwezo wa kununua vifaa tiba
Swali: Ukosefu wa wahudumu wa afya unapelekea wasio na ujuzi kuhudumu na wengi wanaondoka kwenda nchi nyingine (Suzan Lymo)
Jibu: Kimepatikana kibali cha kuajiri wahudumu wapya mwaka huu, mambo yanaenda vizuri japo malengo ya milenia yanaweza yasifikiwe, lakini serikali haina uwezo wa kuzuia watumishi kuhama nchi
Swali: Hospitali ya mkoa wa Mara inajengwa kwa kasi ndogo (Vincent Nyerere)
Jibu: 2011/12, 2013/14 serikali imetoa pesa za kujenga hospitali ya mkoa wa mara, zinaendelea taratibu za kumpata kandarasi wa kujenga awamu ya pili
Swali: Awamu ya kwanza iligubikwa na rushwa(Hospitali ya mkoa wa Mara), serikali itaacha lini kunyamazia watu wanaofanya vitendo hivi
Jibu: Mamlaka ya mkoa ilichukua hatua kwa kuwahusisha TAKUKURU na BRELA
Swali: Fedha za fidia hazifiki kwa wahusika katika ujenzi hospitali ya mkoa wa Mara
Jibu: Ilikua milioni 35 lakini zimeongezwa mpaka milioni 100 kutokana na revaluation(ilipita miezi sita)
Swali: Lini serikali itasikia kilio cha wanawake kukamilisha wodi ya kinamama Kilimanjaro(Grace Kiwelu viti maalumu)
Jibu: Martenity ward ni project kubwa, ni kati ya bilioni 9 na 11. Zilitengwa milioni 700 tu kwa ajili ya shughuli hiyo, lazima kuwe na namna tofauti
Swali: Mitambo ya usalama bungeni inatoa miozi, haihatarishi afya? (Shekifu)
Jibu: Haitofautiani na inayotumika duniani kote na haina madhara kwa afya na haiitajiki kutumia aina ya chakula cha ziada kulinda afya pia hupelekwa tume ya mionzi kila baada ya miezi mitatu mpaka sita kuhakiki usalama wake.
Swali: Kwanini wafanyakazi wasipewe nguo maalumu kuwazuia wasipate mionzi (Shekifu-Lushoto)
Jibu:Serikali imechukua ushauri na itaufanyia kazi
Swali: Toka sakata la escrow lianze, usalama wa wabunge umekuwa mashakani
Jibu(Makinda): Escrow haina mionzi pia inakusudiwa kujenga kijiji cha wabunge kulinda usalama wao
Swali: Vipenyo vya kuingilia nchini vinahatarisha usalama (Sanya)
Jibu: Serikali inafanya tathmini wakati wote wa usalama wa wabunge na wananchi
Swali: Zoezi la kusajili simu bado kuna tatizo, Je! zoezi hilo limesaidia nini?
Jibu: Sheria inasema ni kosa la jinai kutumia namba ambayo haijasajiliwa, zoezi limepunguza kwa kiwango kikubwa uhalifu na kuzima namba ambazo hazijasajiliwa. Ataebainika faini 500,000 na kifungo miezi mitatu na hairuhusiwi kuuza laini za simu kiholela.
Swali: Kwanini badala ya kumuazibu mwananchi, zisibaki kwenye kampuni kama Dubai na China pia India wanavyofanya?, wapi akalalamike mteja kutokana na makampuni ya simu?
Jibu:Tatizo kubwa sio kusajiliwa kwa simu lakiini ni kusajiliwa kwa vitambulisho feki, unaazishwa mfumo mpya na simu zitasajiliwa upyaUshauri umechukuliwa na kuna mpango wa kuongeza adhabuWatu kujisajili kwa majina ya watu na kufanyia uhalifu wa kuchangia, polisi hawana uwezo kudeal na cyber crimes
Utapeli kwa kutumia internet umeongezeka sana, serikali italeta sheria kubwa tatu kudhibiti utapeli kwa njia ya internet, vyombo havina uwezo wa kufatilia vizuri wizi wa mtandao lakini pia wananchi wawe waangalifu kuambiwa kuchangia kwa kutumia majina ya watu maarufu
Swali:Kutumia namba isiyosajiliwa ni kosa, Je sio kosa la jinai kuwauzia watu nyimbo ambao hawajaomba?Matha Mlacha-Singida
Jibu: Sheria inakataza kukata fedha kwa huduma ambayo mteja hajaomba au hajaitumiaKuna kituo kitakua kinapokea malalamiko kwenye makampuni ya simu
Swali: Miongoni mwa vitu vinavyoleta maendeleo ni mawasiliano, lini vijijini!
Jibu: Mfuko wamawasiliano kwa wate una lengo la kupeleka huduma ya wasiliano kwa vijiji visivyovutia mawasiliano kibiashara, inafanyika kwa hatua kulingana na fedha zinavyopatikana
Serikali imeingia mkataba maalamu na Vietel kujenga mkonga maalumu kufikia vijiji vyote ambavyo havijafikiwa na mawasiliano
Swali: Serikali inajipangaje kutumia tech ya kisasa ili wananchi wapate taarifa kwa kupitia simu zao
Serikali imefanya mpango wa kujenga mkongo wa taifa kuunganisha wilaya zote nchini, inaendeela kupeleka mkongo kwa mtumiaji wa mwisho(last user)
na kuanzisha vituo vya mawasiliano
Swali: Mkonga wa taifa umefika lakini kuna tatizo la internet pia bei za internet kwenye mkonga ni kubwa sana wastani wa 120,000 kulinganisha na 30,000 za makampuni za simu Rage
Jibu: Tatizo la Tabora ni mahsusi hivyo nitazungumza na kuona tatizo pia nampongeza Kafulila kwa kuoa na karibu kwenye chama-Makamba
Swali: Kituo cha wazee Makulandoto
Jibu: Kina jumla ya wakazi 41 kwa sasa, serikali inatambua na katika kukabiliana inaendelea kutoa huduma na inatenga fedha kuhudumia wazee wasiojiweza, ilitegwa milioni 38 ili kuendesha kituo. 2014/15 zimetengwa milioni 28 pia wizara ianatoa wito nchini kuhudumia wazee wasiojiweza katika jamii
Swali: Kwa kua kituo cha wazee Kulandoto kimeanzishwa toka 1975 na majengo yana hali mbaya, je lini serikali watajenga majengo mapya
Jibu: Ujenzi wa majengo mapya ni kutokana na bajeti ya serikali na mwaka huu 1.7 bilioni zimetengwa kwa ustawi wa jamii, fedha zikitoka itafanyiwa ukaratibati
Kuhamisha ustawi wa jamii kwa waziri mkuu, ilikua huko na tunaamini ilipo sasa ni mahala sahihi
Swali: 2008 raisi alitoa ahadi ya maji Isaka na Kagongwa leo ni mwaka sita(Ezekiel Maige)
Jibu: Katika kutekeleza ahadi ya Raisi, mshauri kashapatika na ataanda usanifu na itakamilika baada ya miezi sita.
Isaka na Kagongwa kuna tatizo la maji, pia mikutano imeshafanyika na naahidi Kagongwa tutaangalia kisima cha zamani na kukirudisha katika utendaji mapema
Swali:Kwa kua maji ya ziwa Victoria Kahama lakini mtatndao wa maji uko katikati ya mji lakini pembezoni hamna maji
Jibu: Ni mpango wa serikali kutekeleza kama walivyoahidi.
Swali: Kumekua na mfululizo wa maswali kuhusu ahadi za raisi, serilikani iliji-commit kutoa taarifa kwenye vipindi vya bunge, mbona haifanyi?(Mnyika)
Jibu: Waziri alisema atatoa ripoti na mimi nilitoa taarifa na kama kuna haja ya ripoti zaidi, niko tayari kuitoa(Maghembe)
Swali: Programu ya pili ya maji itachukua muda gani?
Jibu: Maji ni uhai, na programu ya awamu ya pili imeshaanza kutekelezwa na miradi mingi kwake imekwama
Swali: Waziri wa maji alisema pesa itapatika na halmashauri zitapelekewa peza, je ni kweli pesa zimeenda kama alivyoahidi?
jibu: Ni kweli na tutaendelea kuwasiliana na mbunge lakini ni kweli pesa zimeenda.
Swali: Raisi alitoa ahadi nyingi, ni wakati muafaka kumba radhi kwa ahadi ambzo hazijatelekelezwa
Jibu: Ahadi bado zinaendelea kutekelezwa na mda haujaisha bado.
Swali: Serikali ina mpango gani na kiwanda cha maliasili (Ngonyani)
Jibu: Serikali iliuza hisa zote na serikali haiusiki na kiwanda cha maliasili na jukumu la kulipa watumishi na la mwekezaji lakini itaendelea kuwapa malighafi
Swali: Wavuvi wengi wanakwama, kwanini serikali haiwasaidii?
Jibu: Kulingana na sheria ya uvuvi kila chombo hukaguliwa na afisa uvuvi ikiwemo vifaa vya kujiokoa, wizara kupitia vituo vya ukaguzi huwa inatoa msaada kwa wavuvi wanaokwama baharini
Serikali 2014/15 itaanza kutoa ruzuku na 2.2 Bilioni imetengwa na pesa ambayo imeshatolewa ni milioni 400 na inalenga kupata zana bora na vifaa vya kujiokolea.
Swali: Kumeibuka wizi Momba Tunduma, Je! jeshi la polisi limekabiliana nalo vipi!
Ni kweli na serikali imechukua hatua zifuatazo-kuongeza askari, kufuatilia taarifa, kukamilisha kituo cha polisi pia kufanya vikao na wananchi kuhusika katika ulinzi shirikishi. Jeshi limefanikiwa kuvunja mtandao wa polisi na si sahihi jeshi la polisi halichukui hatua
Swali: Wananchi wametaja baadhi ya askari kuhusika (Silinde)
Jibu: Naomba orodha ya askari waliohusika nichukue hatua.
Swali: Umuhimu wa dawati la jinsia katika jeshi la polisi, (Kikombe-viti maalumu)Jibu: Serikali inatambua umuhimu dawati la jinsia japo haijafikia nchi nzimalakini inajitahidi
Wageni
Wageni wanatambuliwa, kuna wageni wa Hussein Mwinyi kutoka jeshi, wageni wa Kiboma, wageni 25 wa Lerensia Bukwimba, wageni wa Ezekiel Wenje, wageni 15 wa Amina wakiongozwa na Ibrahim, wageni waliokuja kwa ajili ya mafunzo, sabini kutoka St. John, wanafunzi kutoka UDOM.
Matangazo ya kazi:
Mwnyekiti wa kamati ya ardhi, James Lembeli leo tar 24 kutakua na kikao cha kama jengo la utawala
Komba anawatangazia wanakamani maendelea ya jamii kutakuwa na semina baada ya bunge kusitishwa mchana Pius Msekwa
Mbatia: Naomba kuwasilisha hoja, ofisi yako ilipokea ripoti maalamu kuhusu Escrow na umiliki. Taarifa hii ilikua siri mpaka itakapowasilishwa bungeni na turiarifiwa taarifa ya PAC haijakamilika na tumepata taarifa ripoti hio inagawiwa kama njugu na baada ya kutoa taarifa polisi wamefanikiwa kumkamata mtu mmoja na inavyoonekana taarifa hio imeibiwa na ina muhuri wa katibu mkuu na kwa mujibu wa maelezo taarifa hio imeibwa.
Katiba ya jamhuri 1977 linaainisha bunge lina mamlaka ya kusimamia fedha za umma, kitendo cha kusambazwa mitaani wakati bado haijatolewa rasmi inadhiirisha kuna watu wamejipanga kushusha heshima ya bunge. Kwa kua kumekua na jitihada nyingi zinazolenga kuzuia bunge kushindwa kufanya kazi yake, kwa kutumia kanuni ya 51 naomba kutoa hoja bunge lisitishe shughuli zake za sasa na kujadili ripoti hio
Makinda: Hamna hoja hapo na kaeni msome kifungu cha 51, ofisi ya bunge imeshirikiana na polisi ili muhusika asitoke mpaka aeleze mshine gani zimetumika naikithibitika amefanya atapata kifungo cha miaka mitatu. Tukipata taarifa ya polisi tutachukua hatua na hamna ubabe hapa ninaoufanya.
Order paper imebadilishwa hivyo litajadiliwa humu ndani, nchi inaendeshwa kwa taratibu na kazi inaendelea hivyo hatuwezi kujadili kitu ambacho hakijaishwa.
MIONGOZO MINGI SANA
Mnyaa: Jambo aliloliomba mbatia na mjadala huu ni mpana na halihusiani tu na kusambazwa nyaraka na wengi wameshachafuliwa ikiwemo na wewe kuchukua dola 1,000,000/=, kwa heshima tunaomba uruhusu mjadala huu angalau kwa nusu saa.
Tundu Lissu: Mheshimiwa spika, nashukuru kwa fursa na kwa kuwa ni suala la kikanuni, ni vizuri turidhike kama huja ya Mbatia ina haja kujadiliwa ama laa. Kanuni ya 51: Umeridhika na hili suala na ndio maana umempa nafasi Mbatia, tunajadili yanayotokea na vizuri jambo lizungumzwe ili hii hali isafishwe.
Makinda: Naheshimu profession yako lakini pia na wewe uheshimu taratibu, polisi wanaendelea na wakimaliza spika atapanga.
Ole Sendeka: Kamati itawasilisha lakini jambo hili jambo hili linahitaji kutendewa haki, nna mashaka, bunge litapata muda gani kusoma ripoti. Ripoti ipatikane kwa wabunge rasmi ili siku ya kuwakilisha tuweze kujadili
Makinda: Tunafanya utaratibu mpate ripoti mapema
KUPIGA KURA(AZIMIO LA BUNGE KUZUIA DHIDI YA USALAMA WA MIONDOMBINU ILIYOJENGWA CHINI YA BAHARI)
Ndiyooo(Azimio limepita)
Miswada ya serikali, muswada ya sheria ya marekebisho mbalimbali
KUCHANGIA MUSWADA
Mbaruk: Maoni yangu ni vipengele vilivyoondolewa, mapendekezo ya mabadiliko ya muswada wa mbolea, ni vizuri kumshirikisha mkulima. Iwapo supplier anatoa mbolea ilio chini ya kiwango atapigwa faini na wakala lakini katika sheria pia mkulima aweze kudai iwapo mazao yataharibika kutokana na mbolea isiyokidhi kiwango. Nashukuru
Murtadh Mangungo: Pamoja na maelezo mazuri yaliyotolewa na mwanasheria mkuu wa serikali, Kifungu cha 36/3 inampa mamlaka waziri kufanya uteuzi wa waguzi wa mengi, ningependekeza ungezeko wawe wanatangzwa kuondoa mkanganyiko, Sheria pamoja na uzuri lakiniKiwango cha faini (100,000,000-500,000,000) hakina mantiki hasa kwa maeneo ya vijijini ambapo mbolea ambayo wakala anayo inaweza usifikie hata hio milioni 100, sheria iweke mkazo kwa waagizaji, uwepo ukaguzi wa kutosha na isije kuwaingiza mawakala katika mtego.
Wanaothibitisha ubora ni TBS, wenzetu wanaodhibiti magonjwa waangalie vizuri kabla haijamfikia mlengwa. Kutoza faini kwa waagiza mbegu ambazo hazifai mpaka milioni 8, mara nyingine mbegu kutoota husababishwa na matumizi hivyo watumiaji pia waangaliwe. Sheria ya bodi ya ugavi, bodi inaweza kuanzisha kamati zisizozidi tatu lakini hazijawekewa ukomo ni wa muda gani hivyo ukomo utamkwe na sheria.
Ahadi ya waziri mkuu kuleta sheria itayoweka sawa sheria ya kazi, sheria imekuja lakini hamjaileta na hatujui mkutano unaofata utakuwa lini ni linatakiwa kufanyika kabla ya January. Serikali iweke utaratibu mzuri watu wote wapate mkopo ikiwemo watu wa stashahada, hatuwezi kujenga kada moja tu ya shahada.
Mnyika: Sehemu ya 33 ya sheria hii ambayo inafanya marekebisho ya sheria ya maji safi na maji ----, marekebisho yanafanya sheria hii itumike jiji la Dar es Salaam. Kuingiza marekebisho hakukidhi kiu kuondoa mgongano, kero ya maji Dar ni kubwa mno na miradi ilioanzishwa ina migogoro mikubwa na kuingiza maneno haya pekee hakukidhi kuondoa udhaifu uliopo katika miradi ya maji.
Ningependa kupata tamko la serikali, ni kwanini serikali ilikataa hoja binafsi ya maji na kulidanganya bunge kuwa mambo yote katika utekelezaji wakati kuna mgongano, raisi aliahidi kuitisha kikao kinachowahusu mamlaka zote zinazohusiana na maji Dar es Salaam, naomba kauli ya waziri mkuu ni lini ahadi hii itakamilika. Kwa mujibu wa hotuba ya kambi rasmi ya upinzani(anaeleza), mwanasheria mkuu wa serikali ameondoa sehemu zote za sheria ambayo aliyaleta kwa manufaa ya kumpa yeye mamlaka ya kuingilia taasisi mbali mbali lakini hakutoa sababu, katika majumuisho alisema atakuja kusema sababu. Kitovu cha maombi haya ni kesi mbalimbali hasa zilizoko ndani ya TANESCO na benki kuu.
Niliweka taarifa kuwa ESCROW ni mali ya umma na kuomba pesa zisitolewa mpaka mgogoro utapoisha, katika taarifa ya serikali katika kipindi kifupi zimetumika 60.9 kulipa kampuni ya uwakili ya Mkono na serikali imesema kuna mianya inayohitaji kuchunguzwa. Wakati yanalipwa ofisi ya mwanansheria mkuu ama inaridhia au inakaa kimya.
Tunaomba ofisi ya mwanansheria mkuu inaendelea kusema uongo bungeni. Ni hatua gani serikali imechukua pale ambapo kuna mgongano wa maslahi na mianya ya rushwa. Kuna taarifa kuwa mtuhumiwa atawahishwa mahakamani ili yaje kukingwa hapa kwa kusingizia haya mambo yako mahakamani, kiti chako kitahusishwa na maharamia.
Wanafunzi hawatapata mkopo kwa sheria kutobadilishwa, kwa sababu watadai bilioni 12. Rudisheni fedha za umma ili wanafunzi wote wapate mkopo.
Wizara(Elimu): Muswada unaohusu marekebisho wa bodi wa mikopo umeondolewa, wakati wizara inasoma makadirio katika fungo la HESLB, kazi kubwa ya Heslb ni kuwakoposha wanafunzi wa elimu ya juu 95,000. Baada ya hapo itakopesha makundi ya walimu wa stashahada ya ualimu wa hisabati na sayansi, makundi ya sekondari na shule za msingi
SHUGHULI ZA BUNGE ZIMEAHIRISHWA MPAKA SAA KUMI NA MOJA JIONI
0 comments:
Post a Comment