UCL: Chelsea sio watu wazuri, hiki ndicho walichomfanya kocha aliyewapa ubingwa
Katika mechi zote zilizochezwa usiku wa jana – inawezekana mechi kati ya Chelsea dhidi ya Schalke ndio mchezo uliokuwa umetaliwa na hisia nyingi kutokana na historia iliyopo kati ya wachezaji, mashabiki wa Chelsea na kocha wa Schalke Roberto Di Matteo.
Mchezo huo uliochezwa nchini Ujerumani kwenye dimba la Gelsenkirchen ulikuwa muhimu kwa timu zote ili kujihakikishia matokeo chanya na kuweza kufuzu kwenda hatua ya pili ya michuano hiyo – hatua ya 16 bora.
Huku mashabiki wa Chelsea wakiwa wanamshangilia kwa kuimba jina lake kocha Roberto Di Matteo, ambaye aliipa Chelsea ubingwa wa kwanza wa ulaya mwaka 2011, – aliishuhudia timu yake ikipokea kipigo kizito kutoka kwa vijana wa Jose Mourinho.
John Terry alifunga goli la haraka zaidi kwa Chelsea katika michuano ya ulaya – dakika ya 2, Willian akaongeza la pili dakika 29, kabla ya Kirchhoff akajifunga dakika moja kabla ya mapumziko. Kipindi cha pili Didier Drogba na Ramires wakapigilia misumari ya mwisho kwenye jeneza la Schalke na kuiwezesha Chelsea kufuzu hatua ya 16 bora .
Timu zilipangwa hivi:
SCHALKE (4-2-3-1): Fahrmann
4; Uchida 6, Santana 5, Neustadter 5, Howedes 5; Kirchhoff 4 (Clemens
46, 5), Hoger 6; Choupo-Moting 6.5, Boateng 4 (Meyer 64, 5), Aogo 5;
Huntelaar 5. SUBS NOT USED: Wetkio, Fuchs, Friedrich, Clemens, Sane, Meyer, Barnetta.
BOOKINGS: Hoger
MANAGER: Roberto di Matteo 5.
CHELSEA (4-2-3-1):
Courtois 6; Ivanovic 6, Cahill 6, Terry 6, Azpilicueta 6; Fabregas 7
(Schurrle 78, 6), Matic 7; Willian 7.5, Oscar 7 (Ramires 75, 6), Hazard
7; Costa 7 (Drogba 66, 6). SUBS NOT USED: Cech, Luis, Zouma, Ramires, Mikel.
BOOKINGS
MANAGER: Jose Mourinho 8.
0 comments:
Post a Comment