LAVEDA KURUDI TENA BBA
MWANADADA aliyewakilisha Tanzania katika shindano la BIG BROTHER 2014 ‘HOTSHOTS’ nchini Afrika Kusini. Irene Neema Vedastous 'La Veda' ameitwa tena ili kushuhudia fainali za kinyang’anyiro hicho.
Mrembo huyo amepanda pipa juzi saa 8 mchana kuelekea Sauz ambapo atakaa kwa muda wa wiki moja.
Akizungumza na mwandishi wa tovuti hii, La Veda alisema ameitwa Sauz
japo bado hajajua anaenda kufanya nini hasa japo anaamini hataingia
kwenye jumba la BBA kama mshiriki.
‘’Nimeitwa BBA ila si kwa maana ya kushiriki bali kama mmoja wa
washiriki ili kushuhudia fainali za BBA zinazotegemea kufanyika hivi
karibuni.
Ninafurahi kwa sababu nitakutana na washiriki wenzangu, kama
nikibahatika kupata nafasi ya kuimba, wimbo wangu mpya wa LET IT GO,
nitafanya makubwa sana maana muda mwingi na akili yangu nimeviwekeza
kwenye muziki, nitakuwa Sauz kwa wiki moja kisha nitarejea nyumbani
kujipanga zaidi kimuziki" Alisema La Veda.
Aidha La Veda amemtakia kila la heri mshiriki mwenzie Idris Sultan
ashinde na amewaomba Watanzania kumuombea kwani ushindi wake ni ushindi
wa Watanzania wote.
0 comments:
Post a Comment