'Wajiuza’ kwa kukosa mikopo ya elimu

By
Advertisement

Rais wa Serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha UDOM Masatu Kyabwene amekiri kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu Dodoma kujihusisha na biashara ya ukahaba kutokana na kukosa mikopo.
 “Kuna baadhi ya wanafunzi chuoni kwangu wana maisha magumu sana kutokana na kukosa mkopo,wakati mwingine wananifuata mimi na kunielezea shida zao ili niwasaidie,wengine ni yatima hawana baba wala mama wa kuwalipia ada,siyo siri maisha ya wanafunzi hawa ni magumu sana”amesema.

Nini maoni yako kuhusu jambo hili?

 Hata hivyo, ujio wa vyuo vikuu hasa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), unatajwa na watu wengi kuwa kichocheo cha kuongezeka kwa wanawake wanaofanya kazi ya kuuza miili yao.
 Wateja wao ni wengi lakini katika kundi hilo wanasiasa nao wanatajwa kuwa miongoni mwa wateja wazuri wa wanawake hawa ambao wengi ni wa umri wa makamu. Madai yaliyopo ni kuwa makahaba wengi ni wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu vilivyopo mjini Dodoma.
 Wanafunzi na ukahaba
 Rais wa serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Masatu Kyabwene anakiri kuwapo kwa idadi kubwa ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu mkoani Dodoma wanaojihusisha na biashara ya ukahaba. Anasema hali hiyo inatokana na  maisha magumu ya chuoni baada ya wengi kukosa mkopo.
 Ameitoa kauli hiyo akizungumza na gazeti hili kufuatia taarifa za kuwapo kwa idadi kubwa ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma kujihusisha na biashara ya ukahaba katika kumbi mbalimbali za starehe mjini hapa.
 “Kuna baadhi ya wanafunzi chuoni kwangu wana maisha magumu sana kutokana na kukosa mkopo, wakati mwingine wananifuata mimi na kunielezea shida zao ili niwasaidie,’’ anaeleza.
Anaongeza: “ Wengine ni yatima, hawana baba wala mama wa kuwalipia ada, siyo siri maisha ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu ni magumu sana.”
 Anasema hawezi kukataa moja kwa moja tuhuma hizo au kuzikubali moja kwa moja, lakini akakiri kuwepo kwa baadhi ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu wanaojihusisha na biashara ya ukahaba.
 “Hizi taarifa hata mimi ninazo, lakini siwezi kuzikubali moja kwa moja au kuzitataa moja kwa moja kwa sababu pindi vyuo vinapofungwa, kunakuwa na idadi ndogo  ya wasichana wanaojiuza katika kumbi za starehe, lakini vyuo vinapofunguliwa idadi yao huongezeka,” anasema na kuongeza:
 “Kuna baadhi ya wasichana mjini hapa  wanaofanya biashara ya kujiuza miili yao na kujifanya ni wanafunzi wa Udom ili waonekane ni wa thamani na waweze kupata fedha nyingi kutoka kwa wateja wao.”
 Anasema anachojua wanaofanya kazi hiyo si wanafunzi wa Udom, bali pia wanafunzi kutoka vyuo vingine vilivyopo mkoani humo.
 Wanafunzi na mikopo
 Hivi karibuni Mwenyekiti Taifa wa Jumuiya ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya Juu nchini (Tahliso) Musa Mdede alisema zaidi ya nusu ya wanafunzi waliodahiliwa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu nchini wamekosa mkopo kutoka B
odi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB) nchini.
Mdede alisema  jumla ya watahiniwa 58,037 walitakiwa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu nchini lakini kati yao ni wanafunzi 30,000 tu ndiyo waliopata mkopo.
 Wanafunzi  28,000 wameshindwa kujiunga na vyuo kwa  kukosa mkopo, huku  wengine wakiamua  kujisomesha na hivyo kuishi maisha magumu vyuoni.
 Uongozi wa Udom
 Mdede alisema  jumla ya watahiniwa 58,037 walitakiwa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu nchini lakini kati yao ni wanafunzi 30,000 tu ndiyo waliopata mkopo.
 Wanafunzi  28,000 wameshindwa kujiunga na vyuo kwa  kukosa mkopo, huku  wengine wakiamua  kujisomesha na hivyo kuishi maisha magumu vyuoni.
 Uongozi wa Udom
 Mara kadhaa uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma umekana kuwa wanafunzi wake wanajihusisha na vitendo vya ukahaba.
 Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Idrisa Kikula aliwahi kuzungumza na gazeti hili na kusema kuwa alipolisikia suala hilo kwa mara ya kwanza, alishtuka na kushindwa kuamini kuwa mtoto wa kike aliyejitahidi hadi kufika chuo kikuu anaweza   kugeuka kuwa kahaba.
“Nililisemea na nitaendelea kulisemea suala hilo nikipata fursa, makahaba sio wanafunzi wa Udom bali hutumia jina la chuo kuvutia wateja wao,” anasema na kuongeza kuwa yeye mwenyewe alishafanya utafiti kubaini madai hayo.
Anasema: “Wakati fulani nilikutana na wasichana wawili pale Dodoma Hotel, nilikuwa nimesimama karibu ya. Nilisikia wakimwambia mtu mmoja jirani yangu kuwa wao ni wanafunzi wa Udom.”
Anaongeza: “Alipoondoka yule mtu niliwapa kinywaji wasinishtukie. Niliwauliza wanasoma kozi gani, wakaangaliana na mmoja akajibu bado hawakuwa wamepangiwa masomo na uongozi wa chuo. Nilipowahoji zaidi walicheka na kujibu sio wanafunzi.”
 “Hapa unapata picha gani?  makahaba hawa wanaona fahari kubwa kujifanya wanafunzi, ukweli ni kwamba sio wanafunzi wa Udom,”anasema Profesa Kikula  na kuongeza kuwaameshakutana na matukio ya aina hiyo zaidi ya mara nne na mara zote wahusika walijitambulisha kama wanafunzi.
Rais wa Serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha UDOM Masatu Kyabwene amekiri kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu Dodoma kujihusisha na biashara ya ukahaba kutokana na kukosa mikopo.
“Kuna baadhi ya wanafunzi chuoni kwangu wana maisha magumu sana kutokana na kukosa mkopo,wakati mwingine wananifuata mimi na kunielezea shida zao ili niwasaidie,wengine ni yatima hawana baba wala mama wa kuwalipia ada,siyo siri maisha ya wanafunzi hawa ni magumu sana”amesema.
Nini maoni yako kuhusu jambo hili?


0 comments:

Post a Comment

Pages