MKE KUMCHUNA MUMEWE, IPO SANA!

By
Advertisement


NIJumanne tena, naamini wapenzi wasomaji wa safu hii mpo vizuri sana. namshukuru Mungu kwa hilo kwani bila yeye sisi si lolote!Leo mada yangu imesimama kwenye ndoa kwamba, mke anaweza kumchuna mume wake?
MAANA YA NENO KUCHUNA

Kwanza ni muhimu kujua matumizi ya neno ‘kuchuna’. Ni neno lililojipatia umaarufu mkubwa kwenye jamii katika miaka ya hivi karibuni.
Mara zote neno hili hutumiwa na wanawake wanaoalikwa na wanaume ambao si wa kwao. Katika mialiko hiyo ambayo sehemu kubwa ni baa, mwanamke anaponunuliwa pombe na chukula na baadaye kupewa nauli na fedha za matumizi, wenyewe husema ‘wamechuna.’…
NIJumanne tena, naamini wapenzi wasomaji wa safu hii mpo vizuri sana. namshukuru Mungu kwa hilo kwani bila yeye sisi si lolote!Leo mada yangu imesimama kwenye ndoa kwamba, mke anaweza kumchuna mume wake?
MAANA YA NENO KUCHUNA
Kwanza ni muhimu kujua matumizi ya neno ‘kuchuna’. Ni neno lililojipatia umaarufu mkubwa kwenye jamii katika miaka ya hivi karibuni.
Mara zote neno hili hutumiwa na wanawake wanaoalikwa na wanaume ambao si wa kwao. Katika mialiko hiyo ambayo sehemu kubwa ni baa, mwanamke anaponunuliwa pombe na chukula na baadaye kupewa nauli na fedha za matumizi, wenyewe husema ‘wamechuna.’ Mwanaume wa kuchunwa huitwa buzi.
Lakini si kwa mwanamke kualikwa baa tu, hapa mwanaume anapokuwa na mwanamke ambaye si mkewe na  anampa pesa za matumizi mbalimbali huitwa buzi kwa hiyo anakuwa anachunwa.
Kwa maana hiyo, sifa ya mwanaume kuchunwa ni kuwa na mwanamke ambaye si mke wake. Kwa sababu mwanamke huyo atakuwa anahitaji fedha tu kutoka kwa mwanaume huyo huku akijua ana mke wake.
TURUDI KWENYE MADA
Nimefanya utafiti nikabaini kuwa, wapo wanawake ambao nao huwachuna waume wao. Kwa hiyo naweza kusema mke naye anaweza kumfanya mumewe buzi!
KWA NINI?
Imezoeleka kuwa, mke ni msaidizi wa mume kimawazo katika maisha nikimaanisha na kuijenga familia. Ili maisha ya mwanaume yawe bora ni lazima mawazo ya mkewe yawepo. Ndiyo maana wanaume wengi huweza kununua kitu cha thamani ndani kwa sababu ya kuhimizwa na mke wake kwa kumpigia kelele kila siku. Ili kuepusha kelele hizo, mume anaamua kutafuta pesa kununua kitu hicho.
Tabia hii husababisha hatua katika maendeleo ya kila siku. Na hali hii hutokea hata kwenye mahitaji yake mwanaume. Wapo ambao wanapigiwa kelele kununua nguo zao, kununua viatu na mambo mbalimbali zikiwemo simu nzuri.
WAPO HAWA
Wapo baadhi ya wanaume wanapenda sana wakishapata pesa kumalizia baa kwa kunywa pombe lakini wapo pia ambao wakishapata fedha hizo hukimbilia kuziacha kwa mkewe na nyingine kuwa nazo mwenyewe kwa ajili ya matumizi binafsi.
Na baadhi ya wanawake hao sasa, wapo ambao wakishapewa fedha na waume zao nao huanza kutapanya kwa matumizi binafsi kama kwenda saluni, kununua vitenge vingine hata kama anavyo na siku mbili tatu husema pesa zimekwisha.
Lakini pia wapo wanawake ambao wakishapewa fedha hubana matumizi ili nyingine afanyie mambo yake ya siri kama kununua kiwanja na kujenga nyumba au kuwatumia wazazi wake wajenge, wanunue mashamba au kufanyia shughuli nyingine yoyote ya maendeleo.
NINAOWASEMA MIMI SASA
Wanawake hawa wa kundi la mwisho ndiyo hasa ninaowasema mimi. Kwamba, anaishi na mume lakini kila senti anayopewa anabana ili akafanyie maendeleo yake kwa siri mumewe asijue!
Inapotokea ameona mumewe ana pesa nyingi yupo radhi amwambie waende bichi wakatumbue maisha kuliko kumwambia anunue viatu au aongeze mashati.

Itaendelea wiki ijayo.

0 comments:

Post a Comment

Pages