BSS: MADAM RITA ALIA NA BASATA

By
Advertisement

BSS: MADAM RITA ALIA NA BASATA

Stori: Mwandishi wetu
MKURUGENZI wa Benchmark Production, Madame Rita Poulsen, amelia na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), chombo cha serikali kinachosimamia utamaduni kwa ujumla, akilielezea kuwa halina msaada wowote kwa shindano la kutafuta na kuibua vipaji vya wasanii wa muziki nchini, linalofahamika kama Bongo Stars Search (BSS).
Mkurugenzi wa Benchmark Production, Madame Rita Poulsen.
“Tunalipa fedha BASATA kwa ajili ya shindano, tunatoa ajira nyingi kwa vijana na…
Stori: Mwandishi wetu
MKURUGENZI wa Benchmark Production, Madame Rita Poulsen, amelia na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), chombo cha serikali kinachosimamia utamaduni kwa ujumla, akilielezea kuwa halina msaada wowote kwa shindano la kutafuta na kuibua vipaji vya wasanii wa muziki nchini, linalofahamika kama Bongo Stars Search (BSS).
Mkurugenzi wa Benchmark Production, Madame Rita Poulsen.
“Tunalipa fedha BASATA kwa ajili ya shindano, tunatoa ajira nyingi kwa vijana na kubadili maisha yao, wasanii tunaowaibua ndio hao hao wanaotumika katika shughuli nyingi za Serikali, lakini ajabu, hatuna msaada wowote tunaopata toka kwao, ikifika fainali wanataka tiketi nyingi za bure (complimentary), lakini tuliposhindwa kulifanya hili shindano mwaka jana, hata simu tu ya kutuuliza sababu, au hata salam hatupati,” alisema Rita.
Shindano la BSS halikufanyika mwaka jana kutokana na wadhamini kushindwa kutoa taarifa mapema ya kutoendelea na udhamini wao, lakini mwaka huu, Rita Paulsen amesema watafanya kila wanachoweza kuhakikisha linafanyika.

0 comments:

Post a Comment

Pages