Msimamizi
wa bodi ya michezo ya kubahatisha,Mrisho Millao(kulia)akiandika namba
ya Hynes Petro Kanumba (20) Mkazi wa kijiji cha Inyonga mkoani Rukwa
aliyeibuka mshindi wa Shilingi Milioni 10/- katika droo ya nane kupitia
promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,wengine
katika picha kutoka kushoto Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni
hiyo,Matina Nkurlu na Meneja uhakiki wa mapato Vodacom Zakaria
Kamweru.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda
15544.…
Msimamizi
wa bodi ya michezo ya kubahatisha,Mrisho Millao(kulia)akiandika namba
ya Hynes Petro Kanumba (20) Mkazi wa kijiji cha Inyonga mkoani Rukwa
aliyeibuka mshindi wa Shilingi Milioni 10/- katika droo ya nane kupitia
promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,wengine
katika picha kutoka kushoto Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni
hiyo,Matina Nkurlu na Meneja uhakiki wa mapato Vodacom Zakaria
Kamweru.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda
15544.
Meneja
Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akiongea na
mshindi wa shilingi Milioni 10/- Hynes Petro Kanumba (20) Mkazi wa
kijiji cha Inyonga mkoani Rukwa,aliyeibuka na ushindi huo katika droo ya
nane kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom
Tanzania,kushoto ni Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha,Mrisho
Millao na Meneja wa huduma za ziada wa kampuni hiyo Mathew Kampambe.Ili
mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
Meneja
Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akiongea na
waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusiana na mshindi wa shilingi
Milioni 10/-Hynes Petro Kanumba (20) Mkazi wa kijiji cha Inyonga mkoani
Rukwa,aliyeibuka na ushindi huo katika droo ya nane kupitia promosheni
ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni hiyo,kushoto ni Msimamizi wa
bodi ya michezo ya kubahatisha,Mrisho Millao na Meneja wa huduma za
ziada wa kampuni hiyo Mathew Kampambe.Ili mteja kujua kama ameshinda
anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
Mkazi wa kijiji cha Inyonga Mkoani Rukwa Hyness Petro Kanumba (20)
leo ameibuka mshindi wa kwanza wa Milioni 10 katika droo ya nane ya
promosheni ya Jaymilions inayoendeshwa na kampuni ya mawasiliano ya
Vodacom Tanzania.
Hyness ambaye ni mama mwenye mtoto mmoja pia
mkulima amesema kuwa amepokea taarifa hizo kwa furaha akiwa shambani
katika kazi zake za kilimo, kwa kuwa anaamini Mungu amemuona na kwa
ushindi huu utabadilisha maisha yake kwa kiasi kikubwa.
“Kwa muda
mrefu nimekuwa nikihangaika na kazi za kilimo na kukumbana na
changamoto nyingi kama vile ukosefu wa masoko ya mazao ,pembajeo za
kisasa .Kwa ushindi huu naamini nitaboresha shughuli zangu za kilimo
ikiwemo kuanzisha biashara ndogo na kuboresha makazi yetu,nashukuru
Vodacom kwa kuanzisha promosheni hii”.Alisema Hynes kwa furaha.
Akiongea
muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi,Meneja Uhusiano wa Umma wa
Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu amempongeza mshindi na kuwahimiza wateja
wote wa Vodacom kuchangamkia promosheni hii kwa kuhakikisha wametuma
neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza nafasi zao za kushinda.
Alisema
kuwa tangu promosheni hii ianze mapema mwezi huu tayari wateja watano
wamejishindia shilingi milioni moja kila mmoja na maelfu wengine
tayari wamejishindia muda wa maongezi.
“Promosheni hii itadumu
kwa muda wa siku mia moja hivyo leo ni droo ya nane hivyo bado kuna
mamilioni ya fedha yamewasubiri watanzania,wanachopaswa kufanya ni
kuhakikisha kila siku wameangalia kama namba zao zimeibuka kwenye droo
ya siku kwa kutuma neno Jay kwenda namba 15544. Promosheni hii
inayoendelea ya Jaymillions inawahusisha wateja wote wa Vodacom,kiasi
kikubwa cha fedha kitaendelea kutolewa kila siku na ni rahisi kabisa
kila mtu kushiriki. Mara tu ujumbe huu unapotumwa, mteja atapokea ujumbe
mfupi utakaomjulisha kama ameshinda na ikiwa hajashinda siku hiyo
atajulishwa hivyo na kuambiwa ajaribu tena siku inayofuata. Kila SMS
itagharimu Sh. 300/- tu”.Alisema.
Vodacom imepanga kutoa mshindi
mmoja wa Sh. 100m/-, washindi kumi wa Sh. 10m/- na washindi thelathini
wa Sh. 1m/- KILA SIKU kwa siku mia moja! Pia washindi elfu kumi
watapokea muda wa maongezi wa bure wenye thamani ya Sh. 1000/-
MWISHO
0 comments:
Post a Comment