CHRISTIAN BELLA 'KING OF THE BEST MELODIES' AAHIDI MAKUBWA SHOO YA VALENTINE'S DAY, DAR LIVE
Staa huyo ameyasema hayo hivi punde wakati wa mkutano na wanahabari wa vyombo mbalimbali uliofanyika katika ofisi za Global Publishers.
Bella amesema atakuwepo ndani ya kiwanja hicho mapema kuanzia saa 7 mchana na atapiga picha za red carpet na mashabiki wake watakaohudhuria sambamba na kuzungumza nao mawili-matatu.
Mbali na kuwahi ukumbini, Bella amewaandalia nyimbo zake zote kali za mapenzi kama vile Msaliti, Safari Siyo Kifo, Nakuhitaji pamoja na wimbo bora uliofunga mwaka wa Nani Kama Mama.
Kuonyesha kuwa utakuwa Usiku wa Wapendanao, Bella amewaandalia mashabiki wake zawadi ya wimbo mpya uitwao NASHINDWA ambao atauchia kwa mara ya kwanza huku video akienda kuifanyia nchini Afrika Kusini wiki ijayo.
Mbali na Bella usiku huo ambao ni maalum kwa wapendanao, mkali wa muziki wa Mwambao, Mfalme Mzee Yusuf naye atakuwepo katika kuwaburudisha mashabiki wote watakaokuwepo ukumbini hapo.
Usiku huo Mzee Yusuf atashuka na kundi lake la Jahazi Modern Taarab na kuangusha ngoma zake zote kali za mapenzi kama vile My Valentine, Wapendanao, Tiba ya Mapenzi, Wasiwasi Wako pamoja na hii ambayo ni habari ya mjini kwa sasa ya Mahaba Niue.
0 comments:
Post a Comment