JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
________
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI (PAC)
_________________
TAARIFA YA KAMATI KUFUATIA MATOKEO YA UKAGUZI
MAALUM WA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA
SERIKALI KATIKA AKAUNTI YA TEGETA ESCROW ILIYOKUWA
KATIKA BENKI KUU YA TANZANIA
OFISI YA BUNGE
S.L.P 941
DODOMA NOVEMBA 2014
1
1.0 UTANGULIZI
1.1 Chimbuko la Hoja ya Ukaguzi Maalum wa Akaunti ya
Tegeta ESCROW kwa Upande wa Bunge
1.1.1 Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za
Mashirika ya Umma (POAC) kwa Mwaka wa Fedha
2009/2010
Mheshimiwa Spika, kuwasilishwa kwa Hoja inayohusiana na
Akaunti ya Tegeta ESCROW kwa mara ya kwanza ndani ya Bunge
lako Tukufu, kulitokana na kuwasilishwa kwa Taarifa ya Mwaka ya
iliyokuwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma
(POAC) kwa Mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2010.
Mheshimiwa Spika, kuwasilishwa kwa hoja hiyo Bungeni
kulitokana na Kamati ya POAC kuchambua na kujadili Taarifa ya
Hesabu zilizokaguliwa za Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa Mwaka
wa fedha ulioishia Juni 30, 2009. Mojawapo ya Hoja ya Ukaguzi
kwa mwaka husika ilikuwa ni uendeshaji wa Akaunti ya Tegeta
2
ESCROW ambapo Kamati ilifahamishwa kuwa Kampuni ya IPTL
ilikuwa chini ya ufilisi na hivyo kulikuwa na uwezekano wa fedha
katika Akaunti hiyo kutolewa na kulipa madeni ya IPTL wakati wa
ufilisi.
Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa hiyo, Kamati ya POAC
iliwasilisha Bungeni pendekezo la kuzuia utoaji wa fedha katika
Akaunti ya Tegeta ESCROW hadi hapo migogoro yote kati ya
TANESCO na IPTL itakapotatuoliwa kwa maslahi mapana ya Taifa
na baada ya migogoro hiyo kupatiwa ufumbuzi fedha zilizokuwa
kwenye Akaunti hiyo ndio pekee zitumike kulipa madeni ya IPTL.
1.1.2 Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za
Serikali (PAC) na Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu
Mheshimiwa Spika, tarehe 16 Machi, 2014 Kamati ya PAC
ilikutana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Katibu Mkuu wa
Wizara ya Fedha pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali kwa ajili ya kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Agizo
lililotolewa na iliyokuwa Kamati ya POAC mwaka 2009 kuhusu
3
matumizi ya fedha zilizokuwemo kwenye Akaunti ya Tegeta
ESCROW wakati wa kulipa madeni ya IPTL.
Mheshimiwa Spika, katika kikao hicho pamoja na mambo
mengine, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania aliiarifu Kamati kuwa
fedha zilizokuwemo kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW
zimetolewa na kulipwa IPTL. Kamati ilipohoji kama ulipaji huo
umezingatia Azimio la Bunge lako Tukufu kwamba fedha hizo
zisitolewe mpaka mgogoro baina ya TANESCO na IPTL
utakapotatuliwa, haikupatiwa majibu. Hivyo, Kamati kwa
kuzingatia umuhimu wa Azimio hilo la Bunge kutekelezwa ipasavyo
na kuhakikisha utoaji wa fedha katika Akaunti hiyo umefanyika
kihalali na aliyelipwa amelipwa kihalali, ilimuomba Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kufanya Ukaguzi Maalum
kuhusu miamala iliyofanyika katika Akaunti hiyo pamoja na umiliki
wa Kampuni ya IPTL.
1.1.3 Agizo la Kufanyika kwa Ukaguzi Maalum
Mheshimiwa Spika, tarehe 20 Machi, 2014 Kamati ya PAC
iliwasilisha Hadidu za Rejea kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
4
Hesabu za Serikali kwa ajili ya kufanya Ukaguzi Maalum kupitia
barua yenye Kumbukumbu Namba CBC.155/188/01/31. Aidha,
Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi iliwasiliana na Katibu wa Bunge kupitia
barua Kumbukumbu namba CA.27/442/01/53 ya tarehe 27 Aprili,
2014 ikiomba Kamati ya PAC iweze kuridhia Hadidu za Rejea
zitakazoongoza ukaguzi husika. Kamati iliridhia Hadidu za Rejea
husika kwa barua Na. CBC. 155/188/01 ya tarehe 3 Mei, 2014.
1.1.4 Majadiliano Bungeni
Mheshimiwa Spika, katika mijadala mbalimbali ambayo imekuwa
ikiendelea katika Bunge lako Tukufu, Waheshimiwa Wabunge
mbalimbali wamekuwa wakizungumzia kwa namna tofauti suala la
Akaunti ya Tegeta ESCROW. Michango hiyo imekuwa ikijikita
katika mambo makubwa mawili, kundi moja limekuwa likidai kuwa
fedha hizo ni za umma na zimetolewa bila kufuata taratibu za
kisheria. Kundi lingine limekuwa likisema fedha hizo siyo za umma
ni za IPTL na zilitolewa kihalali. Baadhi ya Wabunge ambao
wamewahi kuzungumzia suala hili ni pamoja na Mhe. David
Kafulila, (Mb.) Mhe. John Mnyika, (Mb.), Mhe. Profesa Sospeter
Muhongo, (Mb.) Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Stephen
5
Masele, (Mb.) Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Jaji.
Fredrick Mwita Werema, (Ex Official) Mwanasheria Mkuu wa
Serikali Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda, (Mb.)
Nukuu ya baadhi ya yaliyosemwa na Wabunge hawa zimeainishwa
katika uchambuzi wa Kamati ambao ni Sehemu ya Tatu ya Taarifa
hii.
1.2 Kuwasilishwa kwa Taarifa ya Ukaguzi Maalum
Mheshimiwa Spika, tarehe 14 Novemba, 2014, Taarifa ya
Ukaguzi Maalum wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali kuhusiana na Miamala iliyofanyika katika Akaunti ya
Tegeta ESCROW pamoja na Umiliki wa Kampuni ya IPTL
iliwasilishwa kwenye Ofisi ya Spika na Katibu wa Bunge na tarehe
17 Novemba, 2014 ilikabidhiwa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Hesabu za Serikali (PAC) ili ichambuliwe na kutolewa maoni na
mapendekezo. Tarehe 18 Novemba, 2014, Kamati ya PAC ilianza
uchambuzi wa Taarifa hiyo (Kiambatisho Na.1).
1.3 Kamati ya PAC ilivyofanya kazi
6
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 119 ya Kanuni za
Bunge, Toleo la 2013 Spika anaweza kukabidhi jambo lingine
lolote kwa Kamati yoyote kadri atakavyoona inafaa kwa ajili ya
kufanyiwa kazi na Kamati hiyo. Hivyo, Kamati ya PAC katika
kutekeleza jukumu la kuchambua Taarifa ya Ukaguzi Maalum
ilifanya kazi kama “Kamati ya Uchunguzi” ikiongozwa na masharti
ya Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge, Sura ya 296.1
Mheshimiwa Spika, Kanuni ya 117 imetoa pia mamlaka kwa
Kamati za Kudumu kujiwekea utaratibu wake na kuweza
kuwaruhusu Wabunge ambao sio Wajumbe wa Kamati husika
kuhudhuria na kushiriki katika shughuli za Kamati. Kwa kutumia
Kanuni hiyo, Kamati iliwaalika Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla (Mb),
Mhe. Luhaga Joelson Mpina (Mb) na Mhe. Alphaxard Kangi Lugola
(Mb) kuhudhuria na kushiriki vikao vya Kamati.
Mheshimiwa Spika, pamoja na kupitia Taarifa ya Ukaguzi
Maalum tarehe 19 Novemba, 2014 Kamati ilifanya mahojiano na
mashahidi wawili hususan Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali, Ndugu Francis Mwakapalila na Kamishna Mkuu
1The
Parliamentary
Imunities,
Powers
and
Privileges
Act,
Cap
296
7
wa TRA Ndugu Rished Bade. Pia Kamati ilimwandikia Mkurugenzi
Mkuu wa TAKUKURU Dkt. Edward Hosea kama rafiki wa Kamati.
Aidha, Kamati ilipitia Nyaraka na Sheria mbalimbali zilizoletwa na
mashahidi pamoja na Kumbukumbu Rasmi (Hansard) za Vikao vya
Bunge na Kamati za Kudumu za Bunge ambapo suala la Akaunti ya
Tegeta ESCROW limewahi kujadiliwa.
Mheshimiwa Spika, Wajumbe wa PAC na Wabunge waalikwa
walioshiriki kazi hii ni hawa wafuatao:-
1. Mhe. Zitto Zuberi Kabwe (Mb), - Mwenyekiti
2. Mhe. Deo Haule Filikunjombe (Mb), - Makamu
Mwenyekiti
3. Mhe. Asha Mshimba Jecha (Mb), - Mjumbe
4. Mhe. Desderius John Mipata (Mb), - Mjumbe
5. Mhe. Zaynab Matitu Vulu (Mb), - Mjumbe
6. Mhe. Zainab Rashid Kawawa (Mb), - Mjumbe
7. Mhe. Kheri Ali Khamis (Mb), - Mjumbe
8. Mhe. Abdul Jabir Marombwa (Mb), - Mjumbe
9. Mhe. Gaudence Cassian Kayombo(Mb), - Mjumbe
8
10. Mhe. Hezekiah Ndahani Chibulunje (Mb), - Mjumbe
11. Mhe. Amina M. Mwidau(Mb), - Mjumbe
12. Mhe. Lolesia M. Bukwimba (Mb), - Mjumbe
13. Mhe. Lucy Fidelis Owenya (Mb), - Mjumbe
14. Mhe. Esther Nicholas Matiko (Mb), - Mjumbe
15. Mhe. Ally Keissy Mohamed (Mb), - Mjumbe
16. Mhe. Faida Mohammed Bakar (Mb), - Mjumbe
17. Mhe. Ismail Aden Rage (Mb), - Mjumbe
18. Mhe. Modestus Dickon Kilufi (Mb), - Mjumbe
19. Mhe. Kombo Khamis Kombo, (Mb) - Mjumbe
20. Mhe. Catherine Valentine Magige (Mb), - Mjumbe
21. Mhe. Dkt. Haji Mponda (Mb), - Mjumbe
22. Mhe. Luhaga Joelson Mpina (Mb), - Mjumbe
Mwalikwa
23. Mhe. Alphaxard Kangi Lugola (Mb), - Mjumbe
Mwalikwa
24. Mhe. Dkt. Hamisi A. Kigwangalla (Mb), - Mjumbe
Mwalikwa
Kamati ilisaidiwa na Sekretarieti iliyoongozwa na Katibu wa Bunge
Dkt. Thomas D. Kashililah na Makatibu wengine ambao ni Ndg.
9
Nenelwa Mwihambi Wankanga, Ndg. Mathew Nionzima Kileo, Ndg.
Mswige Dickson Bisile na Ndg. Erick Sosteness Maseke.
10
2.0 UCHAMBUZI WA KAMATI KUHUSU TAARIFA YA UKAGUZI
MAALUM NA YALIYOJITOKEZA KWENYE MAHOJIANO YA
KAMATI NA KAIMU MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA
HESABU ZA SERIKALI, KAMISHNA MKUU WA TRA NA
MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU
2.1 UTEKELEZAJI WA MKATABA WA TANESCO NA IPTL
Mheshimiwa Spika, katika kuchambua hadidu za rejea
zilizofanyiwa kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali, Kamati ilijielekeza kwanza kufanya uchambuzi kuhusiana
na utekelezaji wa Mkataba wa kuzalisha umeme kati ya Kampuni
ya IPTL na TANESCO, uchambuzi wa Kamati katika Taarifa ya
Ukaguzi Maalum umebaini mambo mbalimbali. IPTL ilianzishwa
chini ya Wanahisa wawili ambao ni Kampuni ya Mechmar Malaysia
Berhad iliyosajiliwa nchini Malaysia ambayo ilikuwa inamiliki hisa 7
sawa na asilimia 70 katika IPTL na Kampuni ya VIP Engineering
and Marketing iliyosajiliwa hapa nchini ikiwa na hisa 3 sawa na
asilimia 30 ya hisa zote. Mwaka 1995 Serikali kupitia TANESCO
iliingia Mkataba wa miaka 20 na IPTL kwa ajili ya kuzalisha na
11
kuuziana umeme wa megawati 100 japokuwa makubaliano ya
awali (MOU) yalionyesha kuwa mkataba ungekuwa wa miaka 15.
Mahitaji ya umeme ilikuwa ni kwa dharura kutokana na ukame
uliosababisha upungufu wa maji katika mabwawa ya kuzalisha
umeme.
Mheshimiwa Spika, mwaka 1997 ujenzi wa mtambo wa
kuzalisha umeme ulikamilika. Hata hivyo, TANESCO ilibaini
kwamba gharama za ujenzi wa mtambo wa kuzalisha umeme
ambazo IPTL iliwasilisha kwake zilikuwa kubwa tofauti na
makubaliano ya kwenye Mkataba. IPTL ilikuwa imefunga injini
zenye msukumo wa kati (medium speed) zenye gharama ndogo
na uwezo mdogo badala ya injini za msukumo mdogo (low speed)
zenye nguvu kubwa na bei kubwa. Wakati huo huo IPTL
waliendelea kutoza kiasi kikubwa cha fedha kinacholingana na
gharama ya ufungaji wa mtambo wenye msukumo mdogo (low
speed). Katika utekelezaji wa Mkataba IPTL walitakiwa kufunga
jenereta 5 zenye uwezo wa kuzalisha megawati 20 kila moja lakini
badala yake walifunga jenereta 10 zenye uwezo wa kuzalisha
megawati 10 kila moja jambo ambalo lilikuwa ni kinyume na
makubaliano ya Mkataba.
12
Mheshimiwa Spika, kutokana na IPTL kukiuka makubaliano ya
Mkataba kama ilivyoelezwa hapo juu, mwaka 1998 TANESCO
ilifungua Shauri Na. ARB/98/8 katika Baraza la Kimataifa la
Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (The International Centre for
Settlement of Investiment Disputes - ICSID) kupinga ukiukwaji
huo. Katika Hukumu iliyotolewa na ICSID, IPTL iliagizwa
kupunguza gharama za uwekezaji kutoka USD 163.531 milioni hadi
USD 127. 201 milioni kwa mwezi.2 (Kiambatisho Na. 2)
Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Mtambo ulikamilika mwaka 1997
lakini uzalishaji na uuzaji wa umeme ulianza mwaka 2002. Kwa
mujibu wa makubaliano ya kuzalisha umeme, TANESCO ina wajibu
wa kulipia gharama za uwekezaji (capacity charges) kwa wastani
wa USD 2.6 milioni kila mwezi;3 gharama za kutumia umeme
(energy charges) wakati uzalishaji halisi unapofanyika na
kugharamia mafuta ya kuendeshea mitambo husika. Hivyo,
kuanzia mwaka 2002 capacity charges ambayo ni gharama za
uwekezaji kutokana na uwepo wa mtambo wa kuzalisha umeme,
2Shauri hili hurejewa kama ICSID-1
3
Baada
ya
utekelezaji
wa
ICSID
1
13
zilianza kulipwa na TANESCO kwa IPTL. Ikumbukwe kuwa capacity
charges huendelea kulipwa kwa muda wote ambao Mkataba
unaendelea bila ya kujali kama mtambo unazalisha umeme au
hauzalishi.
Mheshimiwa Spika, gharama hizi zilikoma kulipwa moja kwa
moja kwa IPTL mwaka 2007 baada ya TANESCO kubaini kuwa
IPTL inakokotoa gharama hizo kwa msingi wa USD 38.16 milioni
(ambayo ni sehemu ya mkopo wa USD 105 milioni uliochukuliwa
na wanahisa kutoka Umoja wa Mabenki ya Malaysia (Consortium
of Malaysian Banks) ambao baadaye ulinunuliwa na Standard
Chartered Bank ya Hong Kong) badala ya mtaji wa uwekezaji wa
kiasi cha Sh. 50,000 uliosajiliwa BRELA na hivyo kufanya tozo ya
capacity charges kuwa kubwa. Endapo ungetumika mtaji wa
uwekezaji wa Sh. 50,000/= katika kukokotoa capacity charges
TANESCO ingekuwa inalipa tozo ndogo kuliko ilivyo sasa.
Mheshimiwa Spika, kutokana na kutoridhishwa na kiwango cha
capacity charges kilichokuwa kinatozwa na IPTL mnamo mwaka
2004, TANESCO ilifungua Shauri la Pili ICSID kupinga kiasi kikubwa
14
cha tozo ya capacity charges.4 Uamuzi wa Baraza ilikuwa ni
kwamba Wanahisa waketi na Mteja wao (TANESCO) na
kukubaliana kuhusu kanuni ya ukokotoaji wa tozo hiyo.
Mheshimiwa Spika, mpaka tunapowasilisha Taarifa hii Bungeni,
Uamuzi wa ICSID-2 kwamba IPTL ikae na TANESCO kwa ajili ya
kukokotoa upya capacity charges haujatekelezwa, hivyo TANESCO
wanaendelea kulipa USD. 2.6 milioni (sawasawa na shilingi
4,511,000,000/= kwa mwezi)5 kila mwezi kama capacity charges
kwa IPTL izalishe au isizalishe umeme. Hivyo, utekelezaji wa
Mkataba wa uzalishaji wa umeme kati ya IPTL na TANESCO
umetawaliwa na migogoro toka ulipoanza mpaka sasa.
2.2 UFUNGUAJI WA AKAUNTI YA TEGETA ESCROW
Mheshimiwa Spika, Hadidu Rejea namba tatu ilimtaka Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuchunguza sababu za
Kufungua Akaunti Maalumu ya ESCROW – Tegeta (Tegeta-
ESCROW Account), Pia kuchunguza Chanzo cha mgogoro kuhusu
4 Shauri hili hurejewa pia kama ICSID 2.
5
Kiwango
cha
kubadilishia
fedha
Dola
1
kwa
wastani
wa
shilingi
1,735
(chanzo
BOT
tarehe
25/11/2014)
15
Tozo baina ya TANESCO na IPTL na kuthibitisha iwapo Mgogoro
uliamuliwa kwa Masilahi ya pande zote mbili yaani (TANESCO na
IPTL).
2.2.1 Chanzo cha kufunguliwa kwa Akaunti ya Tegeta ESCROW
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Ukaguzi maalum wa Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, sababu ya msingi ya
kufungua Akaunti ya Tegeta ESCROW ni kipengele Na. 6.8 cha
Mkataba wa kununua umeme, (Power Purchasing Agreement -
PPA) baina ya TANESCO na IPTL ambacho kinaeleza kuwa iwapo
upande wowote kati ya TANESCO au IPTL utapinga usahihi wa
tozo za Ununuzi wa umeme, Washirika hao watalazimika kutumia
jitihada zao kuhakikisha kuwa mgogoro juu ya Malipo husika
unamalizika kwa mujibu wa kipengele Na. 18.1 cha PPA.
Mheshimiwa Spika, kipengele husika (18.1 (a)) cha Mkataba wa
kununua umeme kinaitaka TANESCO na IPTL kujadiliana iwapo
hawaafikiani katika masuala ya Tozo na kinasomeka kama
ifuatavyo:
16
“In the event that a dispute arises, the Parties
shall attempt in good faith to settle such Dispute
by mutual discussion, which may include
referring the Dispute to the Operations
Committee, provided that any matters are
described in Article 7.4 shall be referred to the
Operations Committee for its review and
recommendations or attempted resolution,
where appropriate”
Mheshimiwa Spika, Aidha, kwa kuzingatia kipengele Na 18.2
(Kiambatisho Na. 3) wahusika katika mkataba wa PPA
wanalazimika kutumia mtaalamu wa upatanishi (mediation by
expert) katika utatuzi wa mgogoro kabla ya kutolewa fedha
zilizopo kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW.
Mheshimiwa Spika, kipengele cha 18.2 cha mkataba wa
ESCROW kinaelekeza wahusika kama ifuatavyo:
“In the event that Parties are unable to resolve a
Dispute in accordance with Article 18.1, then
17
either party, in accordance with this Article 18.2
may refer the Dispute to an expert for
consideration of the Dispute and obtain a
recommendation from the expert as the resolution
to the dispute”
Mheshimiwa Spika, uchambuzi wa Kamati kuhusu Taarifa ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali umethibitisha
kuwa kwa muda wote wa Mkataba baina ya TANESCO na IPTL
hapakuwahi kuanzishwa Kamati ya Uendeshaji (Operations
Committee). Kinyume na Kipengele 8.3 (a) cha PPA. TANESCO na
IPTL walipaswa kuunda Kamati ya Uendeshaji siku 180 kabla ya
kuanza uzalishaji (Commercial Operation Date). Kamati hiyo
ilitakiwa kuwa na Wajumbe sita ili kuratibu uendeshaji wa mtambo
na pia ingehusika na usuluhishi wa migogoro ambayo ingejitokeza
kutokana na Mkataba wa uzalishaji umeme.
Mheshimiwa Spika, umuhimu wa kufanyika usuluhishi kwenye
masuala ambayo TANESCO na IPTL wameshindwa kuelewana
umetiliwa nguvu na Kipengele 8.6 cha makubaliano ya Akaunti ya
18
Tegeta ESCROW. Kipengele hicho kinawaelekeza wahusika
kutumia taratibu za usuluhishi na makubaliano kama
zilivyoanzishwa na Azimio la Usuluhishi wa Mikataba baina ya
Mataifa na Mataifa (ICSID Convetion). Hivyo basi ni dhahiri kuwa
baada ya TANESCO na IPTL kutokukubaliana katika ngazi ya
Kamati ya Uendeshaji (ambayo haikuwahi kuanzishwa)
wangekwenda kwa Msuluhishi na kama ingeshindikana
wangechukua hatua ya upatanishi (arbitration).
2.2.2 Chanzo cha Mgogoro baina ya TANESCO na IPTL
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa uchambuzi wa Taarifa ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, imebainika kuwa
chanzo cha mgogoro kati ya TANESCO na IPTL ambacho ndio
kilisababisha kufunguliwa kwa Akaunti ya Tegeta ESCROW, ni
taarifa ziliyoifikia Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO mnamo tarehe
01 Aprili, 2004. Kaika Taarifa hiyo, pamoja na mambo mengine
walifahamishwa na mmoja wa wanahisa wa IPTL, Kampuni ya VIP
Engineering, kuwa kuna viashiria kuwa TANESCO wanailipa IPTL
capacity charges kubwa.
19
Mheshimiwa Spika, baada ya kupokea taarifa hiyo, Bodi ya
Wakurugenzi ya TANESCO iliiteua Kampuni ya Uwakili ya Mkono ili
kufuatilia madai hayo na kutoa ushauri kwa Bodi. Aidha, Bodi
iliwateua Ndg. Arnold Kileo, Dr. Enos Bukuku na Bw. Bashiri
Mrindoko ambao walikuwa Wajumbe wa Bodi kufuatilia kwa karibu
usahihi wa madai hayo.
Mheshimiwa Spika, Kampuni ya Uwakili ya Mkono iliishauri Bodi
ya wakurugenzi ya TANESCO kuwa, gharama za uwekezaji
zilizowasilishwa na IPTL na ambazo zilitumika kukokotoa kiwango
cha capacity charges hazikuwa sahihi. Ushauri huu ulitokana na
ukweli kuwa kiwango cha ‘capacity charges’ kilichokuwa kinatozwa
kilizingatia mtaji wa wanahisa (Owners’ Equity) ambao ni USD
milioni 38.16 badala ya Sh. za Kitanzania 50,000/= ambazo
wanahisa wa IPTL wakati wa usajili wa Kampuni hiyo kwa Msajili
wa Makampuni (BRELA) walikionyesha kuwa ndio mtaji (paid up
share capital). Aidha, kiasi hicho kimeonyeshwa katika Hesabu
zilizokaguliwa za IPTL kati ya mwaka 2002 na mwaka 2007.
(Kiambatisho Na. 4).
20
Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia ushauri wa Kampuni ya
Uwakili ya Mkono, Menejimenti ya TANESCO kupitia barua namba
DMDF&CS/02/05, tarehe 17 Juni, 2004 walitoa Notisi kwa IPTL ya
kutoendelea kulipa capacity charges kwa sababu kiwango
walichokuwa wanatozwa ni kikubwa kuliko inavyostahili
(Kiambatisho Na. 5).
Mheshimiwa Spika, pamoja na kutoa Notisi hii Kamati imebaini
kuwa Bodi na Menejimenti ya TANESCO kwa nyakati tofauti
walizitaarifu Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wizara ya
Nishati na Madini, na Msajili wa Hazina kuomba zichukue hatua
stahiki kutatua mgogoro uliokuwa unaendelea.6 Kamati ilifanikiwa
kuona barua Na. NEM/740/05 ya tarehe 6 Desemba, 2005 kutoka
kwa Kampuni ya Uwakili ya Mkono kwenda kwa aliyekuwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Patrick Rutabanzibwa
akirejea mazungumzo yao ya tarehe 5 Desemba, 2005 ambapo
iliamuliwa kuwa Kampuni ya Uwakili ya Mkono iandae Rasimu ya
Makubaliano kwa ajili ya ufunguzi wa Akaunti ya Tegeta ESCROW.
6Barua ya Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali yenye Kumb. Na.
SEC/247/07/04 ya tarehe 05 Julai 2004, Barua ya Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO kwenda kwa Katibu Mkuu
Wizara ya Nishati na Madini yenye Kumb. NaSEC.427/9/2004 ya tarehe 23 Septemba, 2004 na Barua ya
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO kwenda kwa Msajili wa Hazina yenye Kumb. Na. SEC.247/8/2004
21
2.2.3 Kufunguliwa kwa Akaunti ya Tegeta ESCROW
Mheshimiwa Spika, baada ya kukamilika kwa Rasimu ya
makubaliano ya mchakato wa kufungua Akaunti ya Tegeta
ESCROW, Mkataba wa kufunguliwa kwa Akaunti hiyo ulisainiwa na
washirika wawili ambao ni Wizara ya Nishati na Madini kama
mdhamini wa TANESCO katika ulipaji wa capacity charges na
energy charges na Kampuni ya IPTL. Aidha, kwa mujibu wa
Mkataba huo BOT ilikuwa ni wakala wa Uendeshaji wa Akaunti
husika.
Mheshimiwa Spika, wakati mahojiano ya Kamati na Kaimu
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Kamishna Mkuu
wa TRA pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU tarehe 19
Novemba, 2014 waliithibitishia Kamati kuwa kutokana na
makubaliano wa Akaunti ya Tegeta ESCROW, sehemu ya fedha au
fedha yote katika Akaunti hiyo ilikuwa ni fedha ya umma. Katika
mahojiano hayo, Maafisa hao walitamka yafuatayo kuhusiana na
umiliki wa fedha za Akaunti ya Tegeta ESCROW:
22
Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
“… Kwa jinsi tulivyopitia fedha hii, tungesema ipo katika
makundi matatu. Kundi la kwanza hiyo fedha ilikuwa na
kodi ndani yake kwa hiyo tungesema kulikuwemo na
fedha ya Serikali kwa maana ya kodi. Kwa upande
mwingine, kwa sababu mpaka ESCROW inafunguliwa
kulikuwa na dispute, kulikuwa na kutokubaliana juu ya
charges, kwa hiyo kuna fedha ambayo inaweza ikawa ni
ya TANESCO na kuna fedha ambayo inaweza kuwa ni ya
IPTL …”7
Kamishna Mkuu wa TRA
7Hansard ya mahojiano ya Kamati na Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali tarehe 19 Novemba
2014 uk. 19.
23
“… TANESCO walitudhihirishia na kwa evidence
kwamba katika kufanya yale malipo kwenye
ESCROW Account walilipa pamoja na pesa ambayo
ilitakiwa kulipwa kwetu ya VAT. Kwa hiyo,
kulikuwa na VAT Component ambayo haikutakiwa
kwenda kule …”8
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU
“… ninachoweza tu kusema na baada ya kusoma
Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali ni wazi kwamba pesa zilivyotoka TANESCO
kwenda Benki Kuu bado kwa maoni yetu ni fedha
za Serikali kwa sababu ni fedha ya TANESCO. Huo
ndiyo mtazamo ambao tunao kiuchunguzi hadi
wakati huu.”9
Mheshimiwa Spika, majibu haya yaliyotolewa na Kaimu
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Kamishna
Mkuu wa TRA na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU
8Hansard ya mahojiano ya Kamati na Kamishna Mkuu wa TRA tarehe 19 Novemba, 2014 uk. 61.
9Hansard ya mahojiano ya Kamati na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU tarehe 19 Septemba, 2014 uk. 81.
24
yanathibitisha kuwa Waziri wa Nishati na Madini na Naibu
wake pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali hawakuwa
sahihi walipolieleza Bunge kwamba fedha za kwenye Akaunti
ya Tegeta ESCROW siyo za Serikali. Wakijaribu kujibu hoja
mbalimbali za Wabunge kuhusiana na suala hilo kwa nyakati
tofauti kila mmoja wao kwa namna yake alitamka ifuatavyo:
Waziri wa Nishati na Madini. Mhe. Prof. Sospeter
Muhongo (Mb)
“…fedha za ESCROW hizi ni fedha zilizowekwa
baada ya hawa wafanyabiashara wawili
kutokukubaliana na zingeweza kuwekwa popote
… kwa hiyo hizo pesa ni za IPTL, yaani ni kitu
ambacho ni rahisi kabisa, lakini mtu anataka
kupotosha hapa anasema fedha za walipa kodi,
fedha sijui za wakulima, hakuna kitu kama
hicho,”10
10Hansard
ya
tarehe
30
Mei,
2014
ukurasa
wa
415
25
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Stephen
Masele (Mb)
“… nilipokuwa namsikiliza Mheshimiwa David Kafulila,
nikawa najiuliza maswali, Mheshimiwa David Kafulila
yumo humu Bungeni kwa amri ya Mahakama, kama
Mahakama inakupa amri ya kuwa Mbunge, halafu leo
ikiamua kwamba fedha za IPTL zilipwe, unahoji na
unataka umwingize Mheshimwa Muhongo wakati
Muhongo hajaamua chochote, kwa kweli
inasikitisha.”11
Mwanasheria Mkuu wa Serikali
“… kuhusu hili la ESCROW, lazima niseme ukweli.
Suala la ESCROW ni suala ambalo linatokana na
wanahisa wa IPTL ambao ni wanahisa wawili.
Mwanahisa mmoja ni VIP na mwingine ni
Mechmar, hiyo ndiyo IPTL. Ugomvi huu wa
ESCROW siyo pesa ya Serikali (Makofi) …”12
11Hansard
ya
tarehe
30
Mei,
2014
ukurasa
wa
397
12Hansard ya tarehe 25 Juni, 2014 uk. 72.
26
Mheshimiwa Spika, aidha Mheshimiwa Waziri Mkuu
alikuwa ni miongoni mwa waliodai kuwa fedha zilizokuwa
kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW siyo za umma. Akijibu
Mwongozo wa Mheshimiwa Kafulila kwenye Kikao cha Nane,
Mkutano wa 15 Mheshimiwa Waziri Mkuu alisema:
“…fedha zile ambazo zilikuwa zimewekwa
ESCROW Account ni fedha za IPTL kwa maana ya
hiyo Kampuni. Katika uamuzi wa Mahakama
uliotolewa ikaamua kuwa fedha ile ipelekwe IPTL
kwa sababu ni fedha ya IPTL. Tukasema ni
vyema, kukawa na mvutano pale kidogo sasa
tupeleke au tusipeleke, tukasema hapana, uamuzi
wa Mahakama unasema pelekeni, fedha zile
zikapelekwa kwa sababu ni za IPTL…”13
2.2.4 Kuibuka kwa madai ya IPTL Kutaka kulipwa fedha katika
Akaunti ya Tegeta ESCROW
13Hansard
ya
tarehe
9
Aprili,
2014
uk.
50-‐51
27
Mheshimiwa Spika, uchambuzi wa Kamati umebainisha kuwa
baada ya hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania katika Shauri
Na. 49 la 2002 na Na. 254 la 2003 ya tarehe 05 Septemba, 2013,
Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa PAP ambaye sasa
anajitambulisha kama Mmiliki wa IPTL, Bw. Harbinder Singh Sethi,
alimuandikia Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO barua yenye
Kumb. Na. IPTL/TANESCO/2013/03 ya tarehe 13 Septemba, 2013
akimtaka kulipa fedha zote zilizokuwa kwenye Akaunti ya Tegeta
ESCROW. (Kiambatisho Na.6). barua hiyo ilinakiliwa kwa Waziri
wa Nishati na Madini, na hapa ndipo upotoshaji wa amri ya
Mahakama ulipoanzia.
Mheshimiwa Spika, Amri ilikuwa inakabidhi ‘affairs’ za IPTL
lakini haikutoa maelekezo kuwa fedha zilizokuwa kwenye Akaunti
ya Tegeta ESCROW zitolewe bila kufuata utaratibu uliokuwa
umeainishwa katika makubaliano ya Akaunti husika. Hukumu ya
Mheshimiwa Jaji Oriyo ya tarehe 16 Desemba, 2008 iliyokabidhi
mali zote za IPTL kwa RITA haikutafsriwa kuwa fedha za Akaunti
ya Tegeta ESCROW zitoke bali ziliwekwa chini ya Mfilisi (RITA)
28
mpaka hapo mgogoro wa capacity charges uishe.14 Ni ajabu
kwamba Serikali nzima ilitafsiri Amri ya Mheshimiwa Jaji Utamwa
kwa matakwa ya Bw. Harbinder Singh Sethi.
Mheshimiwa Spika, Aidha tarehe 18 Septemba, 2013 Bw.
Harbinder Sethi alimwandikia tena Mkurugenzi Mtendaji wa
TANESCO akiendelea kusisitiza kuwa TANESCO wakubali kutoa
fedha zote za ESCROW na kutoendelea kupinga ankara za madai.15
Mheshimiwa Spika, kufuatia madai ya PAP kutaka kulipwa fedha
zilizokuwa kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW, tarehe 16
Septemba, 2013 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,
Bwana Eliakim Maswi, alimwandikia Mwanasheria Mkuu wa Serikali
barua Kumb. Na CBD.88/147/29 akimwarifu kuwa PAP imepewa
umiliki wa hisa za IPTL kwa uamuzi wa Mahakama wa tarehe 5
Septemba, 2013. Hata hivyo alimwarifu pia kuwa Akaunti ya
Tegeta ESCROW ilifunguliwa kutokana na mgogoro wa capacity
charges kati hiyo TANESCO na IPTL na hivyo umiliki wa fedha
zilizokuwemo kwenye Akaunti ya utabainika baada ya wahusika
14
Shauri
Na.
49
la
mwaka
2002,
Mahakama
Kuu
ya
Tanzania
(Dar
Es
Salaam)
15Barua ya Bw. Harbinder Sethi kwenda kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO yenye Kumb. Na.
IPTL/TANESCO/2003 ya tarehe 18 Septemba, 2013
29
kukutana na kujadiliana juu ya jambo hili. Kaatibu Mkuu aliomba
mwongozo wa kisheria kuhusu masuala hayo na akaambatanisha
mapendekezo ya makubaliano ya utolewaji wa fedha kwenye
Akaunti hiyo yaliyokuwa yameandaliwa na Kampuni ya PAP.
Mheshimiwa Spika, tarehe hiyo hiyo 16 Septemba, 2013
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, alimjibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini kwa barua Namba
AGCC/E.80/6/58 akikubaliana na maoni ya Katibu Mkuu wa Wizara
ya Nishati na Madini kuwa washirika wa Akaunti ya Tegeta
ESCROW (TANESCO na IPTL) wakae pamoja kuchambua madai
yanayoihusu TANESCO. Aidha Mwanasheria Mkuu wa Serikali
alielekeza kuwa dhamana ya Serikali kwenye Mkataba wa
uzalishaji umeme ipitiwe na kujadiliwa upya ili kukidhi mabadiliko
yaliyotokea na athari ambazo zingeweza kuipata Serikali.
2.3 MAUZO YA HISA ZA IPTL
Mheshimiwa Spika, Hadidu za rejea Namba 4, 5 na 10 Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuchunguza kama wakati
30
wa kufungua Akaunti ya BOT (Akaunti ya Tegeta ESCROW)
Mechmar ilikuwa inamiliki IPTL. Pia, kuthibitisha kwamba kampuni
ya Mechmar ilikuwa imehamishia umiliki wake kwa Kampuni ya
PAP kabla ya kufilisiwa, na kwamba sasa PAP inamiliki IPTL.
Katika Hadidu Rejea hizi masuala mawili makubwa yamejitokeza,
nayo ni mchakato wa PAP kumiliki IPTL na suala la malipo ya kodi
ya ongezeko la mtaji (capital gain) na ushuru wa stempu (stamp
duty). Kwa upande wa umiliki wa IPTL, Taarifa ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imeonyesha kuwa IPTL
ilikuwa inamilikiwa na Kampuni mbili, Mechmar (hisa 7) na VIP
(hisa 3) kwa mtaji wa Sh. 35,000 kutoka Mechmar na Sh. 15,000
kutoka VIP. Baadaye Mechmar iliuza hisa zake 7 kwa Kampuni
iliyosajiliwa British Virgin Islands (BVI) iitwayo Piper Link kwa USD
milioni 6.
Hata hivyo, uuzaji huu wa hisa kutoka Mechmar kwenda Piper Link
ulipingwa katika Mahakama Kuu ya British Virgin Islands kwa
Shauri lililofunguliwa na Martha Renju (ambaye anawakilisha
masilahi ya Benki ya Standard Chartered Hong Kong). Moja ya
maombi yaliyotolewa Mahakamani ni kuwa Mahakama ishikilie Hati
31
ya hisa husika mpaka shauri la msingi litakapomalizika.16 Siku hiyo
hiyo shauri lilipofunguliwa, tarehe 8 Novemba, 2010 Mahakama
ilitoa amri ya kusitisha uuzaji wa hisa hizo saba za Mechmar
kwenda Piper Link na kuamuru Piper Link iwasilishe Mahakamani
hapo Hati ya hisa 7 za IPTL zinazodaiwa kuuzwa kwake. Taarifa ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imebainisha pia
kuwa baada ya uamuzi wa mwisho kutolewa, tarehe 11 Aprili,
2014 Mahakama ilimkabidhi Martha Renju Hati ya hisa saba (7) za
Mechmar kwa 17barua ya Msajili wa Mahakama Kuu ya BVI
inayosomeka:
“This is to certify that the Share Certificate No. 01 with
07 shares as defined in the Statement of Claim being
held in Custody by The Court in the above matter be
returned to Maples and Calder on behalf of the
Claimant.”18
16 BVIH COM 2010/147
18 Barua ya tarehe 13 Aprili, 2011 kutoka kwa Msajili wa Mahakama Kuu ya BVI kwenda kwa Mawakili
wa Martha Rethu – Maples and Calder. Barua hii ni Kielelezo Namba 64 katika Taarifa ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
32
Katika mahojiano ya Kamati na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali, ilithibitishwa kuwa mpaka sasa Hati ya hisa
saba (7) za Mechmar kwenye IPTL bado ziko mikononi mwa Benki
ya Standard Chartered Hong Kong.19
Mheshimiwa Spika, umiliki wa hisa unakamilika pale ambapo
muuzaji anamkabidhi mnunuzi Hati ya hisa husika, vinginevyo
mnunuzi anakuwa amenunua “hisa hewa”. Pamoja na ukweli huu
bado Piper Links tarehe 21 Oktoba, 2011 ilimuuzia PAP hisa zile
saba kwa gharama ya USD 20 milioni. Swali linalojitokeza hapa ni
kuwa unawezaje kuuza kitu usichonacho? Ni wazi kuwa kwa kuwa
Piper Links hakuwa mmiliki halali wa hisa saba (7) za Mechmar
kwenye Kampuni ya IPTL alichonunua PAP ni “hisa hewa” na
kumiliki Kampuni hewa.
Mheshimiwa Spika, Mchakato huo umeifanya Kamati kuhoji
uhalali wa PAP kuchukua fedha za ESCROW kwa madai kuwa yeye
ndiye Mmiliki mpya wa IPTL. Kutokana na uchambuzi tuliofanya
hapo juu kinachojitokeza ni kuwa hata kama kulikuwa na uhalali
19 Mahojiano ya Kamati na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali tarehe 19 Novemba, 2014
33
kwa IPTL kulipwa sehemu ya fedha zilizokuwa kwenye Akaunti ya
Tegeta ESCROW bado PAP hakustahili kulipwa fedha hizo.
Mheshimiwa Spika, Kutokana na mahojiano kati ya Kamati na
Kamishina Mkuu wa TRA ilibainika kwamba Kampuni ya Piper Links
haijulikani sio tu British Virgin Islands bali hata nchi nyingine.20
Kamati haielewi ni jinsi gani taasisi kubwa kama Benki Kuu ya
Tanzania, Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Fedha, Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali na nyingine zilizohusika katika suala
hili, na ambazo tunaamini zimesheheni Watendaji wenye weledi,
zimewezaje kushindwa kufanya uchunguzi wa kina (due diligence)
ambao ungewezesha utata huu kugundulika na kuepuka
kudanganywa na PAP.
Mheshimiwa Spika, Kamati imejiridhisha kuwa kitendo cha
Kampuni ya Piper Links kukiuka amri ya Mahakama ya British Virgin
Islands ndiyo kilipelekea Bw. Harbinder Singh Sethi kufanya
udanganyifu uliotokea. Kwa maana hiyo Piper Links ni chanzo
kikubwa cha yaliyotokea. Ikumbukwe kuwa Piper Links na
Mechmar walilipa kodi ya ongezeko la mtaji (capital gain tax) siku
20
Ndg.
Rished
Bade,
tarehe
19
Novemba,
2014
34
moja (tarehe 6 Desemba, 2013) na kwenye tawi moja la Benki ya
CRDB na wote waliwakilishwa na mtu mmoja aliyewasilisha nyaraka
za kughushi na kukwepa kodi ya ongezeko la mtaji iliyopaswa
kulipwa.
2.3.1 Kodi iliyopaswa kukusanywa iwapo mauzo ya hisa 7 za
Mechmar kwenda Piper Links na baadaye kwenda PAP
yangekuwa halali
Mheshimiwa Spika, uchambuzi wa kamati umeainisha dosari za
kisheria za uhamishaji wa hisa za Mechmar kwenda Piper Links na
baadaye Piper Links kwenda PAP. Dosari ambazo zinafanya
mchakato huo mzima kukosa uhalali wa kisheria. Hata hivyo
endapo mchakato huu ungekuwa halali ulipaswa kuzingatia sheria
za kodi hususan Sheria ya Kodi ya Mapato kama ilivyorekebishwa
na Sheria ya Fedha ya mwaka 2012.
Mheshimiwa Spika, kama ilivyoelezwa hapo awali, katika
uchambuzi wa Hadidu za Rejea 4, 5 na 10 masuala ya kodi nayo
yaliyojitokeza, hususan kodi ya ongezeko la mtaji na ushuru wa
stempu. Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
alifafanua kuwa kodi ya ongezako la mtaji ni kodi ambayo hutozwa
35
kwenye faida inayotokana na mauzo ya mali na uwekezaji na katika
faida itokanayo na mauzo ya hisa.
Mheshimiwa Spika, Kamati ilishangazwa na kusikitishwa na kiasi
kikubwa cha kodi kilichopotea au kuibiwa kwa makusudi katika
mchakato mzima wa ukusanyaji wa kodi husika. Kama ilivyoelezwa
hapo awali kuwa, tarehe 9 Septemba, 2012 Kampuni ya Mechmar
iliuza hisa saba (7) kwa Piper Links ilizokuwa inamiliki katika
Kampuni ya IPTL kwa bei ya USD milioni 6.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo, taarifa zilizowasilishwa Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) kwa ajili ya kukokotoa kiasi cha kodi ya
ongezeko la mtaji ambacho Mechmar ilitakiwa kulipa, zinaonyesha
kuwa hisa hizo zimeuzwa kwa Sh. milioni 6. Kwa kutumia taarifa
hizo, TRA ilikokotoa kodi husika na hivyo Mechmar ilipaswa kulipa
kodi ya ongezeko la mtaji Sh. 1,919,988,800 na siyo Tsh.596,500
ilizolipa. Aidha, kwa upande wa ushuru wa stempu Mechmar
ilipaswa kulipa shilingi 96 milioni na siyo shilingi elfu 60 ilizolipa.
Hivyo jumla ya kodi iliyopotea kwa maana ya kodi ya Ongezeko la
Mtaji na ushuru wa stempu ni shilingi 2,015,988,800.
36
Mheshimiwa Spika, hisa kutoka Piper Links kwenda PAP ziliuzwa
kwa gharama ya USD milioni 20, lakini taarifa zilizopelekwa TRA
zilionyesha kuwa hisa hizo zimeuzwa kwa USD 300,000. Kwa
mantiki hiyo Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali inaonyesha kuwa Piper Links ilitozwa na kulipa kodi ya
ongezeko la mtaji kiasi cha Sh. 47,940,000 na Sh. 4,800,000 kama
ushuru wa stempu (stamp duty)’. Katika mahojiano, Kamishna
Mkuu wa TRA aliifahamisha Kamati kuwa kwa gharama ya USD
milioni 20 kiasi cha kodi ya ongezeko la mtaji kilichotakiwa kulipwa
ni Sh. 6,399,977,600 na sio Sh. 47,988,800, na kwa upande wa
ushuru wa stempu ‘stamp duty’ kiasi kilichotakiwa kulipwa ni Sh.
320,000,000 na siyo Sh. 4,800,000. Kwa maana hiyo jumla ya kodi
iliyopotea kwa maana ya kodi ya ongezeko la mtaji na ushuru wa
stempu (stamp duty)’ ni Sh. 6,667,188,800.
Mheshimiwa Spika, jumla ya kodi iliyopotea kutokana na uuzaji
wa hisa za Mechmar kwenda Piper Links na za Piper Links kwenda
PAP ni jumla ya shilingi 8,683,177,600.
Mheshimiwa Spika, mahojiano ya Kamati na Kamishna Mkuu wa
TRA yalilenga, pamoja na mambo mengine, kufahamu jitihada
37
zilizofanywa na watendaji wa TRA kuthibitisha uhalali wa taarifa
zilizowasilishwa kwao (due diligence) kabla ya kukokotoa kiasi cha
kodi ya ongezeko la mtaji kwa miamala yote miwili yaani Mechmar
– Piper Links na Piper Links – PAP. Kamati ilipotaka kufahamu ni
hatua gani zimechukuliwa kwa watumishi waliohusika na zoezi hilo,
hatua zinazochukuliwa na TRA ili kukusanya kodi iliyopotea na
kufuta Tax Clearance Certificate, ilijulishwa kuwa kwanza TRA
ilishtushwa na taarifa kuwa kulikuwa na mikataba miwili yenye bei
tofauti ambayo iliandaliwa na wahusika ili iwawezeshe kukwepa
kodi, na kwamba Kampuni ya VIP imeuza hisa zake 3 ilizokuwa
ikizimiliki kwenye kampuni ya IPTL kwa bei ya USD milioni 75
wakati PAP hiyo hiyo iliuziwa na Piper Links hisa 7 kwa USD
300,000. Hivyo, TRA ilifanya uchunguzi wake ikiwa ni pamoja na
kuhoji watu mbalimbali akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa PAP Bw.
Harbinder Singh Sethi (Kiambatisho Na. 7).
Mheshimiwa Spika, Kamati ilipokea taarifa ya uchunguzi wa
ndani iliyofanywa na TRA ambao ulithibitisha ukwepaji mkubwa wa
kodi na udanganyifu wa mikataba. Kamati imekubaliana na uamuzi
wa TRA kuondoa hati za kodi kwa IPTL na hivyo kuna uwezekano
kuwa kuanzia tarehe 24 Novemba, 2014 PAP haitokuwa tena
38
mmiliki wa IPTL mpaka hapo watakapofuata upya tararibu za
kisheria na TRA kukusanya kodi stahiki.
2.4 KIASI CHA FEDHA KILICHOKUWEMO NA KILICHOLIPWA
KUTOKA AKAUNTI YA TEGETA ESCROW
Mheshimiwa Spika, Hadidu rejea ya 7 ilimtaka Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuchunguza kiwango cha
fedha kilichokuwepo kwenye Akaunti Maalumu ya ESCROW, wakati
BOT inahamisha fedha zilizokuwepo katika akaunti hiyo kwenda
IPTL, kiwango cha cha fedha kilichopaswa kuwemo katika akaunti
hiyo maalumu ya BOT pamoja na kiwango cha fedha
kinachopaswa kulipwa zaidi kutoka TANESCO. Hii ilihusisha pia
kuchunguza na kutoa taarifa kuhusu Kiasi cha fedha kilichowekwa
na kila mhusika hadi uamuzi wa mahakama Kuu ya Tanzania
ulipotolewa.
Mheshimiwa Spika, hadi kukamilika kwa Ukaguzi wa Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Kamati imebaini kuwa kiasi
kilichokuwepo kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW ni Sh.
39
167,251.892.330 na USD 22,198,544. Baada ya Uhakiki wa
Akaunti ya Tegeta ESCROW hadi tarehe 05 Novemba, 2013 ilikuwa
na Kiasi cha Sh. 8,020,522,330 na USD 22,198,544. Aidha,
kulikuwa na Kiasi cha Sh. 159,231,370,000 kilichojumuisha fedha
zilizowekezwa kwenye hati fungani (Treasury Bills) Sh.
148,071,081,052 zenye riba ya Sh. 11,160,288,948.21
Mheshimiwa Spika, malipo yote ya Sh. 167,251,892,330 na USD
22,198,544 zililipwa kwa Kampuni ya PAP kupitia Akaunti Na.
912000012534 ya USD na Akaunti Na. 9120000125294 ya Shilingi
za kitanzania katika Benki ya Stanbic zilizofunguliwa tarehe 27
Novemba, 2013 maalum kwa ajili ya kupokea fedha hizo. Hivyo
jumla ya fedha iliyotolewa kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW na
kulipwa kwa PAP ni shilingi 203,102,540,890.22
Mheshimiwa Spika, uchunguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali umebainisha kuwa hadi kufikia tarehe 05 Juni,
2007 kiasi kilichokuwa kwenye akaunti ni jumla ya Sh. 118,
291,827,820 japokuwa TANESCO walipinga gharama za tozo, lakini
21
Taarifa
ya
CAG
kuhusu
Akaunti
ya
Tegeta
ESCROW
ukurasa
wa
35
22
Kiwango
cha
kubadilishia
fedha
Dola
1
kwa
wastani
wa
shilingi
1,615
(chanzo
BOT
tarehe
28/11/2013)
40
waliendelea kulipa gharama hizo kati ya mwaka 2004 na 2007.
Aidha, uhakiki wa Ankara za IPTL za hadi tarehe 01 Juni, 2014
zilizopatikana TANESCO zilibainisha kuwa Akaunti ya Tegeta
ESCROW ilitakiwa kuwa na Sh. 306,675,081,939.
Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la fedha zilizowekwa katika
Akaunti ya Tegeta ESCROW, uhakiki wa wakaguzi ulibainisha kuwa
kulikuwa na jumla ya Sh. 182,771,388,687, kati ya hizo TANESCO
iliweka Kiasi cha Sh. 142,008,357,587 na Wizara iliweka Kiasi cha
Sh. 40,763,031,100.
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa ankara zilizotolewa na IPTL
inaonekana TANESCO ilipaswa kuweka Kiasi cha Sh.
123,903,693,252 zaidi ya fedha ilizoziweka katika Akaunti ya
Tegeta ESCROW ikiwa ni tofauti kati ya Kiasi ilichotakiwa kuweka
cha Sh. 306,675,081,939 na Kiasi kilichowekwa cha Sh.
182,771,388,687.
Mheshimiwa Spika, pamoja na riba ya Sh. 11,160,288,948
iliyopatikana katika uendeshaji wa Akaunti ya Tegeta ESCROW,
fedha hizo zote zililipwa kwa Kampuni ya PAP, huku wakala wa
41
uendeshaji wa Akaunti husika (BOT) hakupewa kiasi chochote
japokuwa walitumia gharama kubwa katika kesi zilizofunguliwa
dhidi ya Akaunti hiyo na gharama za kawaida za uendeshaji.
2.5 USHIRIKI WA TAASISI ZA SERIKALI NA WATU BINAFSI
KATIKA UTOAJI FEDHA KATIKA AKAUNTI YA TEGETA
ESCROW
2.5.1 Benki Kuu ya Tanzania (BOT)
Mheshimiwa Spika, Hadidu ya Rejea ya Pili ilihusu wajibu wa
Benki Kuu ya Tanzania kama ulitekelezwa ipasavyo katika
mchakato wa kutoa fedha kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW.
Miongoni mwa maswali muhimu kwa Kamati ilikuwa ni kwanza
kufahamu kwamba katika suala la Akaunti ya Tegeta ESCROW
Benki Kuu ilikuwa na Wajibu gani na iliutimizaje? Ama je, ilikuwa
sahihi namna Wajibu huo ulivyotimizwa?
Uchambuzi wa Kamati katika Taarifa ya Ukaguzi Maalum na
Makubaliano ya Uendeshaji wa Akaunti ya Tegeta ESCROW
42
yaliyokuwepo kati ya Serikali na IPTL umebainisha kwamba Benki
Kuu ya Tanzania ilikuwa na wajibu ufuatao:
a) Kufungua na kuhifadhi Akaunti ya Tegeta ESCROW katika
sarafu mbili, yaani Shilingi ya Tanzania na USD.
b) Kupokea, kuhifadhi na kuwekeza fedha za Akaunti ya Tegeta
ESCROW;
c) Kushughulikia kutolewa kwa fedha hizo kwa kuzingatia masharti
yaliyopo katika Sehemu ya Nne ya Makubaliano ya Akaunti ya
Tegeta ESCROW (Kiambatisho Na. 3) ambayo ni kujiridhisha
kwamba mgogoro kuhusu capacity charges kati ya IPTL na
TANESCO umetatuliwa, na kwamba Makubaliano yanayohusiana
na utatuzi wa mgogoro huo yanakuwepo katika Hati iliyosainiwa
na kuwasilishwa kwake kwa ajili ya mchakato wa utoaji wa
fedha hizo.
d) Kutoa taarifa za kila robo Mwaka kwa IPTL na TANESCO kuhusu
hali ya Akaunti.23
23Kipengele
Na.
2
cha
Makubaliano
ya
Uendeshaji
wa
Akaunti
ya
Tegeta
ESCROW
43
Mheshimiwa Spika, kabla ya kuchambua namna Benki Kuu
ilivyotimiza wajibu wake kama ulivyoelezewa hapo juu tujielekeze
kidogo kwenye ufahamu wa dhana nzima ya Akaunti ya Tegeta
ESCROW. Akaunti ya aina hii hutumika kuhifadhi kiasi cha fedha
pale washirika wa mkataba wa kibiashara wanapokuwa kwenye
mgogoro na hivyo kuhitaji kutunza fedha zinazotokana na
utekelezaji wa mkataba husika kwenye jambo linalobishaniwa ili
kusubiri uamuzi wa msuluhishi au maridhiano ya washirika.
Mheshimiwa Spika, baada ya kuyafahamu majukumu ya msingi
ya Benki Kuu ya Tanzania katika Akaunti ya Tegeta ESCROW,
Kamati ilijielekeza katika kufahamu namna Benki Kuu ya Tanzania
ilivyotimiza wajibu huo. Uchambuzi wa Kamati umebaini kwamba
ili kutekeleza wajibu ambao Benki Kuu ya Tanzania ilikuwa nao
katika Akaunti ya Tegeta ESCROW, iliishauri Serikali kujiridhisha
zaidi kabla ya kutoa fedha kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW juu
ya mambo yafuatayo:
(a) Kuwepo kwa ushahidi kwamba hisa zilizokuwa zinamilikiwa
na Mechmar zimenunuliwa na PAP na manunuzi husika
yamesajiliwa na BRELA;
44
(b) Kuwepo na ushahidi kuwa mgogoro uliokuwepo kati ya IPTL
na TANESCO kuhusu capacity charges umepatiwa suluhu, na
imeafikiwa kwamba IPTL ilipwe fedha husika;
(c) Wizara ya fedha ilete ushauri kuhusiana na uwepo wa Kodi ya
Ongezeko la thamani katika fedha zilizopo katika Akaunti ya
Tegeta ESCROW.
(d) Serikali kupatiwa kinga ya IPTL ili kujiepusha na uwezekano
wa kushitakiwa na IPTL hapo baadaye kutokana na Benki Kuu
kutoa fedha za IPTL.24
Mheshimiwa Spika, baada ya uchunguzi wa Kamati kuhusiana
na ushauri uliotolewa na BOT kwa Serikali yafuatayo yalibainika:
(i) Kuhusu kuwepo ushahidi kwamba hisa zilizokuwa
zinamilikiwa na MECHMAR zimenunuliwa na PAP na
manunuzi husika yamesajiliwa na BRELA,
24Ushauri wa Benki Kuu ulitolewa kwenye Kikao cha maridhiano kilichoitishwa kwa dharura na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini Bw. Eliakim Maswi kupitia barua yake yenye kumbu Na. CBD. 88/417/31 ya tarehe
23 Septemba, 2013 kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Servacius Likwelile.
45
kilichowasilishwa kwa Gavana wa Benki Kuu ni Deed of
Assignment of Shares na Mkataba wa kuuza hisa kati ya PAP na
Piper Link (Kiambatisho Na. 8) na siyo hati halisi ya umiliki
wa hisa.
(ii) Kuhusu ushahidi kuwa mgogoro uliokuwepo kati ya
IPTL na TANESCO kuhusiana na overcapacity charges
umepatiwa suluhu na imeafikiwa kwamba IPTL ilipwe
fedha husika, Kamati yangu, imethibitisha kwamba hakukuwa
na makubaliano kati ya TANESCO na IPTL ambao ndiyo
washirika wa Akaunti ya Tegeta ESCROW. Uthibitisho huu
unatokana na maelezo ya kipengele Na. 3.2 na 7.1 cha Taarifa
ya Kamati ya Wataalam iliyokutana tarehe 24 Septemba, 2013
kuhusu utoaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta ESCROW.
Taarifa hiyo ya Wataalam ndiyo iliyotumika kama kielelezo cha
ushahidi kuwa mgogoro uliokuwepo kati ya IPTL na TANESCO
kuhusiana na capacity charges umepatiwa suluhu jambo
ambalo ni kinyume na yaliyomo katika kipengele 3.2 na 7.1 cha
Taarifa husika (Kiambatisho Na. 9). Vipengele hivyo
vinasomeka kama ifuatavyo:-
46
“3.2 Discussions between TANESCO and IPTL on
disputed capacity charges are ongoing, therefore,
the team could not make concrete observation on
this issue.”
“7.1 TANESCO and IPTL should conclude the
ongoing verification of the outstanding capacity
charges invoices and issues relating to it and
submit a joint resolution to PS-MEM as soon as
possible to enable other process to take off.”
Mheshimiwa Spika, Kamati imethibitisha kuwa uthibitisho na
vielelezo alivyopata Gavana wa Benki Kuu katika kufikia
maamuzi ni Taarifa ya Kamati ya Wataalam kama ilivyotajwa
hapo juu. Hata hivyo Kamati imefanikiwa kuona nyaraka
iliyosainiwa na Ndugu John Kabadi kwa niaba ya TANESCO na
Mwakilishi wa Kampuni ya IPTL ya tarehe 8 Oktoba, 2013
kwamba wamekubaliana kuwa fedha zote za ESCROW zilipwe
kwa IPTL mara moja. Uamuzi huu uliwasilishwa na Mwenyekiti
wa Bodi ya TANESCO kwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na
47
Madini tarehe 9 Oktoba, 2013.25 Makubaliano haya hayaonekani
katika mawasiliano yoyote ya Kiserikali na badala yake Kamati
iliona Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini akiingia
makubaliano na IPTL ya utoaji wa fedha katika Akaunti ya
Tegeta ESCROW (Kiambatisho Na. 10).
(iii) Kuhusu Wizara ya fedha kupeleka ushauri kuhusiana na
uwepo wa Kodi ya Ongezeko la thamani katika fedha
zilizopo katika Akaunti ya Tegeta ESCROW, Kamati
haikupata ushahidi kwamba Wizara ya Fedha ilishauri kuhusu
masuala ya kodi ya ongezeko la thamani katika fedha
zilizokuwepo kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW pamoja na
kushauriwa na TRA kwa barua Na. 100-221-969/214 ya tarehe
29 Oktoba, 2013 iliyonakiliwa pia kwa Gavana wa Benki Kuu.
Katika barua hiyo TRA waliainisha uwepo wa kodi ya ongezeko
la thamani ya Sh. 26,946,487,420.80 kwenye Akaunti ya
Tegeta ESCROW (Kiambatisho Na. 11). Hata hivyo, barua
ya TRA Kumb. Na. TRA/CG/L.3 ya tarehe 4 Februari, 2014 kwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha ilionesha kuwa kiasi cha kodi
25barua yenye Kumb. Na. SEC.427/IPTL/10/2013
48
kinachodaiwa ni Sh. 21,713,935,720.75. (Kiambatisho Na.
12).
Mheshimiwa Spika, Kamati imebaini kuwa Mwanasheria Mkuu
wa Serikali kwa barua yenye Kumb Na. AGCC/E.080/6/70 ya
tarehe 18 Novemba, 2013 alimthibitishia Gavana kuwa hakukuwa
na kodi ya Serikali katika fedha zilizokuwa kwenye Akaunti ya
Tegeta ESCROW na kwamba fedha hizo zihamishiwe IPTL ili
Serikali ijinasue na mashauri yasiyo na tija kwake.
Mheshimiwa Spika, Kamati inaona ushauri wa Mwanasheria
Mkuu wa Serikali ulimpotosha Gavana kwa sababu kwa mujibu wa
kifungu 5(4) cha Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, 2006
capacity charges hukatwa kodi.
(iv) Kuhusu Serikali kupatiwa kinga kutoka IPTL dhidi ya
madai yanayoweza kujitokeza baada ya fedha katika
Akaunti ya Tegeta ESCROW kulipwa.
49
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na kinga hii, Harbinder Singh
Sethi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa PAP alitoa Kinga kwa
hati iliyotolewa tarehe 27 Oktoba, 2013. Hata hivyo, kwa
mujibu wa taarifa za TRA zilizowasilishwa kwa Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali uhalali wa PAP kumiliki
hisa 7 za Piper Links investiment ulitiliwa mashaka na TRA kwa
kuwa PAP haikuwa na Tax Clearance Certificate ambayo ndiyo
hutumika kwa Kampuni kusajiliwa BRELA na hatimaye
kutambuliwa na Wizara ya Nishati na Madini. Kwa maana hiyo
PAP haikutimiza masharti ya Kifungu cha 90(2) cha Sheria ya
Kodi ya Mapato ambacho kinasomeka kama ifuatavyo:
“The installment referred to in subsection 1 shall be
paid before the title to an investment asset is
transferred, and appropriate authorities for
registration, transfer or approval shall not register
such transfer or change of name without the
production of a certificate of the Commissioner
certifying that the installment has been paid or that
no installment is payable.”
50
Mheshimiwa Spika, Kifungu hiki ambacho kilifanyiwa
marekebisho kwa Sheria ya Fedha ya mwaka 2012 (Sheria Na
8 ya 2012) kimeweka utaratibu wa kuwezesha Serikali kutoza
kodi pale makampuni yanapouziana Hisa nje ya nchi. Sheria hii
inataka kwanza kupata hati ya TRA (Tax Clearance Certificate)
kabla ya BRELA kusajili hisa hizo na kabla ya mamlaka za
uthibitisho kuthibitisha. Wakati Wizara inaingia makubaliano ya
kutoa fedha za Akauti ya Tegeta ESCROW kwa PAP na wakati
PAP wanalipwa fedha hizo, Kampuni hiyo haikuwa na uhalali
wa kumiliki IPTL. Hivyo BRELA, Wizara ya Nishati na Madini,
TANESCO na BOT walikiuka Sheria ambazo kama zingefuatwa
pengine leo tusingekuwa tunajadili suala hili.
Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana
kutoka TRA, imebainika kuwa mpaka malipo ya kwanza katika
Akaunti ya Tegeta ESCROW yanafanyika tarehe 28 Novemba,
2013 PAP haikuwa na Tax Clearance Certificate ambayo
ingeiwezesha kumiliki hisa 7 za IPTL. Taarifa hizo zinaeleza
kwamba tarehe 23 Desemba,2013 kwa kutumia mikataba ya
kughushi PAP ilipata Tax Clearance Certificate No. 0049656
51
(Mechmar kwenda Piper Links) na 0049657 (Piper Links
kwenda PAP).
Hata hivyo pamoja na kutokuwa na Tax Clearance Certificate
bado Kampuni ya PAP ilitambuliwa na Wizara ya Nishati na
Madini pamoja na uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania wa
tarehe 5 Septemba, 2013 kupitia Hukumu ya Mheshimiwa Jaji
J.H.K. Utamwa iliyokabidhi shughuli zote za IPTL kwa PAP na
kuiwezesha kulipwa fedha zote zilizokuwa katika Akaunti ya
Tegeta ESCROW.
Mheshimiwa Spika, Kamati imethibitisha juhudi kubwa
aliyofanya Gavana wa Benki Kuu kutaka kujiridhisha vya kutosha
kabla ya kuruhusu fedha hizo kutolewa. Hata hivyo, alipata
maagizo kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwamba fedha
hizo zitoke (Kiambatisho Na.17).
2.5.2 Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO
Mheshimiwa Spika, katika suala la utoaji wa fedha katika
Akaunti ya Tegeta ESCROW, Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO
ilikutana katika Kikao cha
52
dharura mnamo tarehe 19 Septemba, 2013 ili Kujadili suala la
utolewaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta ESCROW. Katika
Kikao hicho, Menejimenti ya TANESCO iliwasilisha taarifa Na. 447
ambapo ilitahadharisha juu ya utolewaji wa fedha katika Akaunti
hiyo kabla ya kuhitimishwa kwa Shauri la madai ya msingi ya
TANESCO juu ya capacity charges (Kiambatisho Na. 13).
Mheshimiwa Spika, siku hiyo hiyo ya tarehe 16 Septemba, 2013
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO Jenerali
Mstaaafu Robert Mboma, alimwandikia Katibu Mkuu Wizara ya
Nishati na Madini akimwarifu kuwa TANESCO itafuata maelekezo
ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwamba washirika wa Akaunti
ya Tegeta ESCROW wakae pamoja kutatua mgogoro wa capacity
charges ili kubaini kiasi kinachostahili kulipwa IPTL na
kinachotakiwa kurejeshwa TANESCO.
Mheshimiwa Spika, Kamati imepata shaka kubwa juu ya uamuzi
wa haraka bila kufanya uchunguzi wa kina, kwa Bodi ya
Wakurugenzi ya TANESCO kufanya vikao viwili mfululizo ili
kuruhusu uchotwaji wa fedha za ESCROW. Kikao cha kwanza
kilifanyika mnamo tarehe 16 Septemba, 2013 ambapo Bodi ilikuwa
53
na msimamo sawa na wa Menejimenti kuwa fedha za ESCROW
zisitoke, Kikao cha pili cha dharura kikafanyika tarehe 19
Septemba, 2013 ambapo Bodi iliazimia pia kuwa fedha zisitoke.
Mheshimiwa Spika, kati ya tarehe 14 hadi 20 Septemba, 2013
TANESCO ilimuagiza Mwanasheria wake Bw. Godwin Ngwilimi
aende nchini Malaysia kufanya “due diligence” kuhusu uhalali wa
Kampuni ya PAP kumiliki IPTL. Wakati huo Bodi ya TANESCO
ilikuwa na vikao vya haraka haraka “supersonic speed” ambavyo
vilikubali haraka bila hata kusubiri ushauri wa Mtumishi wao
kwamba fedha za ESCROW wapewe PAP.
Mheshimiwa Spika, katika barua ya Mkuu huyo wa Sheria wa
TANESCO kwenda kwa Mkurugenzi Mtendaji yenye Kumbukumbu
Na. SEC.427/IPTL/11/2013 ya tarehe 7 Novemba, 2013 alisema:
“Nilishuhudia nyaraka kwamba Piper Link ilinunua
hisa za Mechmar na katika mauziano hayo Kampuni
hiyo iliwakilishwa na Bw. Harbinder Singh Sethi hivyo
huyu bwana ndiye Piper Link na ndiye PAP”
54
Hata hivyo, Bodi ya TANESCO haikukubaliana na ushauri huo na
hatimaye kumwachisha kazi Bwana Godwin Ngwilimi. Kosa lake
kubwa ni kutahadharisha kuwa nchi inatapeliwa. Kama ushauri
huu ungefuatwa tusingefika hapa tulipo leo kwa sababu hadi hapa
fedha katika Akaunti ya Tegeta ESCROW zilikuwa hazijatolewa.
Mheshimiwa Spika, Hata hivyo, mnamo tarehe 9 Oktoba 2013
Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO alimuandikia barua Katibu Mkuu
Wizara ya Nishati na Madini yenye Kumbukumbu Na.
SEC.427/IPTL/10/2013 akimuarifu mambo yafuatayo;
a) Bodi ilipokea kutoka IPTL madai ya kiasi cha ziada cha dola
za kimarekani 45,485,719.97 pamoja na riba na tozo ya
jumla ya dola za kimarekani 33,564,004.53 na hivyo kufanya
jumla ya madai za ziada ya kilichopaswa kulipwa kwenye
akaunti ya Tegeta ESCROW kuwa USD 79,049,724.50. Hivyo,
kuiagiza Menenjimenti ya TANESCO kufanya uhakiki wa kiasi
hicho.
b) Baada ya Menejimenti kuwa imehakiki madai hayo, Bodi
imejiridhisha kuwa IPTL sio tu inastahili kulipwa fedha
55
zilizokuwa kwenye akaunti ya Tegeta ESCROW bali pia
wanastahili kulipwa kiasi cha tozo na riba kilichotajwa hapo
juu.
Mheshimiwa Spika, huku ikieleweka kuwa Bodi ya TANESCO
haikuwa imefanya maridhiano na IPTL kuhusiana na mgogoro wa
‘over capacity charges’ unaohusu fedha zilizokuwa kwenye akaunti
ya Tegeta ESCROW, Bodi ilimuarifu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati
na Madini kuhusu makubaliano mapya yaliyofikiwa baina yake na
IPTL kuhusu kulipa ziada husika kwenye Akaunti ya Tegeta
ESCROW kwa njia mbadala zifuatazo:
a) Kulipa fedha za ziada dola za kimarekani 45,485,719.97 iwapo
TRA itakubali kusamehe kodi ya USD 33,564,004.53 ambayo ni
sawa na kiasi cha tozo na riba ambacho TANESCO anadaiwa na
IPTL. Au,
b) Kulipa USD 79,049,724.50 iwapo TRA haitosamehe kodi ya USD
33,564,004.53 ambayo ni sawa na kiasi cha tozo na riba
ambacho TANESCO anadaiwa na IPTL (Kiambatisho Na. 14
na 15).
56
Mheshimiwa Spika, Kamati imeshangazwa na makubaliano hayo
yaliyofikiwa kati ya Bodi ya TANESCO na IPTL, ikizingatiwa kuwa
mgogoro wa msingi uliohusu madai ya TANESCO kutozwa capacity
charges kubwa na IPTL haukupatiwa ufumbuzi kama ilivyoelekezwa
na ICSID. Kamati imefanikiwa kuona muhtasari wa kikao cha
Menejimenti ya TANESCO na IPTL kilichofanyika tarehe 8 Oktoba,
2013 katika Hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam ambapo
imebaini kuwa walizungumzia mambo yafuatayo:
a) Hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania chini ya Mhe. Jaji
Utamwa, J iliyotolewa tarehe 5 Septemba 2013
b) Uhamishaji wa mali za IPTL ikijumuishwa Mitambo ya kufua
Umeme na madai ya fedha za IPTL kwa TANESCO yaliyowekwa
kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW kwenda kwa PAP.
c) Madai ya ziada ya IPTL kwa TANESCO kama yalivyoainishwa
hapo juu.
57
Mheshimiwa Spika, hakukuwa na uthibitisho kuwa walizungumzia
suala la kutafuta maridhiano kuhusu madai ya TANESCO kutozwa
capacity charges kubwa ili kuwezesha kutolewa kwa fedha
zilizokuwemo kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW ingawa inaonyesha
kwenye mawasiliano mbalimbali yaliyofanyika kati ya Serikali,
TANESCO na IPTL walikuwa wanajua kuwa wanapaswa kufanya
maridhiano katika suala husika.
Mheshimiwa Spika, ni dhahiri kutokana na Bodi ya TANESCO
kukubali kulipa madai ya ziada wakati madai ya msingi ya IPTL na
TANESCO (Fedha iliyowekwa kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW)
hayajapatiwa ufumbuzi, inaonyesha udhaifu wa kiuongozi na
kutanguliza maslahi binafsi mbele kabla ya maslahi ya Umma. Kamati
inahofu iwapo makubaliano hayo yatakubaliwa na kutekelezwa,
Serikali itapoteza fedha nyingi bila manufaa kwa kuendelea kuilipa
IPTL madai hayo ya ziada.
2.5.3 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya VIP Engineering
Ndg. James Rugemalira
58
Mheshimiwa Spika, katika suala zima la IPTL, Ndg. James
Rugemalira anatajwa kama Mkurugenzi Mtendaji wa VIP
Engineering ambaye alikuwa na hisa 3 kati ya hisa 10 kwenye
IPTL. Kwa mujibu wa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali, mwaka 2004, Ndg. Rugemalira aliufahamisha
uongozi wa TANESCO kuwa gharama za ‘capacity charges’
wanazotozwa na IPTL ni za juu tofauti na makubaliano. Taarifa hizi
baadaye zilithibitishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO na
kusababisha Akaunti ya Tegeta ESCROW kufunguliwa kama
tulivyoeleza hapo awali.
Mheshimiwa Spika, Bw. James Rugemalira ameonekana
kuhusika tena na suala la IPTL pale alipofungua Shauri
mahakamani kuomba kuiondoa IPTL kwenye ufilisi na kisha kuuza
hisa zake kwa Kampuni ya PAP. Ni baada ya uamuzi wa Mahakama
Kuu kuhusu shauri hili uliotolewa tarehe 5 Septemba, 2013 ndipo
fedha za Akaunti ya Tegeta ESCROW zilipotolewa kwa uharaka.
Mheshimiwa Spika, Kamati imepitia Mkataba wa mauzo ya Hisa
kati ya Kampuni ya PAP na VIP na kuthibitisha kuwa Waziri wa
Nishati na Madini Mheshimiwa Prof. Sospeter Muhongo (Mb) ndiye
59
alikuwa kiungo kati ya Bw. Harbinder Singh Sethi wa IPTL na Ndg.
Rugemalira wa VIP (Kiambatisho Na. 16). Katika mkataba huo
wa tarehe 19 Agosti, 2013. Ndg. James Rugemalila alithibitisha
kuwa Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof. Sospeter Muhongo
alimwomba kuwasilisha kiasi cha fedha ambacho angependa
kulipwa na IPTL ili kumaliza Shauri lililokuwepo mahakamani.
Aidha, Bw. Sethi aliwasilisha kwa Bw. Rugemalira ushahidi
kwamba PAP imenunua Hisa 7 za Mechmar katika IPTL.
“On 11th July 2013, the Minister of Energy and
Minerals, Hon. Dr. Prof. Sospeter Muhongo invited VIP
to submit to him the amount of money if paid VIP
would conclusively settle VIP claims against IPTL”.
Mheshimiwa Spika, mchakato wote wa kutoa fedha katika
Akaunti ya Tegeta ESCROW ndipo ulipoanza na mauzo ya hisa za
VIP kwenda PAP na baadaye kuhitimishwa na maamuzi ya
Mahakama Kuu ya tarehe 5 Septemba, 2013 ambayo ndiyo
yaliyotumika kuhalalisha utoaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta
ESCROW tarehe 28 Novemba hadi 5 Desemba, 2013.
60
Mheshimiwa Spika, Baada ya fedha kutolewa kwenye Akaunti
ya Tegeta ESCROW Ndg. Rugemalira alipata mgao wake wa USD
million 75, ambazo ndani yake kulikuwa na kodi ya Serikali ambayo
haikukusanywa na gharama za uendeshaji wa Akaunti ya
ESCROW, fedha hizo zote zilipelekwa katika Benki ya Mkombozi.
Huko zilianza kugawiwa kwa watu binafsi. Kamati imearifiwa kuwa
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amepeleka suala
hilo TAKUKURU na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU amekiri
kuendelea na uchunguzi. Kamati pia imekabidhiwa taarifa ya
Benki za Stanbic na Mkombozi ambazo zimeonyesha namna
ambavyo fedha zilichukuliwa na watu na makampuni mbalimbali.
Mheshimiwa Spika, baada ya kupokea taarifa za benki (bank
statements) kutoka Benki ya Stanbic na Benki ya Mkombozi,
Kamati ilibaini yafuatayo: -
a) Kuwepo kwa fedha zilizohamishwa kutoka Akaunti ya PAP
iliyoko Benki ya Stanbic kwenda Akaunti ya VIP iliyoko katika
Benki ya Mkombozi.
61
b) Kuwepo kwa fedha taslimu zilizolipwa kwa watu binafsi ambao
majina yao hayaonekani lakini walifanya miamala mikubwa
kinyume cha Sheria ya Benki Kuu na Taasisi za Fedha ya
mwaka 2006.
c) Kuwepo kwa fedha walizohamishiwa watu mbalimbali katika
Akaunti zao binafsi.
d) Katika fedha ambazo zimelipwa kwa watu binafsi katika Benki
hizi yapo majina ya viongozi wa kisiasa, viongozi wa
madhehebu ya dini, Majaji na watumishi wengine wa Serikali.
Mheshimiwa Spika, Kamati inajiuliza ni nini mahusiano ya moja
kwa moja kati ya Viongozi hawa na malipo yaliyotokana na Akaunti
ya Tegeta ESCROW. Mfano kwa upande wa viongozi wa kisiasa
ambao waliingiziwa fedha katika akaunti zao binafsi ni; Mhe.
Andrew Chenge (Mb), ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa
Serikali na sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Bajeti, shilingi bilioni 1.6; Mhe. Anna Tibaijuka (Mb) na Waziri wa
62
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi shilingi bilioni 1.6; Mhe.
William Ngeleja (Mb) na ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na
Madini shilingi milioni 40.4 na Ndg. Daniel N. Yona ambaye alikuwa
pia Waziri wa Nishati na Madini shilingi milioni 40.4; Ndg. Paul
Kimiti ambaye ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Sumbawanga
shilingi milioni 40.4 na Dr. Enos S. Bukuku ambaye alikuwa
Mjumbe wa Bodi ya TANESCO aliingiziwa shilingi milioni 161.7.
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Majaji Prof. Eudes
Ruhangisa, aliingiziwa milioni 404.25 na Mhe. J.A.K Mujulizi
aliingiziwa shilingi milioni 40.4.
Mheshimiwa Spika, pia kwa upande wa Watumishi wa umma,
Ndg. Philip Saliboko ambaye alikuwa mtumishi wa RITA aliingiziwa
shilingi milioni 40.4, Ndg. Emmanuel Daniel Ole Naiko ambaye
alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)
aliingiziwa shilingi milioni 40.4 na Ndg. Lucy L. Appollo ambaye ni
Mtumishi wa TRA aliingiziwa shilingi milioni 80.8.
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Viongozi wa Madhehebu ya
Dini walioingiziwa fedha na Benki ya Mkombozi ni Askofu
63
Methodius Kilaini shilingi 80.9, Askofu Eusebius Nzigirwa shilingi
milioni 40.4 na Mchungaji Alphonce Twimann Ye Simon shilingi
milioni 40.4.
Mheshimwa Spika, Kamati ilithibitishiwa na Mkurugenzi Mkuu
wa TAKUKURU kuwa baadhi ya watu walienda kugawana fedha
kwenye Benki tajwa wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi,
mabox, magunia na lumbesa. Kutokana na muamala uliofanyika
tarehe 6 Februari, 2014 katika Benki ya Mkombozi kiasi cha shilingi
bilioni 3.3 na muamala wa Benki ya Stanbic wa tarehe 23 Januari
2014 ambapo fedha taslimu (cash) kiasi cha shilingi bilioni 73.5
zilitolewa na kugawanywa kwa watu mbalimbali kinyume cha
Sheria ya Benki Kuu na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006.
Taarifa
ya benki (bank statements) yenye majina na akaunti zote
zilizoingiziwa fedha zimeambatishwa pamoja na taarifa hii
(Kiambatisho Na. 23).
2.5.4 Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG)
64
Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa Ibara ya 59(3) ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwanasheria Mkuu wa Serikali
ndiye mshauri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo
ya sheria na anawajibika kutoa ushauri kwa Serikali kuhusu
mambo yote ya kisheria na ushauri wake ni wa mwisho.
Kamati imebaini mawasiliano mbalimbali kutoka kwa Katibu Mkuu
wa Wizara ya Nishati na Madini na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
kwa nyakati tofauti wakiomba Ushauri kwa Mwanasheria Mkuu wa
Serikali kuhusiana na njia bora za kushughulikia suala la Akaunti
ya Tegeta ESCROW. Kwa kuzingatia uchambuzi wa Taarifa ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na mahojiano,
uhusika wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika suala la utoaji
wa fedha za ESCROW ni kama ifuatavyo:
a) Kuruhusu ulipwaji wa fedha za Akaunti ya Tegeta
ESCROW kabla ya kujiridhisha na mgogoro uliokuwepo
kati ya TANESCO na IPTL
Mheshimiwa Spika, kufuatia hukumu iliyotolewa na Mheshimiwa
Jaji Utamwa mnamo tarehe 05 Septemba, 2013 na baada ya
65
kupokea barua Na. CAC/184/211/01/23 ya tarehe 30 Septemba,
2013 ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dr. Servacius Likwelile
akiwasilisha taarifa ya Wataalam iliyojumuisha Wataalam kutoka
BOT, Wizara ya Fedha, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na
Wizara ya Nishati na Madini kuhusu utolewaji wa fedha kwenye
Akaunti ya Tegeta ESCROW, Mheshimiwa Jaji Fredrick Werema
kupitia barua Kumb. Na. AGCC/E.80/6/65 ya tarehe 02 Oktoba,
2013 alimuarifu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, kuwa ameipitia
Ripoti ya wataalamu kuhusu utoaji wa fedha za Akaunti ya Tegeta
ESCROW na kwa Maoni yake alisema jambo linaloweza kuleta
tatizo katika utoaji wa fedha hizo ni hati fungani zilizowekezwa na
Benki Kuu. (Kiambatisho Na. 17).
Mheshimiwa Spika, inashangaza kuwa bila ya kufanya
uchunguzi wa kina wa mgogoro wa uhamishaji wa hisa za
Kampuni ya Mechmar kwenda Piper Links, na kisha kutoka Piper
Links kwenda PAP, na ilhali akijua fika kuwa kulikuwa na shauri
lililohusu mgogoro wa capacity charges kwenye Kituo cha
Kimataifa cha Usuluhishi wa migogoro ya Uwekezaji (ICSID 2),
Mwanasheria Mkuu badala ya kushauri kupata suluhu ya shauri
66
lililoamuliwa na ICSID 2 alitumia mamlaka yake kuelekeza fedha za
Akaunti ya Tegeta ESCROW kutolewa kwenda IPTL.
Mheshimiwa Spika, ni kwa maelekezo hayo ya mwisho ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Makubaliano ya kutolewa fedha
baina ya Wizara ya Nishati na Madini na IPTL yaliafikiwa.
b) Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya
thamani ya Shilingi 23 bilioni.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na suala la Mwanasheria Mkuu
wa Serikali kusamehe kodi ya Serikali iliyokuwepo katika akaunti
ya Tegeta ESCROW, Kamati imebaini kwamba mnamo tarehe 18
Novemba, 2013, Mwanasheria Mkuu wa Serikali alimwandikia
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania barua yenye Kumb. Na.
AGCC/E.080/6/70 akimfahamisha kwamba hapakuwa na kodi ya
Serikali iliyopaswa kukusanywa kutoka kwenye Akaunti hiyo.
Sehemu ya barua hiyo inaeleza kama ifuatavyo (Kiambatisho
Na. 18):
67
“… hata hivyo, katika suala hili la ESCROW Account
hakuna kodi inayotakiwa kukusanywa … kwa sababu
fedha iliyopelekwa kwenye kwenye Account haikuwa na
VAT iliyolipwa kwa ajili ya capacity charges”
Mheshimiwa Spika, kutokana na ukweli huo, Kamati imebaini
kwamba maelekezo ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa Gavana
wa Benki Kuu, kuwa hapakuwa na kodi ya Serikali iliyopaswa
kukusanywa kutoka kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW,
yalimsababisha Gavana wa Benki Kuu na hivyo kubariki utoaji wa
fedha hizo kabla ya kukata kodi ya Serikali. Aidha maelekezo hayo
yalikiuka masharti ya kifungu cha 5(4) cha Sheria ya Kodi ya
Ongezeko la Thamani ya Mwaka 2006.
Mheshimiwa Spika, kitendo cha Mwanasheria Mkuu wa Serikali
kutofanya mawasiliano na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA)
pamoja na kwamba ana mamlaka ya kutafsiri sheria alipaswa
kujiridhisha kwamba hapakuwa na kodi iliyopaswa kukatwa kutoka
kwenye fedha zilizokuwa kwenye Akaunti hiyo. Aidha, angeweza
kujiridhisha kutoka TANESCO iwapo fedha zilizokuwa zinapelekwa
68
kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW hazikuwa na kodi ya
ongezeko la thamani. Kwa kutotimiza wajibu huo Ofisi yake ilifanya
uzembe wa kutokufanya uchunguzi wa kina wa suala hili (due
diligence) kabla ya kutoa maelekezo kwa Benki Kuu ya Tanzania.
Mheshimiwa Spika, maelekezo ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali kwa Gavana yaliikosesha Serikali kodi ya ongezeko la
thamani (VAT) kwa kiasi cha shilingi 23,154,003,077.
c) Kutoishauri ipasavyo BOT, Wizara ya Fedha na Wizara
ya Nishati na Madini kuhusu kinga kwa Serikali
iliyotolewa na PAP
Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 27 Oktoba, 2013, IPTL ilitoa
hati ya kinga dhidi ya madai yoyote yanayoweza kujitokeza kwa
Serikali na Benki Kuu kuhusiana na fedha zilizokuwa katika Akaunti
ya Tegeta ESCROW mara baada ya fedha hizo kulipwa kwa IPTL.
Hati hiyo ilisainiwa na Bw. Harbinder Singh Sethi Mwenyekiti na
Mtendaji Mkuu wa IPTL na kushuhudiwa na Ndg. Joseph
Makandege Katibu na Wakili Mkuu wa Kampuni ya IPTL.
69
Mheshimiwa Spika, kama ilivyobainishwa katika Ukaguzi
Maalumu wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, ni
dhahiri kuwa hisa za Mechmar zilizonunuliwa na PAP kutoka
Kampuni ya Piper Links ambazo Mahakama Kuu iliziweka chini ya
uangalizi wa Martha Renju (Receiver) zina mashaka. Hivyo ilikuwa
ni jukumu la Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na mambo
mengine kutafsiri vema Hukumu ya Mheshimiwa Jaji Utamwa na
kisha kufanya uchunguzi wa kina kujiridhisha juu ya uhalali wa PAP
kumiliki hisa za Piper Links zilizohamishwa kutoka Kampuni ya
Mechmar.
Mheshimiwa Spika, kutokana na sababu tajwa hapo juu ni
dhahiri kuwa uhalali wa kinga ya PAP kwa Serikali na BOT kuhusu
hatma ya utolewaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta ESCROW
una mashaka, na hivyo kuna uwezekano wa Serikali kushtakiwa na
Mechmar muda wowote kwa madai kuwa yenyewe haikuuza hisa
zake kwa Piper Links.
2.5.5 Wizara ya fedha
70
Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha ilikuwa ndio mratibu wa
vikao vya Kamati ya Wataalam ya Serikali iliyokuwa ikishughulikia
suala la utoaji wa fedha za ESCROW. Uchambuzi wa Kamati
umethibitisha kuwa kulikuwa na mawasiliano mbali mbali
yaliyokuwa yakifanywa na Katibu Mkuu Wizara ya fedha Ndg.
Servacius Likwelile kwenda kwa Gavana wa Benki Kuu na kwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini kuhusiana na jambo
hilo.
Mheshimiwa Spika, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha ndiye
aliyekuwa kiungo katika kulipatia jawabu suala la utoaji wa fedha
katika Akaunti ya Tegeta ESCROW. Hilo limejidhihirisha pale
alipopokea taarifa ya Wataalam na kuiwasilisha kwa Katibu Mkuu
wa Wizara ya Nishati na Madini na kunakiliwa kwa Gavana wa
Benki Kuu naMwanasheria Mkuu wa Serikali kwa barua yenye
Kumb. Na.CAC/184/211/01/23 ya tarehe 30 Septemba, 2013 kwa
maamuzi.
Mheshimiwa Spika, uhusika wa Wizara ya Fedha hususan Katibu
Mkuu Ndg. Servacius Likwelile unaishia katika kuwasilisha taarifa
71
ya wataalamu ambayo baadaye inafanyiwa kazi na Mwanasheria
Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini.
2.5.6 Bw. Harbinder Singh Sethi
Mheshimiwa Spika, miongoni mwa wahusika wakuu wa suala
zima la IPTL hususan Akaunti ya Tegeta ESCROW ni Bw. Harbinder
Singh Sethi, ambaye anafahamika kama Mwenyekiti na Mtendaji
Mkuu wa IPTL na wakati huohuo kama Mkurugenzi Mtendaji na
Mmiliki wa PAP. Uhusika wake unaanzia katika ununuzi wa hisa
saba (7) za Mechmar kwenda Piper Links Investments na kisha
kutoka Piper Links Investiments kwenda PAP na hatimaye hisa 3
za VIP kwenda PAP na hivyo kumpa umiliki wa IPTL na PAP kwa
asilimia mia moja.
Mheshimiwa Spika, kama ilivyokwishafafanuliwa hapo awali na
kwa mujibu
72
wa matokeo ya Ukaguzi Maalumu, ni dhahiri kuwa Bw. Harbinder
Singh Sethi hajawahi kuwasilisha hati halisi za uhamisho wa hisa za
Mechmar kwenda Piperlinks na kisha PAP. Kwa ushahidi huo ambao
unathibitishwa na Maelezo ya Maofisa wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) na kwa nyaraka alizopeleka BRELA kwa usajili wa
Kampuni, ni dhahiri kuwa PAP sio Mmiliki halali wa IPTL na
wamejipatia fedha za kwenye akaunti ya Tegeta ESCROW kwa njia
ya udanganyifu.
2.5.7 MSAJILI WA MAKAMPUNI (BRELA)
Mheshimiwa Spika, uhusika wa BRELA katika suala zima la
utoaji wa Fedha
katika Akaunti ya Tegeta ESCROW, unatokana na ushahidi kuwa
Kamati imeshindwa kuthibitisha kama Hisa za Piper Links toka
Kampuni ya Mechmar na Hisa za PAP toka Piper Links ziliwahi
kusajiliwa BRELA kabla Fedha hazijatolewa. Katika uchunguzi wake
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alitilia mashaka
mauzo ya hisa hizo baada ya kupata uthibitisho wa uwepo wa hisa
7 za Mechmar kutoka kwa Msimamizi Martha Renju. BRELA ilisajili
73
umiliki wa hisa za PAP kwa IPTL bila kujali matakwa ya Sheria ya
Kodi ya Mapato kama ilivyofafanuliwa hapo awali.
2.5.8 Wizara ya Nishati na Madini
Mheshimiwa Spika, Hadidu ya rejea ya tisa ilimtaka Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuchunguza iwapo Wizara ya
Nishati na Madini ambayo iliingia Mkataba na IPTL wa kufungua
akaunti Maalumu ya ESCROW ilifanya uadilifu na kuweka
uangalifu wa kutosha kabla ya kuingia makubaliano na IPTL ya
kutoa fedha zilizokuwepo kwenye Akaunti hiyo na kuilipa IPTL.
Mheshimiwa Spika, Wizara ya Nishati na Madini ilikuwa mmoja
wa washirika wakati wa ufunguzi na uendeshaji wa Akaunti ya
Tegeta ESCROW. Aidha, lilikuwa ni jukumu la Wizara hii
kuhakikisha kuwa Maslahi ya Taifa na TANESCO yanalindwa
ipasavyo kabla ya kutolewa kwa fedha katika Akaunti husika.
Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia Taarifa ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Ukaguzi maalumu wa
74
miamala ya Akaunti ya Tegeta ESCROW, Kamati imebaini
yafuatayo kuhusu ushiriki na uadilifu wa Wizara ya Nishati na
Madini katika suala zima la utoaji wa fedha za ESCROW:
a) Viongozi wa Wizara kutotambua Umiliki wa Fedha za
ESCROW
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Mkataba wa ufunguaji wa
Akaunti ya Tegeta ESCROW, washirika wawili katika akaunti hiyo
walikuwa ni Wizara ya Nishati na Madini kwa niaba ya TANESCO
na IPTL na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ilikuwa ni Wakala wa
Akaunti husika kwa ajili ya utunzaji wa fedha na uwekezaji.
Mheshimiwa Spika, uthibitisho wa matamshi ya Viongozi wa
Wizara ya Nishati na Madini ya mara kwa mara kuwa umiliki wa
fedha za ESCROW ni wa watu binafsi yanatia shaka juu ya uadilifu
wao katika kulinda maslahi ya TANESCO na Taifa katika mgogoro
uliokuwapo baina ya TANESCO na IPTL.
Kamati imebani kuwa uongozi wa Wizara kwa namna moja au
nyingine umefanikisha utoaji wa fedha kwenye akaunti ya
75
ESCROW Kinyume na kipengele 2.1 cha Mkataba wa ESCROW
ambacho kinabainisha kuwa washirika wa Akaunti ya Tegeta
ESCROW ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Kampuni ya IPTL na sio vinginevyo, kama kinavyonukuliwa hapo
chini:
“The ESCROW Agent shall establish and maintain an
account, to be held in trust for the benefit of
Government of Tanzania and IPTL, and to be
designated as the “Tegeta ESCROW Account”
Mheshimiwa Spika, ni kwa msingi huo hapo juu na kwa
kuzingatia kuwa Makubaliano ya kufungua Akaunti ya Tegeta
ESCROW yalibainisha kuwa wadau wa fedha za kwenye akaunti
husika ni Serikali na IPTL, Wizara ya Nishati na Madini haikutimiza
wajibu wake ipasavyo ili kuhakikisha haki za TANESCO zinalindwa
kabla ya utoaji wa fedha husika hasa kwa dhana iliyokuwa
imejengeka miongoni mwao kuwa fedha hizo ni za wanahisa wa
IPTL na sio za Serikali au sehemu ya fedha hizo si ya Serikali.
76
Mheshimiwa Spika, Kamati ilipowahoji Mkurugenzi Mkuu wa
TAKUKURU, Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali pamoja na Kamishna Mkuu wa TRA walithibitisha kuwa
sehemu ya fedha zilizokuwemo kwenye Akaunti ya Tegeta
ESCROW ilikuwa ni ya Serikali kwa maana kwamba kwa vyovyote
vile palikuwa na fedha za umma katika Akaunti husika.
b) Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini kubadili
msimamo wake kuhusu umiliki wa Fedha za kwenye
Akaunti ya Tegeta ESCROW
Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 16 Septemba, 2013, Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Eliakim Maswi
alimwandikia barua Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na
mambo mengine kuomba ushauri wa kisheria kuhusu Akaunti ya
Tegeta ESCROW huku akimfahamisha kuwa wamepokea jalada la
hukumu ya mahakama kuu kuhusu uamuzi wake wa tarehe 05
Septemba, 2013 uliokuwa ukiiondoa IPTL kuwa kwenye ufilisi.
77
Mheshimiwa Spika, katika barua hiyo Katibu Mkuu, Wizara ya
Nishati na Madini anamfahamisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali
kuwa:
“The ESCROW Account was established as a
result of tariff dispute between TANESCO and
IPTL on the power generated by IPTL, therefore
the ownership of the money in the ESCROW
Account will only be established after the tariff
dispute is resolved…. We are of the opinion that
PAP will be entitled to the amount which belongs
to the IPTL after the dispute is resolved and not
the entire amount in the ESCROW Account”
Mheshimiwa Spika, pamoja na msimamo huo wa Katibu Mkuu
wa Wizara ya Nishati na Madini kuwa umiliki wa fedha za ESCROW
au sehemu ya fedha hizo ni ya Umma, tarehe 20 Septemba, 2013
siku nne baada ya kuwa na mtizamo kuwa fedha za ESCROW ni za
Umma au kiasi chake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
alimjulisha Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa IPTL Bw. Harbinder
78
Singh Sethi ambaye pia ni Mmiliki wa PAP kupitia barua yenye
Kumb. Na. SBD.88/147/01/4 (Kiambatisho Na. 19) kuwa Wizara
haikuwa na pingamizi dhidi ya kutolewa kwa fedha za ESCROW
kama bwana Sethi angewasilisha ushahidi wa kuuzwa kwa hisa
asilimia 70 za Mechmar katika IPTL na kutoa kinga kwa Serikali na
TANESCO baada ya utoaji wa fedha hizo.
Mheshimiwa Spika, Kamati imepata mashaka makubwa juu ya
sababu iliyomshawishi Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
kubadili msimamo na kuondoa masharti yake ya awali kwa
Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa IPTL ndani ya siku nne na
kuamua kuwa Wizara haioni tena kikwazo cha kuruhusu utoaji wa
fedha ikiwa ni Kinyume kabisa na mkataba wa ESCROW uliohitaji
kukamilika kwa mgogoro baina ya TANESCO iliyokuwa ikisimamiwa
na Wizara na IPTL.
c) Wizara ya Nishati na Madini kutojiridhisha ipasavyo na
Uhamishaji
wa Hisa za Mechmar kwenda Piper Links na baadaye
kwenda PAP
79
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na kisha
kuthibitishwa na ushahidi katika mahojiano ya Kamati, imebainika
kuwa kuna utata mkubwa kuhusu uhamisho wa hisa za Mechmar
kwenda Piperlink na baadaye kwa PAP. Ushahidi uliopatikana hadi
Akaunti ya Tegeta ESCROW inafunguliwa ulionyesha kuwa
Mechmar ilikuwa mmiliki halali wa IPTL (Kiambatisho Na. 3).
Aidha, uchunguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali ulibainisha kuwa Mechmar waliuza hisa zao saba kwa Piper
Link Investment mnamo mwaka 2010 kwa USD milioni 6,
japokuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alibaini
kuwa hati halisi ya umiliki wa hisa hizo bado inashikiliwa na Martha
Renju huko BVI, hii inathibitisha kuwa hapakuwa na uhalali wa
PAP kumiliki IPTL na kisha kulipwa fedha zilizokuwa kwenye
Akaunti ya Tegeta ESCROW.
Mheshimiwa Spika, Kamati iliendelea kubaini kuwa makubaliano
ya uuzwaji wa hisa za Mechmar kwenda kwa Piper Links
Investment yamejaa utata mkubwa kutokana na uchunguzi wa
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kubaini kuwa
watia saini katika makubaliano husika hawakuainisha majina yao
80
dhidi ya sahihi walizoweka, hivyo kutoa tafsiri kuwa kuna jambo
lilikuwa linafichwa kwa makusudi. (Kiambatisho Na. 8).
Mheshimiwa Spika, ni dhahiri kuwa Wizara ya Nishati na Madini
kupitia kwa Katibu Mkuu wa Wizara, haikufanya jitihada za
kutosha kuhakiki mauziano hayo ya hisa kama alivyokuwa
ameomba hapo awali. Katibu Mkuu, Nishati na Madini Ndg. Eliakim
Maswi kupokea makubaliano ya uuzaji wa hisa za Piper Links
Investment kwenda PAP bila kujiridhisha na kufahamu kuwa hisa
hizo zimeshikiliwa na mtu binafsi inathibitisha mashaka ya Kamati
kuwa Katibu Mkuu huyo kwa uzembe au kwa makusudi amehusika
katika kufanikisha utoaji wa fedha za Akaunti ya Tegeta ESCROW
bila kuzingatia taratibu husika.
Mheshimiwa Spika, Waziri wa Nishati na Madini ndiyo mamlaka
ya kuthibitisha uhamishaji wa umiliki wa Kampuni katika sekta
yake. Sheria ya Kodi ya Mapato Kifungu cha 90 (2) kinaitaka
mamlaka hii kutotambua uhamisho wa umiliki mpaka kwanza
itakapopatikana hati ya kodi kutoka TRA. Kamati iliona Wizara
ikiitambua PAP kwa barua zake tu bila kujali matakwa ya kisheria.
81
d) Wizara ya Nishati na Madini kuingia makubaliano ya
utoaji wa fedha za ESCROW bila kupata ufumbuzi wa
masuala yenye utata.
Mheshimiwa Spika, pamoja na mapungufu yaliokwishaonekana
hapo awali mnamo tarehe 21 Oktoba, 2013 Katibu Mkuu Wizara ya
Nishati na Madini Bw. Eliakim Maswi pamoja na Mwanasheria wa
Wizara hiyo Bi. Salome Makange kwa niaba ya Serikali waliingia
makubaliano na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa IPTL, Bw.
Harbinder Singh Sethi na Mwanasheria wa IPTL Bw. Joseph
Makandege juu ya utoaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta
ESCROW (Agreement for delivery of funds to Independent Power
Tanzania Limited (IPTL) (Kiambatisho Na. 10).
Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia uchunguzi wa Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na uchambuzi wa Kamati
ambao ulibainisha dosari nyingi zilizotakiwa kufanyiwa kazi na
Wizara ya Nishati na Madini kabla ya kusaini makubaliano ya kutoa
fedha zilizokuwemo kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW, ni dhahiri
kuwa uharaka wa mawasiliano kati ya Wizara ya Nishati na Madini
na Kampuni ya PAP hadi kutolewa kwa fedha yanatia mashaka na
82
ni muhimu kujiuliza uharaka huo ulisababishwa na jambo gani.
Suala hili linatia shaka uadilifu wa Viongozi wa Wizara ya Nishati
na Madini kwa jinsi walivyoshughulikia.
2.6 MADENI YA IPTL
2.6.1 Uhalali wa Madai ya Benki ya Standard Chartered ya Hong
Kong kwa IPTL (USD. 125,970,570.57)
Mheshimiwa Spika, Kamati imebaini kuwa madai ya Benki ya
Standard Chartered ya Hong Kong kwa IPTL ni halali. Madai hayo
yanatokana na Benki hiyo kununua deni la IPTL kwa Umoja wa
Mabenki ya Malaysia (Consortium of Malaysian Banks) Mwezi
Agosti 2005. Kimsingi baada ya TANESCO kuingia Mkataba wa
kununua umeme wa IPTL, Kampuni ya IPTL iliingia pia Mkataba na
Umoja huo wa mabenki tarehe 28 Juni 1997 kwa ajili ya mkopo wa
jumla ya USD. 105,000,000 ili kuwezesha Ujenzi wa mradi wa
ufuaji wa umeme uliopo Tegeta. Ingawa, ni kiasi cha USD
85,862,022 tu kati ya USD. 105,000,000 ndicho pekee
83
kilichopokelewa na IPTL katika ya Mwezi Agosti 1997 hadi
Desemba 1999.
Mheshimiwa Spika, pamoja na kwamba kumekuwa na mvutano
juu ya uhalali wa madai ya SCB-HK ikielezwa kuwa matakwa ya
kifungu Na. 79 (1) na Kifungu Na. 172 vya Sheria ya Makampuni
CAP 212 (iliyorekebishwa mwaka 2002) hayakutimizwa kwa IPTL
kutowasilisha makubaliano yaliyoingiwa kuhusu deni hili na
dhamana zake26, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
amethibitisha uhalali wa madai ya SCB-HK kwa kuzingatia
yafuatayo:
a) Uamuzi wa Shauri Na. ARB/10/20 lililofunguliwa ICSID ulioeleza
kuwa kutosajiliwa kwa makubaliano yenye maslahi ya dhamana
‘Security Interest’ haiondoi uhalali wa deni dhidi ya Kampuni
husika.
b) IPTL ilikuwa ikifanya marejesho hata baada ya deni hilo
kununuliwa na SCB-HK, ambapo hadi kufikia mwaka 2007
26 Kifungu cha 79(1) cha Sheria hiyo kinaelekeza kuwa makubaliano yeyote yanayoingiwa na kampuni
iliyosajiliwa Tanzania yanayogusa maslahi katika mali na biashara zake, yanatakiwa yawasilishwe pamoja na
nyaraka zinazoshuhudia kwa Msajili wa Makampuni Tanzania ndani ya Siku 42 baada ya tarehe ya makubaliano
hayo.
84
ilikuwa imelipa jumla ya USD 58.69 milioni na kati ya hizo USD
20 milioni zililipwa kwa SCB-HK.
c) Hukumu ya tarehe 5 Septemba, 2013 ya Mahakama Kuu ya
Tanzania ilirejesha IPTL kuwa Kampuni hai.
Mheshimiwa Spika, ikumbukwe kwamba capacity charges
humwezesha mwekezaji kulipia mtaji wake (Return on Equity) na
kulipia mkopo. Kati ya mwaka 2002 hadi 2006 TANESCO ilikuwa
inalipa capacity charges katika kiwango kamili na hivyo IPTL
walipaswa kuwa wamekamilisha kulipa mikopo yao. Aidha, katika
kipindi hicho TANESCO iliilipa IPTL ziada ya shilingi bilioni 152
ambazo zingepaswa kumaliza deni hilo. Hivyo, deni la USD
125,970,570.57 ambalo Standard Chartered Bank Hong Kong
inaidai IPTL linapaswa kulipwa na Mechmar na siyo TANESCO.
2.6.2 Uhalali wa Madai ya TANESCO kwa IPTL (Sh.
321,041,364,000)
Mheshimiwa Spika, Kamati imejiridhisha kuwa madai ya
TANESCO kwa IPTL ni ya msingi na yana uhalali ingawa usahihi
85
wa madai (kiasi cha deni) hayo utapatikana tu baada ya kufanyika
kwa mambo yafuatayo;
a) Kutekelezwa kwa uamuzi uliotolewa na Kituo cha Usuluhishi wa
Migogoro ya Uwekezaji cha Kimataifa (ICSID) mwezi Februari
2004 (ICSID 2). Aidha, ICSID 2 ilielekeza TANESCO na IPTL
kukokotoa upya kiwango cha capacity charges.
b) TANESCO na IPTL kukubaliana kuhusu usahihi wa madai ya
TANESCO baada ya washirika hao kukubaliana kuhusu kiwango
sahihi cha Capacity charges.
2.6.3 Uhalali wa madai ya Watsila Tanzania Ltd (USD.
7,730,018.16) Watsila Netherlands B.V
(USD.11,908,195.70 na GBP. 1,439,836.50 ) kwa IPTL
Mheshimiwa Spika, Kamati imebaini kuwa Madai ya Watsila
Tanzania Ltd USD 7,730,018.16 yanayotokana na utekelezaji wa
Mkataba wa uendeshaji na ukarabati wa Mitambo ya IPTL na
Madai ya Watsila Netherlands B.V ya USD 11,908,195.70 na Pauni
za Kiingereza 1,439,836.50 yanayotokana na utekelezaji wa
86
Mkataba wa Ujenzi wa Mitambo ya IPTL ni madai halali. Aidha,
Kamati imepata uthibitisho kuwa wadeni hao wawili wanaendelea
kulipwa na IPTL katika utaratibu waliokubaliana.
2.6.4 Wadai wa IPTL walioainishwa katika Taarifa ya Mfilisi hadi
kufikia tarehe 5 Septemba, 2013
Mheshimiwa Spika, kwa sababu zisizoeleweka Taarifa ya Mfilisi
wa muda (RITA) iliyotolewa tarehe 5 Septemba, 2013 wakati wa
makabidhiano ya IPTL kutoka kwake kwenda kwa PAP, madeni
yaliyoorodheshwa yalikuwa ya USD 14,623,062.02 tu bila
kujumuisha madai ya Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong,
TANESCO, Watsila Tanzania Ltd na Watsila Netherlands B.V
yaliyoainishwa hapo juu.
2.6.5 Tahadhari iliyochukuliwa na Serikali dhidi ya Madai
yanayoweza kujitokeza
Mheshimiwa Spika, Kamati imebaini kuwa Serikali haikuchukua
tahadhari ya kutosha dhidi ya madai mengine yanayoweza
kujitokeza kabla ya kutolewa kwa fedha katika Akaunti ya Tegeta
87
ESCROW. Licha ya kwamba IPTL kupitia barua Na. IPTL/GEN/010-
2013 ya tarehe 28 Oktoba, 2013 (Kiambatisho Na. 20)
iliwasilisha kinga yake kwa Serikali na Benki Kuu dhidi ya madai
yanayoweza kujitokeza.
Mheshimiwa Spika, Serikali ilitakiwa kujiridhisha kuhusu uhalali
wa PAP kumiliki IPTL na hivyo uhalali wa kinga inayotolewa na
IPTL ikizingatiwa kwamba kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa TRA
na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU mchakato wa Piper Links
kununua hisa za Mechmar na kisha PAP kununua hisa za Piper
Links haukuwa halali na TAKUKURU wanaendelea na uchunguzi
zaidi kuhusu mauziano ya hisa husika. Kwa sababu hizo, Kamati
ina wasiwasi na uhalali wa kinga hiyo suala ambalo linaweza
kusababisha hasara kwa Serikali endapo Mechmar itathibitisha
kutouza hisa zake kwa kuwa bado zinashikiliwa na mtu binafsi.
2.7 HATUA ZILIZOCHUKULIWA BAADA YA UAMUZI WA
MAHAKAMA KUU
Mheshimiwa Spika, Kamati haikuridhishwa na jinsi Serikali
ilivyotafsiri hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania chini ya Mhe.
88
Jaji J.H.K Utamwa iliyotolewa tarehe 5 Septemba 2013 ambayo
ikielekeza utekelezaji wa masuala yote matano (5) kama
yalivyoombwa na VIP Engineering & Marketing (Kiambatisho Na.
21).
Mheshimiwa Spika, Hukumu husika ilihusu utatuaji wa mgogoro
wa wanahisa ambapo, pamoja na mambo mengine ilimuamuru
Mfilisi wa muda kukabidhi mali zote za IPTL, ikiwa ni pamoja na
mtambo wa kuzalisha umeme kwa Kampuni ya PAP ambayo
ilidhamiria kuwalipa wadai wote halali wa IPTL na kuongeza uwezo
wa mtambo hadi kufikia MW 500 na kuuza umeme kwa TANESCO
kwa bei ya kati ya USD 0.6 hadi 0.8 kwa uniti moja ya umeme.
Mheshimiwa Spika, hukumu hii haikuhalalisha PAP kulipwa
fedha zilizokuwa kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW kwa sababu
fedha hizo ziliwekwa chini ya makubaliano kati ya Serikali na IPTL
kutokana na madai kuwa TANESCO wamekuwa wakitozwa
capacity charges kubwa. Hivyo, utoaji wa fedha hizo ungefanyika
tu kama TANESCO na IPTL wangepata suluhisho la mgogoro huo
na kisha kwa pamoja kusaini hati ya makubaliano na kuomba
kutolewa kwa fedha hizo wakionyesha kiasi ambacho kinatakiwa
89
kulipwa kwa mshirika anayestahili kulipwa (Kiambatisho Na. 3).
Hivyo, kwa Serikali kutumia hukumu hiyo ya Mahakama kama
kigezo mahsusi cha kutoa fedha kwenye Akaunti ya Tegeta
ESCROW haikuwa sahihi.
Mheshimiwa Spika, Kamati haikuridhishwa pia na jinsi Serikali
ilivyojipanga kutekeleza uamuzi huo wa mahakama ikizingatiwa
kuwa uamuzi huo unaitaka IPTL kuongeza uzalishaji wa umeme
kufikia megawati 500 wakati Mkataba wa kununua umeme (PPA)
baina ya TANESCO na IPTL wa mwaka 1995 ulikuwa wa uzalishaji
wa megawati 100 tu. Serikali hadi sasa haijapitia na kujadili upya
utekelezaji wa Mkataba husika hivyo kuna hatari ya Serikali kupitia
TANESCO kuingia katika migogoro mipya.
Mheshimiwa Spika, Kamati ilishangazwa kuona kwamba katika
hali isiyo ya kawaida, Mahakama katika Shauri hilo tajwa ilikwenda
mbali zaidi hadi kupanga kiwango cha bei ya umeme kuwa USD
0.6 hadi 0.8 kwa uniti moja ya umeme, ikizingatiwa kuwa bei ya
umeme hupangwa katika mkataba wa mauziano ya umeme au
mwenendo wa soko.
90
3.0 MAONI NA MAPENDEKEZO YA KAMATI
3.1 MAONI YA KAMATI
Mheshimiwa Spika, baada ya kupitia hadidu rejea kumi
zilizochambuliwa hapo juu na kuzipatia majibu yote kwa mujibu wa
Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu
ukaguzi maalum katika akaunti ya Tegeta ESCROW, Kamati
inapaswa kutoa mapendekezo ya njia sahihi za kisheria zinazoweza
kutumika kwa ajili ya kulinda Serikali isipate hasara tena katika
utekelezaji wa Mkataba wa Uzalishaji umeme kati ya TANESCO na
IPTL. Vilevile Kamati inatoa mapendekezo juu ya hatua stahiki
ambazo zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya wahusika kulingana na
matokeo ya ukaguzi maalumu.
91
Mheshimiwa Spika, Kamati imethibitisha bila chembe ya
mashaka kwamba mchakato mzima wa kutoa fedha katika akaunti
ya Tegeta ESCROW uligubikwa na mchezo mchafu na haramu
wenye harufu ya kifisadi ulioambatana na udanganyifu wa hali ya
juu ambao kwa kufuata sheria tu ungeweza kugundulika na
kuzuiwa. Hata hivyo, Mheshimiwa Spika, mfumo mzima wa Serikali
ni kama ulipata ganzi au uliganzishwa ili kuwezesha zaidi ya
shilingi bilioni 306 kuporwa kutoka Benki Kuu ya Tanzania na
kutakatishwa kupitia Benki mbili hapa Nchini na baadhi ya mabenki
ughaibuni.
Mheshimiwa Spika, Kamati imethibitisha kuwa hukumu ya Jaji
Utamwa ya kukabidhi masuala yote ya IPTL kwa Kampuni ya PAP,
ilitafsiriwa vibaya kwanza na Bwana Harbinder Singh Sethi
mwenyewe na baadaye ikatafsiriwa vibaya pia na viongozi wa
Wizara ya Nishati na Madini, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na
hata baadhi ya viongozi wakuu wa Serikali akiwemo Mheshimiwa
Waziri Mkuu. Tafsiri hii potofu ilirudiwa rudiwa na kuimbwa na
viongozi wa Wizara kiasi cha kuliaminisha Bunge na Umma
kwamba ndio ilikuwa tafsiri sahihi. Baada ya kupata ushahidi usio
na mashaka kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
92
Serikali na Mamlaka ya Mapato Tanzania, ni dhahiri Kampuni ya
PAP haikuwa na uhalali wowote wa umiliki wa IPTL wakati inalipwa
fedha za kutoka Akaunti ya Tegeta ESCROW.
Mamlaka ya Mapato Tanzania kupitia uchunguzi wake imebaini
kukiukwa kwa Sheria ya Kodi ya Mapato Sura ya 333, kifungu cha
90 (2) kama ilivyofanyiwa marekebisho na sheria ya Fedha, sheria
namba 8 ya mwaka 2012 kuhusiana na mabadiliko ya umiliki wa
hisa kutoka Kampuni moja kwenda nyingine zilizoko nje ya
Tanzania na zenye mali hapa Tanzania. Vile vile uchunguzi
umeonyesha ukwepaji mkubwa wa kodi uliotokana na kuwasilisha
nyaraka za kughushi kulikofanywa na mawakala wa Kampuni ya
PAP ambapo hata kama wangekuwa wamefuata sheria hiyo hapo
juu bado wangekuwa wamesababisha ukwepaji kodi wa shilingi
8.7 bilioni.
Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 19 mwezi Novemba 2014,
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania alimwandikia
barua Msajili wa Makampuni (BRELA) akionesha kusudio la
kuondoa uhalali wa hati za malipo ya kodi ya ongezeko la mtaji
(capital gains tax certificates) zilizolipwa kuthibitisha mauzo ya hisa
93
za Mechmar kwenda Piperlink na baadaye PAP akitoa siku 6. Barua
hiii iliwasilishwa mbele ya Kamati. Hivi sasa tunavyowasilisha
taarifa hii siku sita zilikamilika jana bila Kampuni ya PAP kuchukua
hatua zozote za kufanya malipo halisi na halali kama Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato alivyoelekeza.
Mheshimiwa Spika, CAG amebainisha pia kuwa Bwana
Harbinder Singh Sethi hana hati halisi ya hisa za Kampuni ya
Mechmar katika IPTL maana zilizuiwa na Mahakama ya British
Virgin Island. Hivyo Kamati inaitaka Serikali kwenda mahakamani
kuomba mapitio ya hukumu ya Jaji Utamwa, J na kwa kutumia
ushahidi huu ili kuirejesha IPTL katika hali iliyokuwa awali.
Mheshimiwa Spika, Kamati pia imeridhika kuwa Mkataba wa
IPTL uligubikwa na tuhuma za ufisadi toka kuanza kwake, tuhuma
ambazo mara kadhaa zimethibitishwa na maafisa waandamizi wa
Serikali na hata Baraza la Kimataifa la Usuluhishi wa Migogoro ya
Uwekezaji (ICSID 1) kupelekea kushusha gharama za uwekezaji
wa mitambo hiyo. Mkataba huu pia umekuwa ukikiukwa mara kwa
mara bila kujali (impunity) ikiwemo kukosekana kwa Kamati ya
pamoja ya uendeshaji kama ilivyoonyeshwa katika taarifa ya CAG.
94
Kamati inaitaka Serikali, kwa mujibu wa Sheria na kwa kutumia
mkataba wa mauziano umeme kati yake na IPTL, kuuchukua
mtambo huu na kuumilikisha kwa Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO).
Mheshimiwa Spika, Kamati inakubaliana na Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali kwamba Benki ya Standard Chartered
ilikuwa na madai yake katika IPTL kufuatia kunununua deni
lililotolewa kwa IPTL na mabenki ya Nchini Malaysia. Vile vile
Kamati imethibitisha kuwa mkopo uliotolewa ni wa thamani ya
Dola za kimarekani 105 milioni, lakini zilizotumika kwa ajili ya
mradi huu ni Dola za kimarekani 85 milioni tu. Hata hivyo, Kamati
inapenda kulifahamisha Bunge lako tukufu, kama
tulivyokwishasema huko awali, kwamba kupitia malipo ya ‘capacity
charges’ kati ya mwaka 2002 – 2006 ambapo TANESCO ililipa
ziada ya shilingi 152 bilioni, deni hili lilipaswa kuwa limelipwa.
Ikumbukwe kuwa ‘capacity charges’ ni malipo ya mtaji na mkopo
na sio malipo ya huduma ya umeme ulionunuliwa. Kwa maana hii
Benki ya SCB-HK haipaswi kuwa na madai yeyote yale dhidi ya
Serikali ya Tanzania au TANESCO wala haki ya dhamana ya
95
Serikali kwa IPTL. Kwa kuwa Kamati inapendekeza kuchukuliwa
kisheria kwa Kampuni ya IPTL na kuimilikisha kwa Shirika la
TANESCO, Serikali ielekezwe kwanza kuchunguza malipo ya
‘capacity charges’ yaliyolipwa kati ya mwaka 2002 – 2006 kama
yalihudumia mkopo kabla ya makubaliano yeyote na Benki ya SCB
– HK ili kukwepa kulipa mkopo huo mara mbili.
Mheshimiwa Spika, Kamati imethibitisha kuwa Bwana Harbinder
Singh Sethi kwa makusudi na kwa lengo la kujitwalia fedha
alifanya udanganyifu, kuwasilisha nyaraka za kughushi za umiliki
wa hisa 70% za Kampuni ya Mechmar katika Kampuni ya IPTL
kwenda Kampuni ya PiperLink iliyopo ‘offshore’ na kisha kwenda
Kampuni anayomiliki ya PAP. Vile vile Bwana huyu alifanya ujanja
kwa kushirikiana na viongozi waandamizi wa Serikali, maafisa wa
BRELA na maafisa wa ngazi ya chini wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania na hivyo kufanikiwa kuchota fedha asizostahili jumla ya
shilingi 306 bilioni kutoka Benki Kuu ya Tanzania. Fedha hizo
ziliwekwa katika akaunti nambari 9120000125294 ya Kampuni ya
PAP iliyopo Benki ya Stanbic, jijini Dar es Salaam, akaunti ambayo
ilifunguliwa tarehe 28 Novemba 2013 kwa kazi maalumu na kisha
kufungwa tarehe 16 Septemba, 2014. Kamati imeridhika kuwa
96
Bwana Harbinder Singh Seth alikiuka Sheria za kodi, alijipatia mali
asiyostahili na hivyo kuhujumu uchumi wa Nchi yetu na
alitakatisha fedha haramu kwa kuzitumia kununua hisa 30% ya
Kampuni ya VIP inayomilikiwa na Bwana James Rugemalira kwa
thamani ya dola za kimarekani 75 milioni.
3.2 Kamati inapendekeza kama ifuatavyo: -
3.2.1 Mheshimiwa Spika, Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) mara moja
wachukue hatua ya kumkamata Bwana Harbinder Singh Sethi na
kumfikisha mahakamani kwa makosa ya Anti money laundering,
ukwepaji kodi na wizi. Kamati pia inaelekeza Serikali kutumia
sheria za Nchi, ikiwemo sheria ya ‘Proceeds of Crime Act’
kuhakikisha kuwa Bwana Harbinder Singh Sethi anarejesha fedha
zote alizochota kutoka Benki Kuu ya Tanzania. Kwa kuwa suala hili
ni suala la utakatishaji wa fedha haramu, Mamlaka ziwasiliane na
mamlaka za Nchi nyingine kuhakikisha mali za Bwana huyu
zinakamatwa na kufidia fedha hizo.
97
3.2.2 Mheshimiwa Spika, Kamati imethibitsha kuwa Bwana James
Rugemalira aliuza hisa ambazo Kampuni yake ya VIP inamiliki
katika IPTL na kulipwa na Bwana Sethi kutoka katika Fedha za
Akaunti ya Tegeta ESCROW. Kamati imethibitisha kuwa fedha
kutoka akaunti za Kampuni ya PAP katika Benki ya Stanbic
zilizofunguliwa maalumu kwa ajili ya kupokea fedha kutoka
Akaunti ya Tegeta ESCROW iliyokuwa Benki Kuu zilipelekwa katika
Akaunti nambari 00151002368801 na Akaunti nambari
00151002368802 za Kampuni ya VIP ziliyopo Mkombozi
Commercial Bank.
Kwa mujibu wa Taarifa ya CAG na kuthibitishwa na Mkurugenzi
Mkuu wa TAKUKURU fedha hizo pia ziligawiwa kwa watu
mbalimbali binafsi. Kamati haina tatizo na watu wawili kuuziana
makampuni yao kwa thamani wajuazo wenyewe, au jinsi ya
kuzitumia fedha zao, ama kuwachagulia watu wa kuwagawia,
lakini Kamati imejidhihirishia kuwa fedha iliyotumika kulipia
manunuzi hayo ni fedha ambayo sehemu yake ni ya umma
iliyochotwa bila huruma wala aibu, kutoka Benki Kuu. Hivyo,
Kamati inazitaka mamlaka za uchunguzi kuhakikisha kuwa fedha
hizo zinarudi Benki Kuu hata ikibidi kwa kufilisi mali za watu wote
98
waliofaidika na fedha hizo kwa thamani ya fedha walizopewa na
Bwana Rugemalira.
Mheshimiwa Spika, baadhi ya waliofaidika na fedha hizo ni
Viongozi wa Umma ambao wanapaswa kuzingatia Sheria ya
Maadili ya Viongozi wa Umma (Sheria namba 13 ya Mwaka 1995)
ambayo inawataka kutoa taarifa ya zawadi wanazopokea au
malipo wanayolipwa. Vyombo vya uchunguzi vifanye uchunguzi
kutambua kama walifuata matakwa ya sheria na hatua mahsusi
zichukuliwe, ikiwemo kuvuliwa nyadhifa zao zote za kuchaguliwa
na/au kuteuliwa, kufilisiwa mali zao na kushtakiwa mahakamani
kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
ibara ya 132 (1) – (6).
3.2.3 Mheshimiwa Spika, Kamati pia imethibitisha kwamba fedha
zilizolipwa kwa Watu binafsi zilitokana na Akaunti ya Tegeta
ESCROW zilizolipwa kwa PAP ambayo si mmiliki halali wa IPTL.
Kwa maana hiyo fedha hizo zilitolewa kwa watu hao kama rushwa
na kuzitakatisha fedha hizo haramu. Aidha, kamati inapendekeza
kwamba Akaunti zote zilizohusika na miamala hii haramu ya
Akaunti ya Tegeta ESCROW, akaunti zao zifungwe (freeze) na
99
wenye akaunti hizo walazimishwe kurejesha fedha hizo kwa
mujibu wa Sheria (Anti Money Laundering) ikiwa ni pamoja na mali
zao kufilisiwa. Kwa upande wa viongozi wa Kisiasa wawajibike na
Watumishi wa umma wafukuzwe kazi.
3.2.4 Mheshimiwa Spika, Kamati imejiridhisha kwamba, suala la
akaunti ya Escrow ni jambo la utakatishaji wa fedha (Money
Laundering), kama alivyosema Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU
katika mahojiano yake na Kamati. Kamati inazitaka mamlaka
zinazohusika, ikiwemo Benki Kuu kuzitangaza benki za Stanbic na
Mkombozi Commercial Bank kama asasi za utakatishaji fedha
(Institutions of Money Laundering Concern).
3.2.5 Mheshimiwa Spika, Aidha, Kamati inalikumbusha Bunge lako
tukufu pendekezo muhimu lililotolewa na Kamati Teule ya
Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe kuhusu sakata la maarufu
la Richmond. Kamati ilipendekeza:
“Mkataba kati ya TANESCO NA Richmond Development
Company LLC na sasa Dowans Holdings S.A. kama ilivyo
mikataba kati ya TANESCO na IPTL, SONGAS, AGGREKO
100
na Aistom Power Rentals inatoa unafuu usiostahili kwa
makampuni hayo ya umeme na kuiumiza TANESCO na
hatimaye watumiaji na walipa kodi kimapato, k.m.
mikataba hiyo kuwa na vipengele vya kuibana TANESCO
kuyalipa makampuni hayo kodi zinazohusika na
uendeshaji (operations) matengenezo/marekebisho ya
mara kwa mara ya mitambo (maintenance) gharama za
bima, ada za mawakili na washauri elekezi (consultants)
gharama za mafuta na gesi ya kuendeshea mitambo,
gharama za ukodishaji mitambo (capacity charges)
ambazo TANESCO hulipa kila mwezi si chini ya wastani
wa shilingi bilioni 2 kwa kila kampuni, izalishe au
isizalishe umeme. Kamati Teule inatoa rai kwa Serikali
kuwa mikataba yote hii ipitiwe upya mapema
iwezekanavyo kama ambavo mikataba ya madini
knavyopitiwa upya sasa na Serikali. Bila kufanya hivyo,
mzigo mkubwa wa gharama za umeme utawaelemea
wananchi na kushindwa kufikia azma ya Serikali ya
maisha bora kwa kila Mtanzania.”
101
Mheshimiwa Spika, Kamati inapendekeza kwamba, azimio hili
litekelezwe kwa kupitia upya mikataba yote ya umeme ambayo
inalitafuna Taifa letu.
3.2.6 Mheshimiwa Spika, Kamati imejiridhisha kuwa Bodi ya Shirika la
Ugavi wa Umeme Nchini (TANESCO) bila sababu zozote za msingi
ilikataa mapendekezo ya Menejimenti ya Shirika ya kutoruhusu
uchotwaji wa fedha kutoka Benki Kuu akaunti ya Tegeta ESCROW
na hivyo kusababisha kulikosesha Shirika fedha zake inazohitaji
sana kutokana na hali mbaya ya Shirika. Ikumbukwe kuwa Shirika
la TANESCO lilipata hasara ya shilingi bilioni 467.7 katika mwaka
wa fedha unaoishia Desemba 31, 2013. Hasara hiyo imekuwa
ikiongezeka mwaka hata mwaka toka mwaka 2010 (bilioni 5),
2011 (bilioni 43), 2012 (bilioni 177) na hivyo hadi kufikia Desemba
31, 2013, jumla yote kuu ya hasara (accumulated loss) ilikuwa
imefikia shilingi trilioni 1.45.
Kamati pia imethibitisha kuwa Bodi ya TANESCO mpaka sasa
haijatekeleza hukumu ya ICSID 2 na kukokotoa upya viwango vya
malipo ya ‘capacity charges’ na hivyo kupelekea TANESCO na
Serikali kuendelea kuilipa IPTL/PAP kila mwezi shilingi Bilioni 4.5
102
($2.6m kila mwezi) izalishe au isizalishe umeme. Kamati inaitaka
Serikali kuvunja mara moja Bodi ya TANESCO na TAKUKURU
iwafungulie mashtaka ya matumizi mabaya ya ofisi wajumbe wote
waliohusika kupitisha maamuzi hayo ya kifisadi, ili iwe fundisho
kwa wajumbe wengine wa bodi za Mashirika ya Umma kwamba
watahukumiwa kwa maamuzi mabovu wanayoyafanya.
3.2.7 Mheshimiwa Spika, Kamati imethibitisha kuwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini aliingia makubaliano ya kutoa fedha
katika Akaunti ya Tegeta ESCROW bila kujiridhisha kikamilifu kuwa
maamuzi ya hukumu ya ICSID 2 yalikuwa bado kutolewa na hivyo
kusababisha fedha kutolewa bila kukokotoa upya gharama za
‘capacity charges’, jambo ambalo limesababisha kupoteza fedha za
umma.
Vile vile, Kamati imebaini kuwa, Katibu Mkuu hakufanya uchunguzi
wa kina (due diligence) kujiridhisha uhalali wa Kampuni ya
Mechmar kuuzwa kwa Piperlink na baadaye kuuzwa kwa PAP, na
hivyo kusababisha fedha za akaunti ya Tegeta ESCROW kulipwa
kwa asiyestahili na kinyume cha Mkataba wa akaunti ya Escrow.
Kwa maana hiyo, Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini,
103
pengine kwa uzembe wake ama kwa kukusudia kwa sababu
anazozijua yeye mwenyewe zaidi, amesaidia uchotwaji na
hatimaye utakatishaji wa fedha haramu.
Mheshimiwa Spika, Kamati pia imethibitisha uzembe wa hali ya
juu uliofanywa na Katibu Mkuu huyo, kushindwa kujiridhisha kama
masharti ya Sheria ya kodi ya Mapato Sura ya 333, Kifungu cha
90(2) yalitekelezwa. Kifungu hicho kimsingi kinaitaka mamlaka ya
‘approval’’ ya uhamishaji wa Makampuni kutotambua Kampuni
mpaka kwanza kodi za uhamishaji ziwe zimelipwa na hati za
malipo ya kodi zimetolewa na mamlaka ya kodi.
Mheshimiwa Spika, Kamati inapendekeza kuwa uteuzi wa Katibu
Mkuu huyu utenguliwe, na TAKUKURU wamfikishe mahakamani
mara moja, kwa kuikosesha Serikali Mapato, matumizi mabaya ya
ofisi na kusaidia utakatishaji wa fedha haramu.
3.2.8 Mheshimiwa Spika, Kamati imethibitisha kuwa Naibu Waziri wa
Nishati na Madini alisema uongo Bungeni kwa kutamka kauli
ambazo zilizokuwa na lengo la kupotosha umma kuhusu akaunti ya
Tegeta ESCROW ikiwemo kutoa kauli ambazo zingeweza
104
kusababisha Nchi kuingia kwenye mgogoro wa kidiplomasia na
nchi ya Uingereza.
Kamati inapendekeza kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini
(Madini) achukuliwe hatua kali za kinidhamu ikiwemo kutenguliwa
uteuzi wake. Kamati pia inapendekeza kuwa Naibu Waziri huyu
afikishwe mbele ya Kamati ya Bunge ya Maadili ili aadhibiwe kama
Mbunge kwa kusema uwongo Bungeni ili liwe fundisho kwa
wabunge wengine kuhusiana na kauli wanazotoa ndani ya Bunge
lako tukufu.
3.2.9 Mheshimiwa Spika, Kamati imethibitisha kuwa Waziri wa Nishati
na Madini amekuwa, mara kwa mara, akilipotosha Bunge lako
tukufu na Taifa kwa ujumla kuhusiana na Fedha za Akaunti ya
Tegeta ESCROW kwamba ndani ya fedha hizo hakukuwa na fedha
za umma.
Mheshimiwa Spika, hata mtu wa kawaida angeweza kujua
kwamba washirika wa ‘Tegeta Escrow Account’ ni akina nani na
masharti ya kutoka kwa fedha hizo kwenye akaunti ni yapi kwa
mujibu wa Mkataba wa uendeshaji wa akaunti hiyo.
105
Hata hivyo, katika hali ya kushangaza, aidha kwa makusudi ama
kwa sababu anazozijua vizuri zaidi mwenyewe, Waziri wa Nishati
ananukuliwa kwenye kumbukumbu rasmi za Bunge, Kwa nguvu
kubwa na kwa kujiamini, akitetea uchotwaji wa fedha hizo
kinyume na masharti ya Mkataba wa Escrow.
Aidha, Kamati imebaini kuwa Waziri wa Nishati na Madini ndiye
alikuwa dalali mkuu aliyewakutanisha Bwana Harbinder Singh Sethi
na Bwana James Rugemalira, tena katika ofisi ya Umma; na
pengine hii ndiyo iliyokuwa sababu ya upotoshaji huu. Waziri wa
Nishati na Madini alifanya udalali huo akijua dhahiri kuwa Bwana
Sethi hana uhalali wa kisheria kufanya biashara kwa jina la IPTL.
Iwapo Waziri wa Nishati na Madini angetimiza wajibu wake
ipasavyo, Fedha za Tegeta ESCROW zisingelipwa kwa watu
wasiohusika, na Nchi ingeweza kuokoa mabilioni yaliyopotea kama
kodi za VAT, Capital Gain Tax na Ushuru wa Stempu ambazo ni
sawa na takribani shilingi bilioni 30.
106
Mheshimiwa Spika, Kamati inapendekeza kuwa Mamlaka yake
ya uteuzi itengue uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini kutokana
sababu hizo zilizoelezwa.
3.2.10 Mheshimiwa Spika, Kutokana na kukua na hivi sasa
kukomaa kwa vitendo haramu vya wizi wa fedha ama mali za
umma na kukua ama kukomaa kwa vitendo vya rushwa kubwa na
uhujumu uchumi, inapendekezwa kwamba Bunge lako Tukufu
liridhie kuitaka Serikali kuanzisha kitengo maalumu cha
kushughulikia rushwa kubwa (grand corruption) kitakachokuwa na
nguvu ya kuendesha mashtaka kwa uhuru kamili, na kwamba
Bunge lako Tukufu liridhie kuanzishwa kwa Mahakama Maalum ya
kushughulikia Rushwa kubwa itakayoshughulikia kesi za rushwa
zitakazokuwa zikipelekwa kwake na kitengo maalum cha
kushughulikia rushwa kubwa.
3.2.11 Mheshimiwa Spika, Kamati imethibitisha kuwa
Mwanasheria Mkuu wa Serikali alitoa ushauri ulioipotosha Benki
Kuu ya Tanzania kuhusiana na hukumu ya Jaji Utamwa J. Kwa
kutumia madaraka yake vibaya, Mwanasheria Mkuu wa Serikali
aliagiza kodi ya Serikali yenye thamani ya shilingi 21 bilioni isilipwe
107
na hivyo kuikosesha Serikali mapato adhimu. Mwanasheria Mkuu
wa Serikali kwa kujua na kwa makusudi alilipotosha Bunge na
Taifa kwamba mgogoro uliopelekea kufunguliwa kwa Akaunti ya
ESCROW ulikuwa ni mgogoro wa Wanahisa wa IPTL badala ya
mgogoro kati ya TANESCO na IPTL. Kamati inapendekeza kuwa
uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali utenguliwe mara moja na
kisha afikishwe mahakamani kwa matumizi mabaya ya Ofisi
yaliyopelekea Serikali kupoteza mabilioni ya fedha.
3.2.12 Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa Waziri Mkuu
kuhusiana na suala hili, Kamati iliipitia kwa umakini Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 iliyoainisha
Kazi na Mamlaka ya Waziri Mkuu na kubaini kuwa, kwa mujibu wa
Ibara ya 52 (1):
“Waziri Mkuu atakuwa na madaraka juu ya udhibiti,
usimamiaji, utekelezaji wa siku hata siku wa kazi na
shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano.”
Na, Ibara ya 52 (2), inayosema;
108
“Waziri Mkuu atakuwa kiongozi wa shughuli za Serikali
Bungeni.”
Kisha Kamati ikajiuliza maswali kadhaa. Kwa mfano katika kutaka
kubaini ukweli na kujiridhisha Kamati ilijiuliza maswali yafuatayo
kuhusu Waziri Mkuu:
(a) Je, Waziri Mkuu alikuwa anajua sakata la utoaji wa
fedha katika Akaunti ya Tegeta ESCROW?
(b) Je, Waziri Mkuu alitimiza wajibu wake kwa mujibu wa
Ibara ya 52(1)?
(c) Je, Waziri Mkuu wakati akitoa matamshi yake Bungeni
alikuwa akitimiza wajibu wake kwa mujibu wa Ibara ya
52 (2)?
(d) Je, nini maana, uzito na ukweli wa matamshi ya mara
kwa mara ya Waziri Mkuu ndani na nje ya Bunge
kuhusiana na suala hili?
(e) Je, Waziri Mkuu alitoa maamuzi au maelekezo yoyote
ya kuzuia jambo hili lisifanyike?
109
Mheshimiwa Spika, Baada ya kupitia vielelezo vilivyomo kwenye
ripoti ya CAG, Kamati imejiridhisha pasipo mashaka kuwa, Waziri
Mkuu, alikuwa ana taarifa zote kuhusiana na mchakato mzima wa
kuchotwa fedha kutoka katika akaunti ya ESCROW.
Ushahidi ulioletwa na ofisi ya CAG kwenye Kamati unaonyesha
kuwa Waziri Mkuu alikuwa akipata taarifa za jambo hili. Na Kamati
imesikitishwa kuona kuwa Waziri Mkuu hakuchukua hatua zozote
kuzuia muamala huu usifanyike.
Mheshimiwa Spika, Kamati, kwa kuzingatia kielelezo namba 22,
inathibitisha bila shaka kwamba, Waziri Mkuu alikuwa analijua
jambo hili vizuri na kwamba aliridhia muamala huu ufanyike. Ndiyo
maana katika maelezo yake ya Bungeni mara kadhaa Waziri Mkuu
alithibitisha kuwa fedha za Escrow hazikuwa fedha za Umma.
Mheshimiwa Spika, Mwalimu Julius Nyerere katika kitabu chake
cha Uongozi Wetu na Hatma ya Tanzania aliandika:
“…kubadili Waziri Mkuu sio jambo la ajabu. Ndugu
Rashid Mfaume Kawawa alikuwa Waziri Mkuu wangu
110
kwa muda mrefu. Hakuwa amefanya kosa lolote; lakini
nilitaka kumbadili na kuteua Waziri Mkuu mwingine.
Nilimwita, nikamwambia hivyo. Tukakaa pamoja mimi
na yeye, tukashauriana na kukubaliana nani anafaa
kushika nafasi yake. Nikamteua Hayati Edward Moringe
Sokoine. Najua kuwa watu wa aina ya Rashidi Kawawa
ni adimu sana Duniani, hawazaliwi kila siku; hata hivyo
ni jambo la kushangaza kidogo kwamba viongozi wetu
wa Mageuzi, hata bado hatujafa, wanaona kuwa ni
kosa kuwakumbusha kuwa vyeo walivyonavyo ni
dhamana. Wanadhani kuwa Uwaziri ni Usultani;
ukishakuwa Sultani utakufa sultani! Nadhani
wanakosea. Nchi hii imewahi kung’oa Masultani wa kila
aina. Tukianza kuvumilia Masultani wa kuchaguliwa,
tutapanda mbegu ya Masultani wa kuzaliwa. Narudia;
kumbadili Waziri Mkuu sio jambo la ajabu. Anaweza
kujiuzulu, anaweza kufukuzwa Nchi isitikisike. Lakini
huwezi kumtimua Rais wa Nchi bila kuitikisa Nchi
yenyewe. Ni vizuri jambo hili likatamkwa waziwazi na
likaeleweka sawasawa. Maana watu wengine
wananong’ona nong’ona kuwajibika kwa Rais kana
111
kwamba ni jambo la mchezo mchezo tu. Kulazimika
kumchukulia hatua Rais wa nchi ni mkasa na balaa kwa
Nchi yeyote ile.”
Mwisho wa kunukuu.
Mheshimiwa Spika, ni dhahiri kwamba viongozi wenye mamlaka
makubwa wanapaswa kila wakati kukumbuka kauli ya muasisi wa
Mapinduzi ya Zanzibar na Muasisi wa Muungano, Sheikh Thabit
Kombo, ambaye alikuwa akipenda kusema ‘weka akiba ya
maneno’.
Ni wazi kwamba maneno ya Waziri Mkuu hapa Bungeni
yaliuaminisha umma kuwa fedha zile siyo fedha za umma kiasi
kwamba gazeti la Serikali la Daily News la tarehe 1 mwezi Mei,
2014, likachapisha habari yenye kichwa kikubwa cha habari ‘IPTL
clean Deal – Pinda’. Na ofisi ya Waziri Mkuu haikukanusha.
Mheshimiwa Spika, ni jambo la kushangaza kuona kwamba,
jambo kubwa na zito kama hili lingeweza kufanyika bila ya
mamlaka za juu, hususan Mhe. Waziri Mkuu kufahamu.
112
Mheshimiwa Spika, kwa uzito na unyeti wa jambo hili, kwa
vyovyote vile, Waziri Mkuu anapaswa kuwajibika kwa kauli zake na
kwa kutokutekeleza wajibu wake wa kikatiba ipasavyo, ili
kurejesha imani ya wananchi kwa serikali yao na viongozi wao wa
kisiasa.
3.0 HITIMISHO
Mhesimiwa Spika, napenda kukushukuru sana kwa kuiamini
Kamati yetu kwa kuikabidhi jukumu hili nyeti. Nakuhakikishia
kwamba kazi hii imetekelezwa kwa haki iliyojengwa katika msingi
wa Taarifa ya Ukaguzi Maalum wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali, na vyanzo vingine muhimu
vikijumuisha maelezo ya Ofisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).
Mheshimiwa Spika, Kamati inatoa shukrani za dhati kwa vyombo
vya habari kwa kuwapasha habari Watanzania kuhusiana na suala
hili. Kwa namna ya pekee kabisa Kamati inalipongeza gazeti la
The Citizen kwa msimamo wake thabiti bila kujali vitisho.
113
Mheshimiwa Spika, Kamati yetu inayo imani na Bunge Lako
Tukufu kwamba litaitumia Taarifa hii ipasavyo katika kutekeleza
Wajibu wake wa kuisimamia na kuishauri Serikali itekeleze wajibu
wake katika misingi ya haki, uadilifu, uzalendo, usawa, uwazi na
uwajibikaji. Tunawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge wote
kwani katika kipindi chote cha kuandika Taarifa hii mlitutia moyo
kwa kuonesha dhahiri kwamba mnaihitaji Taarifa yetu ijadiliwe
Bungeni.
Mheshimiwa Spika, naomba pia kuishukuru Ofisi ya Spika kwa
maelekezo thabiti ya namna ya kutekeleza jukumu hili.
Naomba pia kumshukuru Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas D.
Kashillilah na Wajumbe wa Sekretarieti yake kwa ushauri makini
katika kipindi chote ambacho Kamati ilikuwa ikitekeleza jukumu
hili. Kipekee nawashukuru pia Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali, Ndg. Francis Mwakapalila, Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Dkt. Edward
Hoseah na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini, Bw.
Rished Bade kwa ushirikiano walioipatia Kamati.
114
Mwisho, nawashukuru Watumishi wote wa Bunge na vyombo
vingine vya kiusalama vilivyohusika katika kuisaidia Kamati
kutekeleza jukumu lake.
Mheshimiwa Spika, naomba Bunge lako tukufu lipokee Taarifa
hii, lijadili na kupitisha mapendekezo yote tuliyoyatoa kuwasilisha.
Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.
Zitto Zuberi Kabwe, Mb.
MWENYEKITI
KAMATI YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI (PAC)
26 NOVEMBA, 2014
0 comments:
Post a Comment