SAKATA LA ESCROW: PINDA, MUHONGO WAHUSISHWA

By
Advertisement


Waziri Mkuu Mizengo Pinda aandamwa bungeni leo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda aandamwa bungeni leo.
Sakata la wizi wa bilioni 306 fedha zilizokuwemo katika akaunti ya Escrow limefikia patamu leo  kufuatia Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanika wahusika wate pamoja na kiwango cha fedha walichochukua. Ripoti hiyo iliyosomwa Bungeni leo na Mwenyekiti wa PAC Zitto kabwe imewabainisha  watuhumiwa hao pamoja na kushauri hatua zitakazochukuliwa.
Kwa mujibu  wa uchambuzi wa taarifa  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, imebainika kuwa chanzo cha mgogoro kati ya TANESCO na IPTL ambacho ndio kilisababisha kufunguliwa kwa Akaunti ya Tegeta ESCROW ambayo ilikuwa na kiasi cha shilingi Bilioni 306 fedha za umma.
Kwa upande wa waliopata mgawo wa fedha zinazodaiwa kugawiwa kama njugu huku wengine wakibeba kwenye mifuko katika Benki ya Mkombozi  wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi, mabox, magunia na lumbesa. Hii ni  Kutokana na muamala uliofanyika tarehe 6 Februari, 2014 katika Benki ya Mkombozi  ambapo kiasi cha shilingi bilioni 3.3 na muamala wa Benki ya Stanbic wa tarehe 23 Januari 2014 ambapo fedha taslimu (cash) kiasi cha shilingi bilioni 73.5 zilitolewa na kugawanywa kwa watu mbalimbali kinyume cha  Sheria ya Benki Kuu na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006.
Waliopata mgawo wa fedha za iptl  ni hawa  wafuatao:  Andrew Chenge (Mb), ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, shilingi bilioni 1.6; Mhe. Anna Tibaijuka (Mb) na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi shilingi bilioni 1.6; Mhe. William Ngeleja (Mb)  ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini shilingi milioni 40.4 , Ndg. Daniel N. Yona ambaye alikuwa pia Waziri wa Nishati na Madini shilingi milioni 40.4,  Ndg. Paul  Kimiti ambaye ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Sumbawanga  shilingi milioni 40.4 , Dr. Enos S. Bukuku ambaye alikuwa Mjumbe wa Bodi ya TANESCO aliingiziwa shilingi milioni 161.7
Majaji wanaohusika katika tukio hilo ni  Prof. Eudes Ruhangisa, aliingiziwa milioni 404.25 na Mhe. J.A.K Mujulizia  liingiziwa  shilingi  milioni 40.4.
Nao  Watumishi wa umma waligawana fedha hizo ni  Ndg. Philip Saliboko ambaye alikuwa mtumishi wa RITA aliingiziwa shilingi milioni 40.4, Ndg. Emmanuel Daniel Ole Naiko ambaye alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) aliingiziwa shilingi milioni 40.4 na Ndg. Lucy L. Appollo ambaye ni Mtumishi wa TRA aliingiziwa shilingi milioni 80.8.
upande wa viongozi wa dini  waliochukua mgawo huo  wa  fedha katika Benki ya Mkombozi ni Askofu Methodius Kilaini shilingi 80.9, Askofu Eusebius Nzigirwa shilingi milioni 40.4 na Mchungaji Alphonce Twimann Ye Simon shilingi milioni 40.4.
Wanaotajwa kuwajibishwa kutokana na mgawo wa fedha hizo ni Harbinder Singh Sethi anayejitambulisha   kama Mmiliki wa IPTL ambapo Ripoti imeshauri arudishe fedha na kufilisiwa mali zake zote .
Wengine ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa kutowajibika na kuisababishia serikali hasara ya mabilioni ya fedha za umma, Waziri wa Nishati na Madini Prof Muhongo anayedaiwa kuwa  ndiye alikuwa dalali mkuu aliyewakutanisha Bwana Harbinder Singh Sethi na Bwana James Rugemalira  katika ofisi ya Umma.
Katibu Mkuu Ndg. Servacius Likwelile,Watendaji wa wizara ya Nishati na Madini,Watendaji wa Benki kuu,pamoja na Wizara ya fedha.
Kwa upande mwingine kamati imependekeza Waziri wa Nishati na Madini achukuliwe hatua za kinidhamu ikiwemo kutenguliwa cheo chake pamoja na  Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Jaji  Werena   kuvuliwa cheo chake.Viongozi  wengine  wanaohusika katika kugawana fedha hizo  pia nao kamati imeshauri wavuliwe nyadhifa zao na kufilisiwa  mali zao zote.

0 comments:

Post a Comment

Pages