SAKATA LA ESCROW: MUHONGO AJITOA MUHANGA KUOKOA JAHAZI

By
Advertisement

SAKATA LA ESCROW: MUHONGO AJITOA MUHANGA KUOKOA JAHAZI

Tarehe November 27, 2014
Prof.Muhongo ajibu hoja za PAC Bungeni leo.
Prof.Muhongo ajibu hoja za PAC Bungeni leo.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospete Muhongo  ameikingia kifua serikali kuhusiana na wizi wa zaidi ya Bilioni 306 katika akaunti ya Tegeta Escrow iliyofunguliwa kutokana na kuwepo mgogoro baina ya kampuni ya kufua umeme ya IPTL na Shirika la Umeme la Tanzania (Tanesco).
Waziri Muhongo ameanza kwa kutoa pongezi juu ya mjadala wa Escrow ambapo  amesisitiza kuwa  mengi yamesemwa na ni wakati wa kuanza mjadala kujua ukweli  wa sakata hilo.
Kuhusu Escrow Muhongo amesema  Account ya Escrow ilipaswa kuwa na bilioni 306 zilizowekwa na TANESCO fedha ambazo  Waziri huyo amesema sio za umma. Taarifa hiyo inakinzana na ripoti ya  PAC iliyothibitisha  kuwa ni  fedha za  umma  na  mchakato wa kutoa pesa Escrow umegubikwa na mchezo mchafu ikihusisha  kutakatishwa  fedha na benki mbili nchi.
Madai kwamba IPTL inaidai IPTL 321 Bilioni, amesema kwamba  bodi ya TANESCO imekana kuyatambua madai haya na vitabu vya TANESCO vinavyokaguliwa na CAG hakionyeshi madai haya.
Amesisitiza  kwamba TANESCO kwa kushirikiana na IPTL ilifanya uhakiki ili kujua madai halali ya IPTL kabla ya kufanya malipo. Deni la TANESCO kama capacity charge lilikuwa $370milioni ambazo ni pungufu ya $90 milioni ya madai ya IPTL. Yalifanyika hoteli ya Kunduchi na majina ya waliokuwepo anawataja.
” Hizi takwimu zinaonyesha hakuna fedha yetu pale tunayodai bali tunadaiwa na IPTL. Hamna fedha ya umma popote bali tunadaiwa na makampuni ya uzalishaji umeme(anataja makampuni na madeni wanayodai “. A lisema Muhongo
Kuhusu mjadala uliokuweo kama fedha za Escrow  ni  mali ya umma au ni  TANESCO Prof. Muhongo amesema kwamba Hakuna fedha ya umma katika akaunti ya  Escrow fedha zote ni mali ya kampuni ya IPTL.
Katika hali isiyokuwa  ya kawaida  utetezi huo  wa  Waziri wa Nishati na Madini hadi Bunge linamaliza kikao wabunge hawakuweza kugagiwa ripoti hiyo licha ya kuiomba kwa  nguvu  huku  wakipiga kelele kabla ya Waziri huyo kukamilisha ripoti yake

0 comments:

Post a Comment

Pages