Mshirikishe mwenzako
Palikuwa na kituko cha mwaka kilichotukia katika kituo cha polisi bulenga, wakati mwanamke mmoja alipokuwa akiomba poo na huku akimtaka mumewe amsamehe na kumwachilia aende zake kutokana na mumewe kuwa na hamu ya kufanya ngono isiyo na koma.
Ruth Nakyeyune,alikuwa akilia na hanyamazishwi kwa madhila apatayo kutoka kwa mumewe huku akimuomba mumewe mwenye asili ya Nigeria bwana Sultan Ali Baba kwa pamoja ni wakaazi wa Nakuwade Bulenga,karibu na barabara ya Mityana, mwanamke anaomba poo na mwenyekusema basi yatosha na kutaka waachane kila mmoja ashike hamsini zake.
Bi Nakyeyune amesema pia kwamba amekuwa si mvumilivu kwa muda mrefu na asiyejali chochote na hataki kusikia jibu la hapana linapokuja suala la ngono.bibi huyo amesema kwamba pindi anapokuwa hajisikii vizuri na hawezi kufanya ngono,Sultan haelewi juu ya suala hilo,na humnunia.sultani alipoulizwa juu ya kununa kwake alisema kwamba hamuamini mkewe na sababu anazompa hivyo anadai anamdanganya na kumnyima haki yake bure na kusema kuwa huwa hamridhishi,mara zote mwanamke huyoa amekuwa akitafuta sababu na mara moja ameshawahi kumtishia atajiua.
Sultan alimtaka mwanamke huyo amshukuru Muumba wake kwakuwa yeye ni mume mwema asiyekunywa pombe kama wengine wafanyavyo,na kumshangaa mkewe anashindwaje kumridhisha kirahisi?
Na kumuuliza mkewe bi Nyakyeyune kwanini aliwaacha wazazi na jamaa zake kama hakuwa tayari kumridhisha kingono,na kama shangazi zake ndo walomfunda na kumpeleka kwake kwa shughuli za ndoa, vipi hayuko tayari?
Inaelezwa kuwa wake wa awali wa bwana Sultan walimkimbia mwanamume huyo kwa tabia hiyo hiyo ya kutoridhika kingono,lakini baadaye Sultani alimuomba mkewe kusalia nyumbani kwa ajili ya watoto wao ili wawalee lakini mke alikataa ushawishi huo.
0 comments:
Post a Comment