Arsene Wenger:''Vibali vya kazi vifutwe''
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger
ametaka kanuni za kutoa kibali cha kufanya kazi kwa ajili ya wachezaji ambao
hawamo kwenye umoja wa ulaya zifutwe.
Wenger anaejaribu kumsajili Gabriel
Paulista kutoka Villarreal ambae anahitaji kibali cha uidhinisho toka nchini
kwake sababu hajawahi kulitumikia taifa lake.
Bosi huyo amekosoa mpango wa
mapendekezo ya kupunguza idadi ya wachezajitoka mashirikisho yasiyo ya Umoja wa
Ulaya wenye pasipoti katika michezo ya ligi ya England msimu ujao.
Akasema "Kusema ukweli inapaswa
funguliwa kabisa, na kila mtu anaweza kungia"
Kwasasa kibali cha kufanyia kazi kwa
nchi zisizo umoja wa Ulaya kunahitajika kuwa katika nafasi 70 za juu katika
ubora wa viwango vya Fifa na awe amecheza kwa asilimia 75 katika timu ya taifa
ndani ya miaka miwili.
"Ili kumsajili Paulista
tungeweza kuwashawishi maofisa wa kwao kuwa ni beki wa kipekee mwenye
kipaji."
Chama cha Soka cha Englan kinataka
kupunguza idadi ya wachezaji wasiokua wenyeji wa jumuiya ya ulaya kufikia
asilimia 50 kwenye ligi.
Lakini Wenger anadhani kuondoa
kanuni itakuwa bora kwa ajili vijana wachezaji Kiingereza.
"kufunga mipaka ya nchi na
kuruhusu kucheza wachezaji wa Kiingereza tu Nini kitatokea? Ni kuua mvuto wa
ligi dunia kote.
Wenger alisema Arsenal walitaka
kumsajili winga wa kimataifa wa Ajentina Angel Di Maria lakini kibali cha kazi
kikaleta shida.
Wenger aliongeza "Tulimtambua
Di Maria alipokuwa 17.Tulimuona akiwa katika mashindano ya kimataifa na
tulitaka aje hapa.
"Lakini alikwenda Ureno, na
kutoka Ureno alikwenda Hispania. Kwa nini? Kwa sababu hakuweza kupata kibali
cha kufanya kazi England.
0 comments:
Post a Comment