STEPS ISHU SIYO KUUZA BUKUBUKU, TUTAWAMALIZAJE MAHARAMIA?

By
Advertisement

STEPS ISHU SIYO KUUZA BUKUBUKU, TUTAWAMALIZAJE MAHARAMIA?

KWENU wasambazaji wakongwe wa sinema za Kibongo, Kampuni ya Steps Entertainment. Bila shaka mko poa na mnaendelea na shughuli zenu za kusambaza kazi za wasanii wetu wa Bongo Movies.

Binafsi mimi ni mzima wa afya, naendelea vizuri na majukumu yangu ya kila siku. Kwa heshima ya pekee naomba niutambue uwepo wa Mkurugenzi wa Steps, Diresh Solanki, umechangia kwa kiasi fulani kukuza sanaa nchini.
Dhumuni la barua hii ni kutaka kukueleza juu ya uamuzi wenu wa kuuza CD za wasanii kwa sh. 1000 kwa kigezo cha kumaliza suala la maharamia ambao walikuwa wakiuza kwa bei hiyo.

Niliposikia wazo hilo nilipata…

Niliposikia wazo hilo nilipata shida kidogo. Nilitafakari kwa mapana na kuona mlichokifanya hakiwezi kuwa suluhu ya tatizo moja kwa moja.
Hakiwezi kuwa kwa sababu, natazama urahisi wa kupata CD tupu (empty) kwa bei ya jumla. Natazama urahisi wa kuzidurufu hizo CD, jibu langu ni kwamba kuna uwezekano na wao wakauza CD moja kwa shilingi 500 na wasipate hasara.
Suala la kujiuliza hapo ni kwamba  na nyinyi mtapunguza bei muuze 500 ili kwenda nao sambamba? Hapo bado yatakuwa ni yaleyale, hakutakuwa na jipya na madhara yake yatakuwa ni makubwa zaidi.
Hivi kabla ya kufikia uamuzi huo, mlifikiri kwa makini na kuangalia faida na hasara ya suala hili? Mliwashirikisha wasanii na makampuni yote ya usambazaji nchini? Au mliangalia soko lenu pekee ambapo nyinyi tayari mna mizizi mingi katika nchi mbalimbali?
Hapa najua jibu lipo wazi, hamkuwashirikisha na ndiyo maana baadhi yao wamepinga uamuzi wenu. Nyinyi  mnaweza kuhimili bei hiyo kwa sababu mna msingi mkubwa na mmeanza siku nyingi, vipi kuhusu wasambazaji wengine?
Mlipaswa kujiuliza kwanza, hakuna njia nyingine ya kukomesha suala hili? Hakuna mhuri usioigika kirahisi mnaoweza kuweka katika kazi zenu na kutofautisha na zile feki? Nchi za wenzetu wanafanyaje katika kukomesha maharamia?
Uharamia upo duniani kote, lakini unapunguzwa na suala la kuweka sheria kali, kuweka ulinzi mkali katika kazi orijino na kampeni mbalimbali za kukamata maharamia na kuwapa adhabu kali.
Kupunguza bei  ni kujikaanga wenyewe na kuwaumiza zaidi wale ambao mtaji wao ni mdogo. Kwa muandaaji mdogo, gharama za kuwalipa wasanii, vifaa na uzalishaji wa sinema, ukimwambia aiuze sh 1000 ni sawa na kumwambia aache hiyo biashara.
Ataacha maana haiwezi kumlipa. Atumie fedha nyingi katika kuandaa halafu auze kwa bei ndogo namna hiyo haiwezi kuwa sawa. Mnapaswa kulitazama hili kwa jicho la tatu kama kweli mna nia ya dhati ya kuendeleza sanaa nchini.
Nasema inawezekana, itashindikana kama  mlikuwa na agenda nyingine nyuma ya kapeti.
Kwa leo inatosha, ni matumani yangu mtakuwa mmenielewa. Nitarudia siku nyingine kama mtakuwa bado hamjanielewa.
Wasalaam!

0 comments:

Post a Comment

Pages