WANYAMA WAKALI, MIGOGORO YA ARDHI NI TATIZO

By
Advertisement

WANYAMA WAKALI, MIGOGORO YA ARDHI NI TATIZO


Wengi wanaifahamu Mikumi kama hifadhi ya taifa ya wanyama iliyopo mkoani Morogoro. Lakini pia Mikumi ni jimbo la uchaguzi lililopo ndani ya Wilaya ya Kilosa, likiwa na ukubwa wa karibu kilometa 7,353.
Mheshimiwa Abdulsalaam Seleman Amer (kushoto) akizungumza jambo.
Wiki iliyopita, kama kawaida Gazeti la Uwazi lilichanja mbuga mpaka kwenye jimbo hilo linaloongozwa na mheshimiwa Abdulsalaam Seleman Amer kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ndiye mmiliki wa kampuni ya SAS na kuzungumza na wananchi…
Wengi wanaifahamu Mikumi kama hifadhi ya taifa ya wanyama iliyopo mkoani Morogoro. Lakini pia Mikumi ni jimbo la uchaguzi lililopo ndani ya Wilaya ya Kilosa, likiwa na ukubwa wa karibu kilometa 7,353.
Mheshimiwa Abdulsalaam Seleman Amer (kushoto) akizungumza jambo.
Wiki iliyopita, kama kawaida Gazeti la Uwazi lilichanja mbuga mpaka kwenye jimbo hilo linaloongozwa na mheshimiwa Abdulsalaam Seleman Amer kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ndiye mmiliki wa kampuni ya SAS na kuzungumza na wananchi mbalimbali ambao walieleza matatizo yanayowakabili jimboni humo.
MATATIZO YA WANANCHI NA MAJIBU YA MBUNGE
Naftali Kigoda, mkazi wa Kijiji cha Lumango, alikuwa na haya ya kusema: “Sisi wananchi tunaoishi pembeni ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi tunanyanyasika sana kwa kweli.
“Ukilima kashamba kako, wanyama wanatoka kwenye hifadhi na kuja kula na kuharibu kila kitu. Pia maisha yetu yapo hatarini kwa sababu simba wakishikwa na njaa, wanakuja huku vijijini na kusababisha madhara makubwa kwa binadamu na mifugo yetu, tunaomba mheshimiwa mbunge atusaidie.
Prudencia Safari, mkazi wa Kijiji cha Msindazi, naye alieleza tatizo hilohilo la wanyama wakali na waharibifu kuvamia katika makazi ya watu na kusababisha madhara makubwa, ikiwemo vifo vya wanakijiji wanaoliwa na wanyama wakali kama simba.
Wilfred Akyoo, mfanyabiashara katika Mji Mdogo wa Mikumi, yeye alikuwa na haya ya kusema: “Tatizo kubwa Mikumi ni uzembe wa viongozi wetu. Hawawajibiki ipasavyo kutimiza ahadi wanazotoa wala kutuondolea matatizo yanayotukabili. Maji ni shida, dawa hospitali ndiyo hakuna kabisa lakini wao wapo tu. Halafu viongozi wetu hawana utaratibu wa kuitisha mikutano na kutusomea mapato na matumizi.”
Mheshimiwa Abdulsalaam Seleman Amerakiwa akiwasikiliza wananchi jimboni Mikumi.
“Michango imezidi shuleni, yaani kila mara watoto wanasumbuliwa kisa michango. Tunaomba mheshimiwa mbunge atusaidie. Kingine kuna rushwa sana polisi, yaani mtu ukikamatwa hata kama huna kosa hutoki bila kutoa rushwa, hii siyo sawa kabisa,” Emanuel Chedieli aliliambia Uwazi.
Tatizo lingine ambalo Uwazi lililishuhudia, ni mabinti wengi wadogo kukatisha masomo na kujihusisha na biashara haramu ya kuuza miili yao, kwa madereva wa malori yanayotumia barabara kuu ya Iringa- Morogoro ambapo vitendo hivyo vinafanyika waziwazi bila kificho.
“Ukosefu wa ajira ni tatizo huku kwetu, vijana wengi tunashinda tu vijiweni kama hivi, hakuna kazi wala huwezi kupata mtaji wa kufanya biashara ya maana. Tunaomba mbunge wetu atusaidie,” Malick Mgunda aliliambia Uwazi.
“Mimi namwambia mheshimiwa mbunge asikie kilio chetu sisi wananchi wa Msolwa, tunahangaika sana na hili tatizo la ardhi ambalo yeye anahusika kwa kupewa ardhi yetu ya kilimo kufanyia kazi za makampuni yake. Tunaomba asikie kilio chetu atuachie ardhi tuendelee na kilimo mbona eneo ni kubwa sana?” mwananchi ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini aliliambia Uwazi.
MAELEZO YA MBUNGE
Uwazi lilifanikiwa kuzungumza na mheshimiwa mbunge Abdulsalaam Seleman Amer ambaye alikiri kuzijua kero mbalimbali za wananchi wa jimbo lake na kueleza jinsi anavyohangaika kuzipatia ufumbuzi.
Kuhusu suala la wananchi na mali zao kudhuriwa na wanyama, mbunge huyo alisema amekuwa akihangaika kwa kipindi kirefu kwa kushirikiana na mamlaka zinazohusika kuangalia namna ya kujenga uzio wa kuzuia wanyama kuingia kwenye makazi ya watu wanaoishi kwenye vijiji vinavyopakana na hifadhi.
Kuhusu michango ya watoto shuleni, mbunge huyo amewataka wananchi kutokuwa wazito katika kuchangia maendeleo yao au ya watoto wao kwa sababu serikali peke yake haiwezi kufanya kila kitu kwa wakati kutokana na kuchelewa kwa bajeti kuu.
Suala la ardhi anayomiliki kwenye Kijiji cha Msolwa, mbunge huyo alisema eneo hilo analimiliki kisheria na kwamba hakuna mtu yeyote aliyeonewa, akaongeza kuwa hata hivyo majadiliano yanaendelea kati yake na wananchi na anaamini watafikia muafaka mzuri.

0 comments:

Post a Comment

Pages