Hekaheka ya leo Desemba 01 inahusu yule Msichana Maua aliyepotea kupatikana.
Kama hukusikiliza Hekaheka ya leo
Jumatatu ya Desemba 01 kupitia Clouds Fm kwenye Leo Tena, ni mwendelezo
wa Hekaheka ya Novemba 18 iliyokuwa inahusu msichana Maua mwenye umri
wa miaka 17 aliyepotea siku ya Jumamosi Novemba 15.
Maua ambae alipotea wiki mbili
zilizopita kama amerudi na kusema kuwa alikuwa Mbagala kwa Mpenzi wake
Amiry ambaye alikutana naye njiani siku ambayo aliondoka kwao na kwenda
kwa rafiki yake wa kiume, ambapo baada ya kuchelewa kurudi akahofia
kwamba mama yake huenda angemkalipia, akaamua kwenda kwa Mchungaji
ambaye alimwambia arudi kesho yake ili afanyie maombi.
Kwa mujibu wa maelezo ya Maua anasema
akiwa njiani alikutana na Amiry ambaye ni mlinzi wa Bar, na kumbembeleza
ili waende kwake ambako amekuwa akiishi huko tangu usiku huo mpaka siku
anayorudi nyumbani kwao.
Mama wa Maua amesema siku ambapo
msichana huyo alikuwa anarudi alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha
kwa jina la Amiry na kumpa taarifa kwamba Maua atarudi siku hiyo.
Maua anasema aliongozana na Amiry lakini
walipokaribia kwao aliamua kukimbia baada ya kikundi cha vijana kuanza
kumzonga huku wakitishia kumkatama na baada ya hapo Amiry amekuwa
akipigiwa simu na mama wa Maua ili aje waongee lakini imeonekana amekuwa
akisita kutokana na hali aliyokutana nayo siku ya kwa mwanaume huyo
amekuwa akipigiwa Simu na Mama Maua ili waongee.
Taarifa ambazo zilifika Polisi usiku wa
siku hiyo ni kwamba mama Maua alikutwa akihamisha vitu vyake bila kuaga
hata majirani wakati bado kesi ya mtoto wake ikiwa haijaisha Polisi,
ambapo Polisi waliikamata gari iliyopakia vitu hivyo huku sababu ya mama
Maua kuhama bado haijafahamika.
0 comments:
Post a Comment