MALI ZA VIGOGO ESCROW USIPIME
Stori: Mwandishi Wetu
HUKU moto wa upotevu wa fedha za umma katika akaunti ya Tegeta Escrow ukiwa bado unawaka kufuatia mawaziri wawili, mwanasheria mkuu wa serikali, katibu mkuu mmoja na Bodi ya Tanesco kutakiwa kuwajibishwa, mali zinazomilikiwa na vigogo waliochotewa fedha hizo usipime.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa wanaotajwa kunufaika na fedha
hizo, unaonyesha kuwa, pamoja na mambo mengine, wanamiliki majumba
makubwa ya kifahari, yakiwemo maghorofa katika maeneo mbalimbali ya
mikoa, ikiwemo Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya na Morogoro.HUKU moto wa upotevu wa fedha za umma katika akaunti ya Tegeta Escrow ukiwa bado unawaka kufuatia mawaziri wawili, mwanasheria mkuu wa serikali, katibu mkuu mmoja na Bodi ya Tanesco kutakiwa kuwajibishwa, mali zinazomilikiwa na vigogo waliochotewa fedha hizo usipime.
Mmoja wa wanaotajwa (jina linahifadhiwa kwa sasa) ana jumba kubwa la ghorofa mbili sehemu za Mbezi Beach, Dar, ambalo licha ya kuwa ya thamani kubwa, pia ukubwa wa eneo analomiliki, umemfanya pia kujenga bwawa kubwa la kuogelea.
“Aina ya maisha anayoishi huwezi kusema kama ni Mtanzania, kwa sababu haonyeshi kama anajua uwepo wa shida, kwa sababu watoto wake wote wanasoma nje ya nchi na zipo likizo ambazo hawarudi kwa vile wanasafiri nchi tofauti na wanazosoma kwa ajili ya matembezi tu.
“Acha hii nyumba, ana ghorofa pale Kariakoo
lote limepangishwa na magari anayoendesha huyu bwana ni hatari.
Nafikiri gari la thamani ndogo kabisa ni BMW analoendesha mkewe. Kuna
watu wana fedha hadi wanaudhi aiseee,” alisema mkazi mmoja wa Mbezi
Beach, anayedai kuishi jirani na mfanyabiashara huyo aliyenufaika na
fedha za Escrow.
Kigogo mwingine mwenye asili ya Mwanza, anadaiwa kununua jengo lenye
ghorofa nne lililopo katikati ya Jiji la Mwanza na limeshaanza kufanyiwa
marekebisho, kwani ana lengo la kuifanya hoteli.Wakati ikiwa bado haijafahamika kama watu hao walionufaika na fedha hizo mali zao watafilisiwa au la, habari zinasema baadhi ya waliochotewa, wamekuwa na maisha ya kufuru, kutokana na matumizi ya kutisha ya fedha wanayofanya, huku wakinunua vitu mbalimbali vya thamani.
Hata hivyo, wakati watu hao wachache wakiwa wamegawana kiasi cha shilingi bilioni 306, idadi kubwa ya Watanzania wanaishi maisha ya umaskini mkubwa, kiasi cha kula mlo mmoja kwa siku, huku wakikosa huduma muhimu kama maji safi na salama ya kunywa, huduma bora za afya na elimu.
Mamia ya vituo vya afya vinavyomilikiwa na
serikali huko vijijini havina dawa, hasa kipindi hiki ambacho serikali
inadaiwa kiasi cha shilingi bilioni 90 na Bohari Kuu ya Madawa (MSD).
Kutokana na kukosekana kwa dawa, Watanzania wengi hufariki dunia kwani
zahanati nyingi zina dawa ndogondogo kama panado za kutuliza maumivu tu.
“Wakati wengine wanakufa kwa kukosa dawa, shule zikiwa hazina vifaa
vya kufundishia na uhakika wa kula ukiwa mdogo, Watanzania wengine
wanaishi kifalme, wanapata kila kitu wanachotaka, wanakwenda popote
wanapotaka, wanatibiwa hospitali wanazotaka. Bora maisha wanayoishi
yangekuwa kwa sababu ya fedha halali, lakini hizi za wizi ni hatari
sana,” alisema mwanaharakati mmoja, aliyejitaja kwa jina moja la Nando.Wiki iliyopita, Bunge lilitoa maazimio nane yanayotakiwa kutekelezwa na serikali, ikiwa ni pamoja na kupendekeza mamlaka ya uteuzi kuwavua nyadhifa zao Mawaziri Sospeter Muhongo na Anna Tibaijuka, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, Eliakim Maswi pamoja na kuvunjwa kwa Bodi ya Shirika la Ugavi wa Umeme (Tanesco).
Bunge hilo pia, lilimjadili Singasinga Harbinder Sigh Seth (pichani) ambaye inadaiwa ndiye kinara wa dili hilo.
0 comments:
Post a Comment