ARSENAL FC YATEMBELEA PSPF KWA LENGO LA KUSAKA FURSA ZA MAHUSIANO YA KIBIASHARA
Mkurugenzi
Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa
Mahusiano ya kimaendeleo wa Klabu ya Arsenal Bw. Sam Stone (Kulia) ,
kushoto ni Bw. Daniel Willey, Meneja wa Mahusiano ya Kimaendeleo ya
Arsenal.
Mkurgenzu Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu (kushoto)…
Mkurugenzi
wa Mahusiano ya kimaendeleo wa Klabu ya Arsenal Bw. Sam Stone (Kulia)
akimkabidhi jezi ya timu hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa
PSPF Bw. Adam Mayingu. Kushoto ni Bw. Daniel Willey, Meneja wa Mahusiano
ya Kimaendeleo ya Arsenal. Maafisa hao wapo nchini kwa lengo la
kukutana na wadau mbalimbali ili kufungua mahusiano ya kibiashara,
katika mpango huo makocha wa timu hiyo na baadhi ya nyota waliowahi
kuchezea timu hiyo watapata fursa kutembelea Tanzania. Klabu ya Arsenal
ni kati ya klabu maarufu ulimwenguni ambayo inashiriki ligi maarufu
duniani ya Barclays.
Mkurgenzu
Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu (kushoto) akimkabidhi zawadi Afisa
Mtendaji Mkuu wa EAG Group, Bw Imani Kajura ambaye ni mwenyeji wa
maafisa kutoka klabu ya Arsenal ambao wapo nchini kwa ajili ya kukutana
na wadau mbalimbali kwa lengo kufungua mahusiano ya kibiashara.
0 comments:
Post a Comment