WAZIRI AWAOMBA RADHI WANAFUNZI KENYA
Waziri wa Usalama nchini Kenya Joseph Nkaissery amewaomba radhi wanafunzi wa shule ya msingi waliofyatuliwa gesi ya kutoa machozi wakati walipokuwa wakiandamana kupinga unyakuzi wa kipande cha ardhi ambacho kilikuwa uwanja wao wa kuchezea.
Bwana Nkaissery amempa siku moja mnyakuzi
wa ardhi hiyo kuondoa sehemu ya ukuta iliobaki baada ya wanafunzi
kuuangusha na kisha kuondoka katika eneo hilo.
Nkaisery ameongeza kwamba serikali itaweka uzio katika ardhi hiyo na kuiacha kuwa uwanja wa kuchezea wa wanafunzi hao.
Nkaisery ameongeza kwamba serikali itaweka uzio katika ardhi hiyo na kuiacha kuwa uwanja wa kuchezea wa wanafunzi hao.
0 comments:
Post a Comment