#HABARI ASKARI WAWILI WAUAWA KITUO CHA POLISI
Askari Polisi wawili wa kituo cha Polisi Ikwiriri, wilayani Rufiji
mkoani Pwani nchini Tanzania wameuawa kwa kupigwa risasi na watu
wasiofahamika waliovamia kituo hicho.
Akithibitisha kutokea kwa
tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani SACP Ulrich Matei amesema
kuwa tukio hilo limetokea saa Nane za usiku wa kuamkia leo ambapo mbali
ya kusababisha mauaji hayo watu hao pia wamepora silaha mbalimbali
kituoni hapo ikiwemo bunduki SMG 2, Shotgun 1 na SAR 2.
Kamanda Matei amewataja askari waliouawa kuwa ni Edgar Mlinga na Askari
wa kike ambaye amefahamika kwa jina moja la Judith na kusisitiza kuwa
jeshi la polisi linaendelea na msako mkali ili kuwakamata watuhumiwa na
kuwafikisha mbele ya sheria
0 comments:
Post a Comment