Mboni Masimba haogopi macho ya watu
IN SUMMARY
“Mimi ni mwanamke kama wanawake wengine, kwa hiyo sidhani kama ni kitu cha ajabu sana na kama kazi nafanya kama kawaida, kuna watu ambao wapo kama mimi na wanafanya kazi mpaka miezi tisa,” alisema Mboni na kuongeza:
MTANGAZAJI wa kipindi maarufu cha The Mboni Show, Mboni Masimba amesema watu wengi wanamshangaa kwa uamuzi wake wa kubeba ujauzito, lakini anaamini yuko kwenye njia sahihi kwa sasa kwani kitendo hicho kinaweza kumtokea mwanamke yeyote.
“Mimi ni mwanamke kama wanawake wengine, kwa hiyo sidhani kama ni kitu cha ajabu sana na kama kazi nafanya kama kawaida, kuna watu ambao wapo kama mimi na wanafanya kazi mpaka miezi tisa,” alisema Mboni na kuongeza:
“Kwa nini nishindwe kufanya kazi? Kama mnavyoniona nina nguvu tu na ni mrembo pia, naamini msimu wa pili wa kipindi changu kinachoanza kuonekana leo Ijumaa TBC, hautamchosha mtazamaji kwa sababu ya hali yangu,” alisema kwa utani.
Mboni alisema kipindi chake ambacho kimelenga katika kuelimisha, kuhamasisha na kusaidia jamii ya Watanzania, kina mtazamo chanya ambao umeweza kuwasaidia wengi tangu alipoanza kukiandaa miaka miwili iliyopita.
Hata hivyo, alisema kuhama kwake katika televisheni ya awali iliyokuwa ikionyesha kipindi chake EATV, hakutazuia wala kupunguza chochote kwani ana hakimiliki ya The Mboni Show.
0 comments:
Post a Comment