Mimba ya Aunty Ezekiel utata mtupu!
IN SUMMARY
Sababu kubwa inasemwa kuwa, Aunty Ezekeil hajaonana na mumewe faragha kwa muda mrefu sasa kutokana na sababu zilizo nje uwezo wa wawili hao.
Sababu kubwa inasemwa kuwa, Aunty Ezekeil hajaonana na mumewe faragha kwa muda mrefu sasa kutokana na sababu zilizo nje uwezo wa wawili hao.
Mtu wa karibu na mwigizaji huyo, amethibitisha kwamba ni kweli Aunty ana ujauzito wa miezi kadhaa.
“Ni kweli ujauzito wa Aunty ni wa mpenzi wake na si mumewe. Unajua anatoka na Iyobo na wawili hao bado wanaonekana pamoja, hafanyi tena safari za Dubai ambako ndiko mumewe aliko,” kilisema chanzo hicho.
Kwa mujibu wa Aunty alisema ni kweli ana ujauzito lakini hayo ni mambo yake binafsi na hadhani kama yanamwathiri mtu kwani ni uamuzi wake.
“Umri unakwenda nikae kusubiri nini? Kama nina mimba mimi si mwanamke kama walivyo wengine, kwani kubeba mimba ni ajabu?” Alihoji Aunty Ezekeil
0 comments:
Post a Comment