MBUNGE WA JIMBO LA MOROGOGO MJINI MH ABOOD AMWAGA MISAADA KATA YA BIGWA MOROGORO
Mbunge wa
Jimbo la Morogoro Mjini Mh aziz Abood Akijibu Hoja Mbalimbali Kuhusu
kero Zinazowakabili wakazi wa Kata ya Bigwa Katika Ziara yake ya
Kutembelea Kata Mbalimbali za Jimbo la Morogoro Mjini.Mh Abood Aliata
nafasi ya Kuongea na wakazi wa Mitaa wa Mitaa Mbalimbali inayounda Kata
ya Bigwa.Mh Abood alijibu na Kutatua Kero Mbalimbali zinazowakabili
wakazi wa Kata Hiyo.Mbunge Huyo alitoa Majibu Kuhusu Kero ya Umeme,
Maji ,Barabara na Nyinginezo.Pia Mh Abood alitoa Misaada Mbalimbali iliyogarimu zaidi ya Milioni 20 Katika Kata ya Bigwa.
Mbunge wa
Jimbo la Morogoro Mjini Mh aziz Abood akiwa kwenye banda la Mama Lishe
maarufu Kama Mama Ntilie Ili Kujionea na kujua Changamoto
Zinazowakabili wamama hao katika kazi yao Hiyo wakati wa Ziara yake ya
Kutembelea Kata ya Bigwa Jimbo la Morogoro Mjini
Baadhi ya Misaada aliyotoa Mbunge huyo kwa Wakazi wa Kata ya Bigwa.
Mbunge wa
Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akikabidhi vifaa Mbalimbali kwa
Vikundi vya wakina Mama wanaojihusisha na Shuguli za Mama Lishe Katika
Mitaa ya Vituli, Bomela, Korogozo,Mungi, na Mgolole Iliyopo Kata ya
Bigwa.
Mbunge wa
Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akisikiliza Kwa Makini Kero
iliyokuwa Ikiwasilishwa na Mmoja wa wakazi wa Mtaa wa Mgolole kata ya
Bigwa alipotembelea Mtaa huo kusikiliza na Kutatua Kero za Wakazi wa
Mtaa Huo.
Mbunge wa
Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akiongea kwa Msisitizo kuhusu
watendaji kushugulikia Kero la wananchi wa Kata ya Bigwa kwa haraka.
Badhi ya Wakina Mama wanaojishugulisha na kazi ya Mama Lishe wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood
Mbunge wa
Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akiwa Amezungukwa na Vijana wa
Kata ya Bigwa wakimweleza Kuhusu kero ya Ajira Na Michezo Ambapo Mbunge
Huyo alijibu Hoka Hizo kwa Kuwakabidhi Mpira wa Miguu .Kuhusu Ajira Mh
Abood aliwaagiza Vijana Hao Kujiunga kwenye Vikundi vya Kufanya Shuguli
za Maendeleo na yeye atawawezesha kwa Kuwapa Mitaji.
Mbunge wa
Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akiwa Nyumbani kwa Balozi wa CCM
Mtaa wa Misongeni B Kata ya Bigwa Ndugu Omary Iddy aliyemgonjwa
alipofika Kumjulia hali.
Mbunge wa
Jimbo la Morogoro Mjini Mh aziz Abood Akiwa Nyumbani kwa Balozi wa CCM
Mtaa wa Misongeni B Iliyopo Kata ya Bigwa Manispaa ya Morogoro Ndugu
Omary Iddy aliyemgonjwa kwa Muda Mrefu Alipofika Kumpa Pole.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh aziz Abood Aliofika Kuhani Msiba wa Bi Nuru Binti Ally Ngozi wa Kata ya Bigwa.
Reactions: |
0 comments:
Post a Comment