MSANII MAARUFU WA BONGO FLAVOUR "BINTI KIZIWI" ATOA SIRI NZITO AKIWA GEREZAN HONG KONG

By
Advertisement

MSANII MAARUFU WA BONGO FLAVOUR "BINTI KIZIWI" ATOA SIRI NZITO AKIWA GEREZAN HONG KONG

Wengi mtakuwa mnamkumbuka  mwanadada huyu aitwae Sandra Khan. Mrembo huyu alijulikana sana kwa jina maarufu kama binti kiziwi,aliyecheza  muziki wa bongo flavour na msanii Ally Mohammed,maarufu kwa jina la "Z Anto".Katika wimbo huo Sandra alikuwa ame-act kama 'Binti Kiziwi' na ndipo alipojipatia umaarufu.
Katika mihangaiko ya maisha,Sandra alijikuta kuingia katika uuzaji na usafirishaji wa madawa ya kulevya kutoka Tanzania kwenda  Nchi za mashariki ya mbali.Kwa bahati mbaya siku ya siku alikamatwa China akiwa ameteremka uwanja wa ndege huku akiwa amemeza kete za kutosha alizopita nazo salama uwanja wa Julius Nyerere jijini Dar.Baada ya kukamatwa alihukumiwa hukohuko nchini China  kwa muda wa miaka MITANO kwenye gereza moja la wafungwa wa mihadarati lililoko jijini Hong Kong.
Wafugwa waliopo kwenye gereza hilo huwa wanatembelewa na viongozi wa kiroho akiwamo Padri  John Wootherspoon raia wa Australia.Hivi majuzi Padri huyo amekuja nchini Tanzania na kuonana na baadhi ya ndugu na wazai wa wafungwa wa Kitanzania waliofungwa huko kwa kosa hilo.Padr John amesema kuna watanzania zaid ya 130 waliopo gerezani hapo.Padri John alibahatika kuonana na Sandra,naye Sandra alikuwa na haya ya kusema;
Niliposhuka Uwanja wa ndege China ghafla tumbo lilianza kuniuma ndipo nilipokimbizwa kwenye chumba cha ultra sound.nilipofika huko nilibainika nina kete za mihadarati tumboni ndipo nikatiwa nguvuni"Padri John alipomuuliza kwanini alijihusisha na biashara hiyo haramu,Sandra alijibu kwa kifupi tu kwamba "ni kwaajili ya umaskini na tamaa ya fedha za haraka"picha chini ni Padr John akiongea na mmoja wa ndugu wa wafungwa hao jijin Dar hivi karibuni

0 comments:

Post a Comment

Pages