BALOZI WA JAYMILLIONS AHIMIZA WATEJA KUANGALIA KAMA NAMBA ZAO ZIMESHINDA KILA SIKU
Balozi wa Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania
Hilary Daud”Zembwela” (kulia) akisalimiana na Mshindi wa kwanza wa
shilingi milioni 100 kupitia promosheni hiyo mkazi wa Kilolo mkoani
Iringa Uwezo Magedenge (22)mara alipomtembelea hotelini kwake alipofikia
jijini Dar es Salaam kabla ya kukabidhiwa kitita chake wiki iliyopita
na kurudi mkoani Iringa. Mshindi wa kwanza wa shilingi milioni 100 kupitia…
Balozi
wa Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hilary
Daud”Zembwela” (kulia) akisalimiana na Mshindi wa kwanza wa shilingi
milioni 100 kupitia promosheni hiyo mkazi wa Kilolo mkoani Iringa Uwezo
Magedenge (22)mara alipomtembelea hotelini kwake alipofikia jijini Dar
es Salaam kabla ya kukabidhiwa kitita chake wiki iliyopita na kurudi
mkoani Iringa.Mshindi
wa kwanza wa shilingi milioni 100 kupitia promosheni ya Jaymillions
inayoendeshwa na Vodacom Tanzania ,Uwezo Magedenge (22) ambaye ni mkazi
wa Kilolo mkoani Iringa,akiteta jambo na Balozi wa Promosheni hiyo
Hilary Daud”Zembwela” alipotembewa hotelini kwake na Balozi huyo kabla
ya kukabidhiwa kitita chake wiki iliyopita.
Balozi wa promosheni ya Jaymilioni
inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hillary Daud ”Zembwela”maarufu kwa
jina la Zembwela wiki hii alikuwa kivutio kwa wananchi wengi
alipotembelea eneo maarufu la maduka la Mlimani City lililopo jijini
Dar es Salaam ambapo alitoa ofa ya kuwalipia baadhi ya wateja waliokuwa
wananunua mahitaji ikiwemo pia kuwagawia fedha baadhi ya wananchi
waliokuwa katika eneo hilo.
Ziara hiyo ilileta msisimko mkubwa wa
wananchi waliokuwa eneo hilo ambapo baadhi yao walilazimika kuacha
shughuli zao kumwangalia balozi huyo na wengine kuomba kupiga naye picha
ikiwemo waliompiga picha kwa kutumia simu zao zao mkononi.
Zembwela alitumia fursa hiyo kuwaeleza
wananchi kuwa wanaotumia mtandao wa Vodacom wahakikishe kila siku
wameangalia kama namba zao zimeshinda mamilioni ya fedha kwa kutuma neno
JAY kwenda namba 15544 na aliwataka wale ambao hawako kwenye mtandao wa
Vodacom wajiunge nao ili washiriki kwenye promosheni hii kubwa
iliyolenga kubadilisha maisha ya watanzania wengi kuwa mamilionea.
“Leo nimewafuata huku kuwagawia mapesa kwa
maana naona wengi wenu bado hamjachangamkia fursa hii kwa kuangalia
iwapo namba zenu zimeshinda kila siku,bado tunayo mabilioni ya fedha
kwa ajili yenu hivyo changamkia fursa hii muweze kujishindia mamilioni
ya fedha katika kipindi hiki cha promosheni.Kila siku kuna mshindi 1 wa
shilingi milioni 100,000,washindi 10 wa milioni 10 na washindi 100 wa
shilingi milioni 1 hivyo kazi kwenu na Vodacom.Alisema
Naye Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania
Matina Nkurlu aliwahimiza Watanzania na wateja wote kuchangamkia
promosheni hii kwa kuhakikisha wametuma neno JAY kwenda namba 15544 ili
kutopoteza nafasi zao za kushinda pia alisema kuwa njia nyingine ya
kushinda ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544 iwapo simu haina fedha
ambapo mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/-
Alisema kuwa tangu promosheni hii ianze
mapema mwezi uliopita mteja mmoja ameishajishindia milioni 100, wateja
2 wamekwishajishindia milioni 10 na wateja kumi na moja wameisha
jishindia shilingi milioni moja kila mmoja na maelfu wengine tayari
wamejishindia muda wa maongezi.
Wateja wa Vodacom ambao tayari wamejipatia
mamilioni ya fedha kupitia promosheni hii ni Uwezo Magedenge mfanyakazi
nyumba ya wageni wilayani Kilolo mkoani Iringa ambaye amejishindia
milioni 100. Waliojishindia milioni kumi kila mmoja wao Hynes Petro
Kanumba mkulima kutoka Inyonga mkoani Rukwa na James Mangu
mfanyabiashara kutoka wilayani Magu
Washindi wa milioni moja ni Chiphold
Wanjara mjasiriamali wa Kutoka Mwanza ,Janeth Nganyange wa
Njombe,Evarista Minja mwanafunzi kutoka Mwanza,Stanley Bagashe Mwalimu
wa Shinyanga,Ramadhani Maulid Mkulima kutoka Dodoma, ,Lucas Masegese wa
Shinyanga,Ayub Makonde mfanyabiashara wa Mbeya,Hyasinti Mlowe Fundi
gereji kutoka Njombe,Florian Gwayu mchapishaji kutoka Arusha,Modesta
Millanzi mjasiriamali kutoka Peramiho mkoani Ruvuma na Nobert Minungu
mwanafunzi kutoka Mbwanga mkoani Dodoma.
“Promosheni hii itadumu kwa muda wa siku
mia moja hivyo juma hili inaingia katika wiki ya nne na bado kuna
mabilioni ya fedha yamewasubiri watanzania,wanachopaswa kufanya ni
kuhakikisha kila siku wameangalia kama namba zao zimeibuka na ushindi
kwenye droo ya siku kwa kutuma neno Jay kwenda namba 15544.”Alisema
0 comments:
Post a Comment