WEMA AMTUSI SHEMEJI WA ZARI
Stori: Imelda Mtema/Mchanganyiko
KIMENUKA! Beautiful
Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’ amemporomoshea matusi mazito shemeji wa
Zarina Hassan ‘Zari’, King Lauwrance akidai amemuudhi sana kwa kitendo
cha kuvujisha picha inayomuonesha akiponda raha nchini Afrika Kusini
‘Sauz’ na mume wa Zari, Ivan Semwanga, Risasi Mchanganyiko linakupa
mchapo kamili.
Stori: Imelda Mtema/Mchanganyiko
KIMENUKA! Beautiful
Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’ amemporomoshea matusi mazito shemeji wa
Zarina Hassan ‘Zari’, King Lauwrance akidai amemuudhi sana kwa kitendo
cha kuvujisha picha inayomuonesha akiponda raha nchini Afrika Kusini
‘Sauz’ na mume wa Zari, Ivan Semwanga, Risasi Mchanganyiko linakupa
mchapo kamili.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Wema na staa wa Bongo Fleva, Omari
Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ walikwenda Sauz kurekodi video ya wimbo wa msanii
huyo ambao jina lake bado halijafahamika mara moja ndipo baadae picha ya
Ivan, Wema na King Lawrence ilipovuja na kuzua gumzo.TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichokuwa Sauz, baada ya Wema na Ommy kutua nchini humo na ‘project’ hiyo ya video, King Lawrance alidaiwa kuandaa mpango kabambe wa kuhakikisha kwa namna yoyote wanaonana na Wema kisha kupiga naye picha ambayo akiivujisha mtandaoni kila mtu ataamini wamefanya malipizi kwa zilipendwa wa Wema, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye amemnyakua Zari, mke wa Ivan.
Wema Sepetu (kulia) akiwa na mume wa Zari, Ivan Semwanga (wa pili kushoto), King Lawrance akiwa amemkalia mpenzi wake.
“Ilikuwa ni mpango wa malipizi, King na
Ivan walikuwa wanaumia moyoni kumuona Diamond anatoka na Zari wakati wao
wana fedha kuliko Diamond hivyo waliposikia mtoto wa kike (Wema) yupo
Sauz wakasema watadili naye hadi kieleweke, iwe ni kwa kufanikisha zoezi
la kutoka naye kimapenzi au hata kupiga picha ambazo zikisambaa
mitandaoni, watu watajua kwamba wamefanya malipizi,” kilisema chanzo
chetu.
King Lauwrance (kushoto) akipozi na Ivan( aliyekuwa mume wa Zari).KING AFANIKIWA KUIVUJISHA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, baada ya kufanya project, Ommy na Wema usiku walikwenda katika moja ya klabu kula bata ndipo King na Ivan walipozama na kufanikiwa kupata picha na Wema wakiwa katika kochi moja kisha akaitupia katika mtandao wa Istagram.
Wema aliwachukulia kama washkaji, hakujua jamaa walikuwa na lao kichwani, walipofanikiwa kupata picha tu, wakaitupia mtandaoni fasta na kufanya Wema atukanwe na watu,” kilisema chanzo hicho.
WEMA ACHARUKA
Baada ya picha za Wema na Ivan kusambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, mwandishi wetu alimtafuta Wema kwa njia ya simu ambapo alimcharukia King kwa matusi mazito ambayo kimaadili hayandikiki gazetini hata mtandaoni.
Zarina Hassan ‘Zari’ akipozi.Baada ya picha za Wema na Ivan kusambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, mwandishi wetu alimtafuta Wema kwa njia ya simu ambapo alimcharukia King kwa matusi mazito ambayo kimaadili hayandikiki gazetini hata mtandaoni.
“Yule ni...(tusi) ameniboa kweli...(tusi) unajua vitu vingine vya kipuuzi kabisa, wanatafuta kiki zisizokuwa za msingi wa...(tusi)” alisema Wema.Wema alisisitiza kuwa hataki kumzungumzia sana King kwani anaamini akifanya hivyo atamuongezea umaarufu ambao amekuwa akiutafuta muda mrefu.
King Lawrence amekuwa akimtusi Diamond mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii huku akionesha jeuri ya fedha kwa kile kinachoonekana kuumia kwake roho kwa kijana wa Tandale kumchukua shemeji yake Zari, aliyezaa na Ivan watoto watatu.
0 comments:
Post a Comment