MAZISHI YA MRAKIBU WA POLISI CAPT.KIDAI SENZALA ALIYEFARIKI KATIKA AJALI YA HELKOPTA DAR ES SALAAM
Maafisa
wa Polisi wakiwa wamebeba sanduku lililohifadhi mwili wa Marehemu Capt.
Kidai Senzala Kalise aliyefariki Novemba 29 mwaka huu katika ajali ya
Helkopta iliyotokea Kipunguni B-Moshi Bar Dar es Salaam wakielekea
katika makaburi ya familia huko Gonja Maore Wilaya ya Same mkoa wa
Kilimanjaro Desemba 1, 2014.
Maafisa
wa Polisi wakiwa wamebeba sanduku lililohifadhi mwili wa Marehemu Capt.
Kidai Senzala Kalise aliyefariki Novemba 29 mwaka huu katika ajali ya
Helkopta iliyotokea Kipunguni B-Moshi Bar Dar es Salaam wakielekea
katika makaburi ya familia huko Gonja Maore Wilaya ya Same mkoa wa
Kilimanjaro Desemba 1, 2014.
Maofisa wa Polisi wakijiandaa kulibeba jeneza la Marehemu Capt Kidai.
Maofisa wa Polisi wakiwa wamebeba sanduku la Mrakibu wa Polisi-Capt. Kidai.
Heshima za Kihjeshi zikitolewa kabla ya jeneza kushushwa kaburini na kupigiwa mizinga.
Marehemu Kidai
alikuwa Mrakibu wa Polisi na alizikwa kwa heshima zote za Kipolisi ikiwa
ni kupigiwa mizinga na saluti mbalimbali za kipolisi kabla na baada ya
maziko yake.
Helkopta aina ya Robertson R44 iliyo tolewa msaada
kutoka kwa Taasisi ya Howard G. Foundation inayomilikiwa na
mfanyabiashara mashuhuri nchini Marekani Bw. Warren Buffet ililetwa
nchini kwa lengo la kukabiliana na vitendo vya ujangili na kupokelewa
nchini na Waziri wa Maliasili na Utalii June 14, 2014 jijini Dar es
Salaam na kuikabidhi kwa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania
(TANAPA) ilipata ajali majira ya saa nne asubuhi baada ya upata hitilafu
katika injini yake na kupoteza maisha ya Mrakibu wa Polisi Capt. Kidai
Senzala Kaluse, Mkaguzi wa Polisi Capt. Simba Musa Simba, Konstebo wa
Polisi, Josso Selestine na Capt. Joseph Khalfan wa Malisasili aliyezikwa
Arusha.
0 comments:
Post a Comment