Vyanzo vingine vya habari vimeeleza kuwapo pia kwa ajenda ya hali ya siasa inayohusishwa na harakati za urais, hususan kwa vigogo wanaopishana kusaka nafasi hiyo na wale waliotajwa katika kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow.
Kamati Kuu inatarajia kutumia vikao hivyo kuangalia namna ya kupata wagombea watakaokubalika kwa wananchi kuelekea kwenye kinyang’anyiro cha urais, wabunge na madiwani.
Akiwa katika ziara ya kuwashukuru wananchi kwa kuipa CCM ushindi kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mkoani Tanga, Kinana alisema chama hicho kitafanya kikao hicho kwa lengo pia la kupitia masuala mbalimbali yanayokihusu.
Alisema salamu za CCM kwa Watanzania kwa mwaka huu ni ahadi ya kuweka mkazo katika maadili kwa viongozi wake na itafanya tathimini kwa lengo la kujipanga kwa Uchaguzi Mkuu.
Alipoulizwa kuhusu ajenda katika vikao hivyo wiki iliyopita, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alikuja juu na kusema hakuna kitu kama hicho. “Hata mkiiandika vibaya CCM itashinda tu,” alisema hivi karibuni.
Vigogo waliopewa onyo na CCM ni pamoja na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba na mawaziri wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye.
Wengine ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wasira na aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini ambaye ni Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja na waziri waliokumbwa na kashfa ya escrow ni Profesa Anna Tibaijuka na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
|
0 comments:
Post a Comment