Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, akisalimiana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein, wakati wa sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman, leo Jumatatu Januari 12, 2015.
Zanzibar inaadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi, yalioung'owa utawala wa Sultani.
Katika kilele cha maadhimisho hayo ya kushehrehekea miaka 51 ya mapinduzi ya Zanzibar ,sherehe ambazo zilifanyika uwnaja wa amani na kuhudhuriwa na mamaia ya waannchi na viongozi wakuu wote wa Serikali ya Muungano wa Tanzania Na Zanzibar,viongozi wastaafu wakiongozwa na Rais wa Jamhuri Dr.Jakaya Kikwete, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr Ali Mohamed Shein ametangaza kuondoa gharama zote za kuchangia elimu za msingi na sekondari na sasa huduma hizo zitatolewa Bure.
Dr. Shein amesema Serikali ndiyo sasa itakayobeba jukumu la kulipia gharama hizo huku akisema huo ni uamuzi sio mpya ila uliotolewa na muasisi wa Mapinduzi ,Marehemu Abeid Amani Karume.
Dr. Shein ambaye kabla ya hotuba yake , alipokea maandamano makubwa ya wananchi wa mikoa mitano ya Zanzibar ,wafanyakazi wa SMT na SMZ na taasisi za kiserikali na binafsi na Wanafunzi wa vyuo mbali mbali vya Zanzibar pia alielezea hali ya uchumi wa zanzibar ambapo amesema kiwngo hicho cha uchumi kiazidi kuongezeka kila mwaka sambamba na pato la Seriklai hivyo amesisitiza utendaji na ufanisi wa seriklai katika kuwatumikia wananchi.
|
0 comments:
Post a Comment