WALIONASWA KWA MAPENZI YA JINSIA MOJA KUMBE WALIOANA

By
Advertisement

Na Haruni Sanchawa/Uwazi
SAKATA la wasichana wawili warembo, Maua Sadick (24) mkazi wa Stakishari, Ukonga, Dar es Salaam na Lucy Fred (23) mkazi wa Karakata, Dar ambao walishikiliwa katika Kituo cha Polisi Stakishari, Ukonga jijini kwa madai ya kufanya mapenzi ya jinsia moja limechukua sura mpya.
Habari za kipolisi zinasema wasichana hao ambao walifunguliwa jalada kituoni hapo namba SKT/RB/463/2015 baada ya kukamatwa Januari 12, mwaka huu inadaiwa kuwa walioana.
“Zipo picha zinazodaiwa kuwa walioana na wanaonekana wakiwa wanavishana pete nyingine wakiwa wanafungua shampeni kwenye hafla fupi ambayo waliifanya jijini Dar es Salaam,” kilisema chanzo ndani ya jeshi la polisi.
Habari zaidi zinadai kuwa hafla hiyo waliifanyia katika ukumbi mmoja (jina…
Na Haruni Sanchawa/Uwazi
SAKATA la wasichana wawili warembo, Maua Sadick (24) mkazi wa Stakishari, Ukonga, Dar es Salaam na Lucy Fred (23) mkazi wa Karakata, Dar ambao walishikiliwa katika Kituo cha Polisi Stakishari, Ukonga jijini kwa madai ya kufanya mapenzi ya jinsia moja limechukua sura mpya.
Habari za kipolisi zinasema wasichana hao ambao walifunguliwa jalada kituoni hapo namba SKT/RB/463/2015 baada ya kukamatwa Januari 12, mwaka huu inadaiwa kuwa walioana.
“Zipo picha zinazodaiwa kuwa walioana na wanaonekana wakiwa wanavishana pete nyingine wakiwa wanafungua shampeni kwenye hafla fupi ambayo waliifanya jijini Dar es Salaam,” kilisema chanzo ndani ya jeshi la polisi.
Habari zaidi zinadai kuwa hafla hiyo waliifanyia katika ukumbi mmoja (jina tunalihifadhi) ambao upo Chang’ombe na unatumika kwa shughuli nyingi za burudani na hata michezo.“Mimi nilihudhuria sherehe hiyo na picha ninazo ambazo zinawaonesha wasichana hao wakivishana pete na walikuwepo pia waalikwa kama unavyoona kwenye sherehe za harusi katika jamii yetu,” alisema mtu mmoja ambaye jina lake tunalihifadhi.
Mtu huyo alidai kuwa mmoja wa wasichana hao anamfahamu kwa kuwa sasa hivi anaishi kwa dada yake karibu na Uwanja wa Ndege, Karakata nyuma ya msikiti mpya.Mara baada ya kukamatwa wasichana hao, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mogo, Stakishari,George Mtambalike alilithibitishia gazeti hili ofisini kwake kutiwa mbaroni kwao kwa madai ya kufanya mapenzi ya jinsia moja.
Naye Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP Mary Nzuki alisema wasichana hao bado wanapelelezwa. “Ni kwamba kesi yao ipo Stakishari na uchunguzi dhidi yao ukikamilika watafikishwa mahakamani, “ alisema Kamanda Nzuki. 

0 comments:

Post a Comment

Pages